Fikra sahihi huja kwa lugha sahihi.
Wewe unamaoni gani kuhusu lugha ya kufundishia Elimu katika ngazi zote...??
Niombe radhi kwa
Ultimate . Hapa si pahala pa kujadili hili la Lugha.
Kujadili “Lugha ipi itumike kufundishia-Tanzania” ni kukaribisha njaa. Kuzungumzia hili inabidi uwe umeshiba-ama uwe na Mkate pembeni. Sasa nimeshiba, tunaweza kujadili.
Lugha ni sauti za nasibu ambazo wanajamii wamekubaliana kwa dhati zitumike katika Mawasiliano-Tafsiri ya Lugha. Pia Lugha ndiyo kioo cha utamaduni wa umma na ainisho kuu la Taifa na watu wa popote pale duniani.
Kila Jamii ina Lugha yake. Kila Taifa lina Lugha yake. Ni udunya na maradhi ya kujitakia kuacha-ama kudharau Lugha yako. Na dharau hizi zinaendana na kutokujiamini, ujinga na kuzingatia mapokeo pasina kuchuja. Kipi ni sahihi-kipi si sahihi. La kusikitisha zaidi, mpaka leo kuna baadhi wanaodhani wengine / chochote cha wengine ni bora kuliko chao. Huku ni kuudunisha U-Mungu ndani yetu.
Kuanzia Wafaransa, Waswidi, Wafini, Wanorwey, Wadenish, Waingereza, Wachina, Wakorea, Wareno, Wajerumani na kadhalika huzungumza na kusoma kwa Lugha zao. Katika Masomo na Nyanja zote-Lugha zao ndizo hutumika. Nadhani hili hutokana na kupevuka kwao.
Haya Mataifa makubwa ambayo yamezitawala Nchi zetu Kiuchumi, kisiasa na hata kiutamaduni wanaelewa fika kuwa Lugha ndiyo kioo cha utamaduni wowote ule Ulimwenguni na ndiyo maana yamekuwa yakipigania ufundishaji wa Lugha zao-hususan Kiingereza na Kifaransa.
Aibu ni kwamba Waafrika-Watanzania wengi hawaoni kuwa ni haki yao kutumia Lugha zao katika Nyanja zote-pasina kuacha kujifunza Lugha zingine za dunia. Waingereza wana British Councils, Wachina wana Confucious Institutes. Nadhani hapa tunaonge lugha moja- umenielewa tafsiri yake.
Baadhi tunaodai kuwa Kiswahili ni Lugha ya Taifa dogo/changa, si lugha ya kisasa-haijitoshelezi ni washenzi (kumradhi kwa tafasiri ya hovyo) na ni watu wenye kasumba nilo-iita “Utumwa Mamboleo” ulojificha nyuma ya pazia la Utandawazi-utandawizi (kama Prof Chachage alivyopenda kuita).
Tatizo kubwa la “Wasomi Mamboleo”-Kitabu changu kilichochopo njiani, ni kwamba hawajuia kuwa vita dhidi ya lugha za Kiafrika ina historia ndefu sana. Mbaya zaidi hatupendi kufukua kaburi hili-
so sad kwakweli.
Hakuna Taifa lolote duniani lililopiga hatua kimaendeleo pasina watu wake kutumia Lugha yao. Na sijui kwanini tunadhani kuwa hili linaweza kuanzia kwetu. Huku ni kujiloga ndugu. Mgomba ukikatwa-watoto huchipua. Moto ukizima-hujifukia kwa majivu. Tuwe migomba, tusiwe kama moto.
Ulishawahi kujiuliza ni kwanini wamishenari waliamua kuutangaza Ukristo kwa Lugha ya Kiswahili?. Waarabu kwa Lugha ya Kiswahili?. Sasa kwanini katika Elimu zote hawataki tutumie Lugha zetu na kutung’ang’aniza kutumia Lugha zao?. Mbali zaidi-wanatuwekea mpaka vikwazo vya hovyo kweli. Eti tuisipofundisha kwa kizungu na Kifaransa hawatotupa misaada. Dah, inauma sana.
Ndugu
Alisina , Kujifunza kwa Kiswahili ni kupata elimu. Kujifunza kwa Kingereza, kifaransa ni kujifunza Lugha.
Nadhani nitoshe kusema hivyo-Lugha ya Kiswahili itumike katika Elimu-Taifa zima.
Karibu..