Elections 2015 If you can't beat them, join them! He is the worst dictator. Let's pray for him!


Andika vizuri.
 
Aaagh unamuita kilaza aaagghh basi tumia usafiri wa anga maana barabara za kilaza zitakumeza.

Nyie ndio mnaoshinda mnakulwa rushwa kutumikia wananvhi sasa mnalo.

Kama vile hizo barabara hazimezi watu sasa hivi......

Unakumbuka ile ajali ya basi kutokana na shimo la barabarani, kwenye barabara 'mpya'?
 
Tusitishane hapa. Akiwa rais afanye kazi kwa mujibu wa katiba. Hii habari ya kunyenyekea binadamu mimi huwa sina & inanichefua sana. Kila mtu ataendelea na majukumu yake, tofauti ni kuwa wengine ni viongozi na sisi ni raia wa kawaida.
 

You real make sense brother
 

we pimbi kweli...!!!
 

Sijui hizo takwimu umezitoa wapi, na sijui ina vigezo gani...

Lakini yawezekana kuwa ni hisia tu, hivyo sio fact!!
 
kama Nyerere na kina Kambona wangekua na mawazo hayo basi leo tungekua chini ya wakoloni....yaani wewe huna msimamo ni bendera fuata upepo...siku zote jasiri husimamia unachokiamini mfano mzuri ni Maalim Seif kwa miaka 20 bado anapigania haki za watu wake...
 
Mimi ndio nimekuuliza, ina takwimu/vigezo gani kuona kuwa mgombea wa ccm wa mwaka huu ni "least qualified"...

Sihitaji takwimu wala vigezo vyovyote vile kuona kuwa mgombea wa CCM wa mwaka huu ni bomu kwa sababu hayo ndiyo maoni [ninavyoona] yangu.

Halafu wala hukuuliza. Umetoa kauli tu.

Sasa nikuulize wewe: unajua tofauti ya kauli na swali?

Manake uliandika hivi: "Sijui hizo takwimu umezitoa wapi, na sijui ina vigezo gani..."

Unasema wewe ndiyo umeniuliza. Ulipouliza ni wapi hapo?

Unauliza swali kwa kuandika "Sijui hizo takwimu umezitoa wapi, na sijui ina vigezo gani..."?

Na kwa nini nihitaji takwimu kuona kwamba Magufuli ni bomu?

*Ona jinsi ambavyo maswali huulizwa.*
 

Hukusema kuwa ni maoni yako, rudi kwenye bango lako ujisome tena. Labda kwa vile kingereza changu sio kizuri, lakini kwa uelewa wangu ulifanya generalization, kitu ambacho sio kizuri(kwa maoni yangu).

Kuuliza sio lazima uweke alama(?), maelezo tu kama yangu yanaweza kutosha kuwa swali na likahitaji majibu.

Ili kuthibitisha kauli yako, ni vizuri kutoa vigezo/maelezo ili kulinda hoja yako, kwa nini Magufuli unamuona "least qualified"? Hilo umeshindwa/hutaki kunijibu.
 

Anhaa...kama ambavyo kuuliza si lazima umalizie kwa kuweka alama ya kuuliza baada ya sentensi basi hata kutoa maoni yangu si lazima nianzie au kumalizia kwa kuandika 'haya ni maoni yangu'.

Ili kuthibitisha kauli yako, ni vizuri kutoa vigezo/maelezo ili kulinda hoja yako,

Sihitaji kuthibitisha kauli ya maoni yangu kwa sababu maoni yangu ni yangu na yanabaki kuwa yangu. Kama hukubaliani nayo, basi unakaribishwa kufanya hivyo.

Lakini mimi silazimiki kuyathibitisha hata kidogo.

kwa nini Magufuli unamuona "least qualified"? Hilo umeshindwa/hutaki kunijibu.

Sijashindwa kulijibu. Nimekujibu lakini pengine jibu langu si jiibu ambalo unalitaka wewe.

Sorry, can't help you with that.
 
Tatizo lenu mlifikiri nchi hii wapiga kura ni madereva wa bodaboda peke yao. Mkawapa na viroba ili wakatukane na kuzomea nguo za kijani. Kwa sasa sijui watajificha wapi. Acheni siasa za Ghilba na uongo. Watanzania wanaujua uongo wakiusikia. wewe umeahidi kila kitu buree na bado ukapoteza its a shame!!
 
Anhaa...kama ambavyo kuuliza si lazima umalizie kwa kuweka alama ya kuuliza baada ya sentensi basi hata kutoa maoni yangu si lazima nianzie au kumalizia kwa kuandika 'haya ni maoni yangu'.
..Hata mimi sijasema popote kuwa ni "lazima" uandike hivyo. Lakini katika uandishi, maneno kama "nadhani, nafikiri, naamini" hutumika kuonyesha kuwa alisemalo mhusika ni maoni binafsi, anaposema "ni ukweli usiopingika, takwimu zinaonyesha" hii humaanisha kuwa ana uhakika toka vyanzo vilivyothibitishwa kisheria au kitakwimu.



Nimekusoma kiongozi!!
 
..Hata mimi sijasema popote kuwa ni "lazima" uandike hivyo.

Naam, hata mimi sijasema kuwa wewe umesema kuwa ni 'lazima' kuandika hivyo.

Lakini katika uandishi, maneno kama "nadhani, nafikiri, naamini" hutumika kuonyesha kuwa alisemalo mhusika ni maoni binafsi,

Hiyo ni kweli. Lakini kumbuka kwamba humu ndani si mara zote watu hufuata kanuni za uandishi hususan pale ambapo tunapokuwa tunachangia maoni yetu. Na ndo maana wakati mwingine unaweza ukaona mtu kaliandika jina la mtu fulani kwa herufi zote ndogo, kaandi kwa kutumia mikato, kaweka 'x' badala ya 's' na kadhalika.

Kwa hiyo, nami nilipokuwa naandika yale, nilifanya hivyo kama mtoa maoni tu juu ya kile kilichokuwa kimeandikwa na mwanzisha mada. Sikuwa naandika makala rasmi wala sikuwa naandika kuhusu habari.

Setting ya humu, hususan kwenye uchangiaji mada, ni informal. Wakati mwingine watu tunatiririka tu bila kufuata kanuni za uandishi zinazotumiwa kwenye formal setting.

Sasa, unless mtu uwe unataka ligi tu kwa kutafuta kasoro katika mabandiko ya wengine [jambo ambalo hata mimi nakiri huwa nalifanya hapa na pale], lakini kwa kiasi kikubwa watu huwa tunachangia mada kwa kutoa maoni yetu ambayo mengine kwa kweli huwa hayana misingi yoyote katika ukweli au uhalisia kama wa takwimu, na kadhalika.

anaposema "ni ukweli usiopingika, takwimu zinaonyesha" hii humaanisha kuwa ana uhakika toka vyanzo vilivyothibitishwa kisheria au kitakwimu.

Kaka, ya humu yachukulie hivyo hivyo tu wakati mwingine. Kama ningekuwa naleta taarifa rasmi au naandika andiko rasmi basi nisingekuwa na budi ya kufuata hizo kanuni. Hilo nalitambua kabisa kwani hata mimi ni 'trained journalist', just in case you didn't know.

Nimekusoma kiongozi!!

Nami nimekusoma na nadhani sasa umenielewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…