Elections 2015 If you can't beat them, join them! He is the worst dictator. Let's pray for him!

there are Two possible outcomes with Magufuli
1.MAGUGULI BEING ''MAGUFULI''.....
2.A ''REMOTE CONTROLLED'' MAGUFULI


What?Magufuli awe remote controlled? bila shaka haumfahamu Magufuli wewe, Pasco ebu mueleweshe huyu amfahamu MAgufuli, RAis wa Awamu ya Tano wa Tanzania.

Hofu ya wote ikiwemo wana CCM wenyewe ni chama na serikali kutwaliwa, badala ya serikali na chama cha CCM sasa ni serikali na chama cha MAGUFULI.
 
Roho yako inajua unasema uwongo.... Mungu wetu anjua wewe ni Mwongo.....

Unamtaja Mungu wewe ndio unajijua kuwa hakuna anayeweza kusema roho ya mtu ikoje so niache mie unaniita muongo sababu ukweli unauma na kukuchoma.

Acha kutumia na kuweka Mungu wakati hautii anayotaka tuwe...kama ulilofanya kunihukumu kuwa mimi ni muongo.

Sema lingine unajijazia dhambi tu aaaggghhh
 

Hiyo ndiyo iwe agenda kuu katika agenda za UKAWA kwenye Bunge lijalo...otherwise haitakuja kutokea upinzani ukapata Uraisi.
 

IT IS WHAT IT IS.......the future is always uncertain........
badala ya kujiona mjuvi wa mambo,jiulize..''Samia lilikuwa chagua lake?''....Usidhani Urais ni Uwaziri......
 
Kusema ukweli ntakua mnafiki, huenda nisiweze kupigana nao lakini sitaweza kuungana nao kadri niishivyo.
 

That said, what's your take on the majority - those multitudes - who are heedlessly celebrating their heads off for "winning" by carrying the man and his party into office? As for me, I'm at times awestruck watching processions after processions of exhilarated CCM fans dancing their bottoms off for each win and going berserk at the real prospect of the party reigning forever! Obviously, devoid of any due regard to its meaning to their own destiny! Can't help the feeling that I'm out of context with the real Tanzania, a country of zealots! Over 20 years of multiparty system and nothing changes! Sad! Our political processes are certainly doomed to irrationality for ages to come.
 
sio ili mradi dictator .....anatakiwa awe na added values nyingine kama akili ,focus ,vision ....lakini huyu wa kwenu mhm sijui

Huyu ndo rais wa kwanza mwenye PhD ya kusomea, sio ya kupewa. Huyu ndo rais wa kwanza kuingia madarakani akibebwa na rekodi yake. Wewe sijui unapimaje? Hivi huyo aliyekuwa akipigiwa debe na washabiki lukuki tunaweza kupima intellectual capability yake against huyu aliyeshinda? tuwe honest, tusubiri kuona kama performance yake ita reflect hope tuliyokuwa nayo juu yake.

Kusema tu kuwa hana akili, focus, vision - lete vipimo vya attribute hizo ili tuweze kuona kuwa huyo mwingine alikuwa na zaidi kuliko huyo ambaye inaelekea watanzania wengi wamemchagua!
 


Ulichosema ni kweli tupu mkuu.
Mara nyingi wana siasa siyo wa kuamini kabisa. Kwa sababu kile wanachotuambia siyo wanachomaanisha mioyoni mwao. Japokuwa mimi napenda mabadiliko, lakini kwa uzembe huu, ngoja wapoteze tu. Huwezi kuingia kwenye mechi wakati huo ukijua kabisa referee ni mpenzi wa timu unayocheza nayo. Lazima utafungwa tu.
Na kwa mtazamo wangu, kama walivyoanza mapema hivi kupinga matokeo, yawezekana kabisa wakatuingiza kwenye damu za wanyonge kumwagika. Hili nadhani vyombo husika wangelikemea mapema, wasisubiri mpaka damu ya wasiyo na hatia imwagike ndo wachukuwe hatua.

Sisi sote ni Watanzania no matter our political idiology differences.
Hivyo wasituingize huko. Wajipange ndani ya miaka mitano kupigania kuwepo kwa katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi.
 
Msijifanye vipofu wa kutoona jitihada ambazo vyama vya upinzani vimefanya. hivi si mwaka huu mmeona yaliyotokea kwenye katiba hamjui ccm ilikuaka makubaliano ya kufanya marekebisho kwaajili ya uchaguz
 

Uko sahihi mkuu. Lakini amini nakuambia, CCM na serikali yake wasingekubali katu. Badala yake, akina Mbowe wangepigiwa kampeni chafu sana kuwa hawalitakii mema taifa; wanataka kuvunja amani na utulivu - tunu muhimu sana za taifa. KIBAYA ZAIDI, wangekomalia suala hilo, wangejikuta wapweke vibaya sana. Wananchi wengi wasingewaunga mkono hasa baada ya viongozi wao wa dini na wengineo maarufu kuungana na serikali kukemea "hatari inayolinyemelea taifa" tena ikihusisha maadui wa nje wanaoionea wivu Tanzania! Acha CCM itawale milele hadi Watanzania watakapoona haikubaliki. Hapo hakutakuwa na haja ya mtu mmoja au chama kuchukua hatua; watajituma wenyewe tena kwa gharama kubwa zaidi.
 
Least qualified? EXCUSE ME? What are your criteria?
I'd say you have some personal issues with this dude, possibly he's from your rivary tribal neighbourhood, IF YOU ASK ME!
 
Ukweli ni kwamba kwasasa tunahitaji rais dictator ili nchi inyooke.
Pili nafurahi kuona unakubali kuwa "udhaifu" wa magufuli ni mchapakazi.
Tatu, ni vizuri umekubali kuwa ulikuwa una abuse uhuruwako humu JF.
Niongezee tu...watanzania wanafiki sana..nilishasema hili..Kikwete akiondoka watu wataanza kumsifia...
 
tulishwahi kuonya kua nchi haiwezi kuchukuliwa kwa propaganda na uongo uongo mitandaoni, hicho ndio kilichotokea, mkajipange

Ongezea na kupita angani kwa chopa wakati Magufuli alipita kwa Barbara kijiji kwa kijiji sasa leo wanashangaa, waambie.
 

Kwanini hujapiga kura?
 

Hivi ni profesa gani hapa Tanzania anaweza kumfelisha au hata kumvuta shati/gauni waziri anayesoma chini ya uangalizi wake? Hiyo rekodi inayovuma zaidi kwa kelele kwenye media?

Nina hakika hata ndani ya CCM hivi sasa wanahaha jinsi watakavyomweka kwenye mstari huyu jamaa asiwaaibishe!
 
Drifter

Vyama vya upinzani vimekuwepo tangia 1992

Vimeingia kwenye uchaguzi 1995 bila kushirikiana. Je ni kweli walishirikiana katika hoja na kuunganisha nguvu kudai katiba mpya na tume huru tangia 1995?
Kama umezaliwa juzi siwezi kukulaumu.
UKAWA imezaliwa lini?

Je itachukua muda gani kwa upinzani (kama ushirika au umoja) kuwa serious na kuipa kipaumbele na kupigania katiba mpya na tume huru chini ya mwevuli mmoja? Ikiwa kwa jina la UKAWA au lingine. Hawajawahi kuonesha ulazima juu ya suala hii,usiwatetee.

Uchaguzi ukiisha wanasubiri ikiwa imebakia miezi 3 ndio wanakumbuka "ohhh vipi tutakabiliana na Tyson!!??"

Tyson kwa jeuri na kejeli anawaita, "nyie wapumbavu na malofa"

Miaka 20 na usheee hupati katiba mpya au tume huru. Unajiuliza ni kwa nini? na kama CCM itapewa "ushindi" miaka itaongezeka.

Uhuru wa Tanganyika ulipiganiwa na kupatikana katika muda gani watanganyika walipokuwa tayari na serious wanataka uhuru kutoka kwa mwingereza?
 
Lowassa ana mbinu gani? Hapo ndipo mlishindwa kujipambanua kabisa. Mmetumia muda mwingi kumsafisha - muda ghali kabisa ambao mngeutumia kueleza sera zake kwa ukamilifu mpaka watu wakawaelewa. Hamuwezi kukwepa lawama kwa kushindwa kulielewa hili.
 

Who was the most qualified? And lets compare him with Magufuli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…