If your life was a book, What would the title be?

If your life was a book, What would the title be?

Ni lazima tittle iwe ya kidhungu??
Mana naona mnajiachia tu sisi wa mloganzola A mmetusahau

Neno "tittle" ni Lugha gani?.

Sanaa ni Lugha. Lugha ni ainisho ya maisha katika utamaduni wowote ule Ulimwenguni.

Kuanzia kiingereza, kichina, kifaransa, kireno, kijerumani, kijapan na orodha inaendelea. Wote hujivunia Lugha zao. Tatizo hapa ni "Utumwa mamboleo".

Binafsi ningependa jina "Tafakuri Ya Dahafrazeril".

Asalaam.
 
Heshima kwako Mkuu,

Nitajaribu kugusia matumizi ya lugha zinatumika katika Taifa letu la Tanzania.Elimu yetu hutumia lugha mbili nikimaanisha Swahili na kiingereza,katika ngazi ya msingi miaka 7 Nadhani saizi wamepunguza imekuwa miaka 6(Sina taarifa sahihi kuhusu hili) lugha ya kufundishia imekuwa ni kiswahili,kisha Elimu ya upili ni kiingereza mpaka Elimu ya juu.

Kwangu Mimi hili naliona halijakaa vyema kwanini tusichague lugha moja ya kufundishia ama kiswahili au kiingereza kutoka ngazi ya chini mpaka ya Juu..?.walau basi watu wengi tuweze kuzungumuza lugha moja kwa ufasaha,Manaake utakuta mtu ana PhD lakini lugha zote mbili zinam'piga chenga(na hapa ni wasomi wengi tu wanachemuka) pia na heshimu juhudi binafsi za mtu mmoja-mmoja

"Utumwa Mambo Leo" nimekunukuu hapa.Nadhani hapa watu tubadilike na tuibadilisha jamii Mtu anayezungumza kiingereza anaonekana ndio bora(kiakili) jambo ambalo siliafiki,au kuona lugha moja ni bora kuliko nyingine.

Fikra sahihi huja kwa lugha sahihi.

Wewe unamaoni gani kuhusu lugha ya kufundishia Elimu katika ngazi zote...??

Ahsante!!!
 
Back
Top Bottom