Elections 2015 If you can't beat them, join them! He is the worst dictator. Let's pray for him!

Tupo pamoja

Hapa kazi tu

Nimechoka dharau za wafanyakazi wengi wa serikali kama vile unachotaka wafanye ni kosa huku ni wajibu wao.

Na bado watanyooka tu

Hivi kitufe cha like kimepelekwa wapi jamani?

Yaani huko kwenye halmashauri ndi maghufuli aanze napo, heshima ya kazi irudi, kitu kidogo njoo kesho, kesho ukirudi humkuti, unakalishwa kwenye benchi masaa, yaani watanyooka tu
 

Tanzania kwa sasa inahitaji 'a democratically elected dictator'. Kikwete kawachekea Watanzania mwishowe wanakaanza kumshika sharubu!
 
Dude! No matter how dissappointed you are, the truth remains Ukawa diverting for Lowassa was a wrong turn, that turns off the majority of the pro revolution, institutional change, regime change you name it, it's pure fact, whether you like or not but atleast deep down you know it!
 

Ndugu yangu unaweza kuwa sahihi kulitazama suala hili kama la vyama na viongozi wao. Na hao wanaweza kuwa na mapungufu yao mengi tu. Lakini mwisho wa yote cha maana ni nini hasa kinatakiwa na wananchi? Wanasiasa na vyama hupata nguvu toka kwa wananchi hasa wanapotaka kufanya mabadiliko makubwa. Nimeona juhudi kubwa zilizofanywa na CHADEMA na, baadaye UKAWA, kutaka katiba mpya zikizimwa na CCM kwa mabavu na wananchi hawakuonekana kujali sana - limeachwa kuwa tatizo la akina Mbowe na wapinzani wenzie. Hata suala la mapambano dhidi ya ufisadi lilichukuliwa hivyohivyo tu - ajenda ya kina Dk. Slaa huku wakidaiwa kutokua na ajenda nyingine ya maana ya kuendeleza nchi zaidi ya kelele dhidi ya ufisadi.

Hawa wapinzani wanafanya kazi katika mazingira magumu sana. Kilichobakia ni kuingia mitaani tu kuhamasisha wananchi wailazimishe serikali ya CCM ikubali marekebisho makubwa ya Katiba ili tuwe na demokrasia ya kweli na utawala bora unaotanguliza sheria bila kuangalia sura. Na wakihubutu kufanya hivyo, utaona jinsi hoja ya kutishia amani na usalama wa taifa itakavyotumika kuwagonga. Kwa bahati mbaya (au nzuri) huko nje Tanzania ina sifa nzuri sana ya amani, utulivu na viongozi "wanaofuata katiba"; hawajiongezei miaka ya kutawala na chaguzi zake zinafanyika kwa maelewano mazuri na kukamilika na muafaka.

Hivyo, kwa watu wachache kujaribu kuishinikiza serikali itende haki si rahisi ilhali wananchi wenyewe bado hawajawa tayari kusimama kidete na wanaoongoza kudai haki hiyo kama ilivyotokea huko Burkina Faso na kwingineko. Ndio maana naona ni bora akina Mbowe wasibinafsishe (personalise) sana hizi harakati za kisiasa. Si kwa manufaa yao binafsi. Kama wananchi wengi bado hawaoni tabu na tena wanapenda kuendelea na mfumo wa CCM, ndiyo demokrasia yenyewe hiyo. Siku wakichoka watasema wenyewe tena kwa HERUFI KUBWA. Sio sasa tunajikanyagakanyaga kujua ukweli uko wapi. Pande zote zinashabikiwa kwa namna isiyodhihirisha ni nini na akina nani hasa wanatakiwa kuleta mabadiliko.

Si sahihi kutumia mfano wa uhuru wa Tanganyika. Hapo ilikuwa tunapambana na dola ya kigeni katika anga za kimataifa. Liliungwa mkono na wananchi wengi sana hasa kwa vile adui alikuwa wazi kabisa - mkoloni (mgeni) tena ana rangi tofauti: nyeupe!
 
I PERSONALLY DONT GIVE A FVCK WHAT THE MINORITY OF THE 'SELF PROCLAIMED INTELLECTS OF TZ' are saying, Tanzanians choosing Magufuli over Lowassa was a very right and wise decision, Magufuli is ahead of Lowassa in terms of all the attributes needed for the top job by a street. He's the best and was the best of all presidential candidates, put aside fanaticism!
 

That's a hell of a joke. Corruption has never been a serious factor in Tanzanians' decision-making psyche. Pro-revolutionary Tanzanians voting for CCM? What institutional and which regime change are they aspiring for in the grand old party of patronage run by masters of fraud and deceit?
 
Majanga yote haya tunayapata kwa sababu ya nyerere kutuachia dictator mkapa, najua wengi hamtanielewa ila baada ya mda ukweli ukidhihirika mtanielewa. Pale Dodoma huyu dictator anahusika, mwanza pale kwa sasa wimbo ni huyu dictator na kule Zanzibar muulize seif atakueleza.
 

Tulikubali vipi kwenda kwenye uchaguzi bila kudai tume huru kwanza???
 
Wanabodi,

John Pombe Magufuli ndiye Mahundi wa urais Tanzania kwa mwaka huu wa 2015-2025!, Kuna walioshindana naye, waliopingana nae, na waliopingana nae!. Kuna msemo usemao, "if you can't beat them, join them!".
.

Mkuu hapo kwenye Blue ulikua unamaanisha Mshindi ama? maana Surname zinatuhusu wengine! Lol
 

We kweli Nyani,kama vipi nenda kaishi uhamishoni Rwanda
 
Jimbo la kilindi: Jumla ya Wapiga kura = 46830
Kura halali = 46830
Kura zilizokataliwa = Hakuna

Matokeo
ACT = 324
ADC = 221
CCM = 33942
CHADEMA = 22123
CHAUMA = 40
NLRA = 31
TLP = 27
UPDP = 22

SASA JUMLISHA MWENYEWE UJIONEE MSHANGAO WAKE.
 
Tulikubali vipi kwenda kwenye uchaguzi bila kudai tume huru kwanza???
Kama unakumbuka katiba mpya ndiyo ilikusudiwa kutumika katika uchaguzi huu lakini baada ya kushindikana ndio wakaamua (JK na Viongozi wengine - John Cheyo Mwenyekiti) kuwa vibadilishwe baadhi ya vifungu kama matokeo kupingwa, tume huru. Mbadilishaji alikuwa ni hili bunge la Makinda, lakini Cheyo akawageuka wenzake. Nadhani hata Mkulu kuna jinsi alivyo 'lielekeza' bunge na ndio maana Mh. Mnyika alivyoleta hii hoja kwa kuomba mwongozo wa dharura spika akaipiga chini!

Na jinsi 'demokrasia' ya Tanzania ilivyojaa usaliti mambo ndio yakawa yamekwama. Hata kama UKAWA wangelijitoa kwenye uchaguzi, akina Dr. Slaa na Prof. Lipumba (ambao tulijua rangi zao baadae) wangefifisha hizo move kwa kuchukua forms. Lakini pia ungelishangaa ACT kwa kushirikiana na akina Dovutwa ikisema 'sis tunaenda kwenye uchaguzi'. Kwa maana hiyo kilichofanyika ni busara.

Kuokoa nchi hii ni wananchi wenyewe kwa wingi wetu kudai tunachostahili bila kutegemea viongozi wa vyama bali kushirikiana nao! Joining them kama unavyotaka kutuaminisha utakuwa ukichaa mwingine!

 
Hapa Kazi tu ndio jambo jema kwa Tanzania. Ule wizi wa maofisini na kufumbiwa macho, utayeyuka punde atakapo ingia IKULU. Wengi walizoe kuiba na kufanya yao, lakini kama kufuata sheria na kuwaweka Lupango kwako ni Udiketa, basi na iwe hivyo. Hiyo ndio lugha pekee Mtanzania ataelewa na kunyooka.

Mimi napenda Dikteta tena awabane mafisadi wote kama alivyo sema, without kujali fisadi ni nani? Si, unamkumbuka Hayati Sokoine? Unakumbuka Muziki wake wa WAHUJUMU Uchumi/ Naama MUZIKI huo sasa utaupata kwa Dkt Magufuli na atawanyoosha wengi sana.

Hakuna jinsi nyingine zaidi ya kuwaweka Lupango wezi wote wa UFISADI, ili iwe FUNDISHO kwa wengi kuwa HAPA KAZI TU, anasimamia sheria na haki. Haki huwa mbaya kwa mvunjaji wa sheria ndio maana unamuita Dikteta.

SUBIRINI MUZIKI wa Magufuli, Kama huto weza kuucheza, ni bora uhame nchi.

Hapa Kazi Tu

Mungu Mbariki Dkt Magufuli.
 
Go to the moon. Kule hakuna CCM utaishi upendavyo na utafanya upendayo.
 
Jimbo la kilindi: Jumla ya Wapiga kura = 46830
Kura halali = 46830
Kura zilizokataliwa = Hakuna

Matokeo
ACT = 324
ADC = 221
CCM = 33942
CHADEMA = 22123
CHAUMA = 40
NLRA = 31
TLP = 27
UPDP = 22

SASA JUMLISHA MWENYEWE UJIONEE MSHANGAO WAKE.

Hacha kupotosha umma. Matokeo sio hayo yaliyotangazwa na tume. Angalia hapa matokeo halisi.

https://m.youtube.com/watch?v=NQFWV2JWQd8
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…