Ifahamu Al Ahly watakaomenyana naSsimba SC

son of a teacher

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2017
Posts
541
Reaction score
1,449
1.Thamani ya kikosi cha Al Ahly ni Tsh Billion 89.3 huku thamani ya washambuliaji tu ikiwa ni Billion 50.3 wakati kikosi kizima cha simba sc kina thamani ya Bilion 1...Je Beki Sergi Wawa,Juko wanaweza kuzuia Washambuliaji hawa wenye thamani ya Billion 50 wasifunge magoli 5?

2.Klabu ya Al Ahly imecheza fainali ya CAF mara 2 mfululizo.Mwaka jana walicheza fainali na Esperance ya Tunisia na kushindwa na mwaka 2017 walicheza fainali na Wydad casablanca na kushindwa pia mwaka 2015 walicheza nusu fainali na mwaka 2014 walibeba taji la shirikisho na mwaka 2013 na 2012 walibeba taji la CAF mara 2 mfululizo wakati huo huo klabu ya simba hii ndio mara yao ya kwanza kushiriki michuano ya CAF ndani ya miaka 5..

3. Al Ahly ndio klabu ya pili yenye mafanikio zaidi kwenye michuano ya kimataifa duniani wakiwa nyuma ya Real Madrid yenye mataji 26 huku Al Ahly wakiwa na mataji 24.

4.Al Ahly ndio timu pekee inayoongoza kuwa na mataji mengi ya CAF champions league wakiwa na mataji 8 na rekodi ya makombe 4 ya African super cup.

5.Klabu ya Al Ahly imemsajili msimu huu kiungo mshambuliaji Hussein El shahaat kutoka klabu ya Al ain kwa rekodi ya ada ya uhamisho ya dollar 4.5 Million.El shahaat anatoka Al ain akiwa amecheza michezo 33 na kufunga mabao 15 na kutoa assists 17....Binafsi kwenye mchezo kati ya Al ahly na Vita club huyu player El shahaat nilimtizama alisumbua sana ni mbunifu na mara nyingi hutembea na mpira vigumu kupokonywa.

6.Al Ahly imemsajili mchezaji Mohamed mahmoud kutoka klabu ya Wadi degla kwa Dollar 1.5 Million .Kinda Mohamed anatanabaisha ya kuwa vilabu vya Hoffenheim,Fc Basel na Ajax vilimtaka lakini alivitolea nje licha ya mchezaji wa liverpool Mo salah kumshauri akubali kwenda basel lkn mohamed alikataa na kwenda klabu ya ndoto yake Al Ahly.

7.Al Ahly imemchukua kwa mkopo mchezaji wa timu ya Huddesfield inayoshiriki ligi kuu uingereza Ramadan sobhi.

8.Al Ahly ina wachezaji tishio kama El shahaat,sobhi,walid,marwan na Al ahly wanasifika kucheza pasi fupi fupi na kwa kasi.

9.Al Ahly ndio klabu yenye mashabiki wengi Africa na ni klabu yenye mashabiki wenye amsha amsha na makelele mara nyingi sana vilabu vikienda Misri huchachawa na makelele na amsha amsha za mashabiki na hupelekea kufungwa idadi kubwa ya magoli ..Al ahly kwa lugha ya kiswahili humaanisha taifa hivyo klabu ya Al ahly ni kama timu ya taifa huko misri na ndio maana ina wanachama na mashabiki wengi mno



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fainal 2 mfululizo maana yake pale Simba hatutoki kwa soka afrika.
Ngoja tuone checheme yetu hata sare inakuwa ngumu kupata...daah
 
Hao Al Ahl sio mara ya kwanza Simba kucheza nao walisha cheza na Simba mara kadhaa hata mara ya mwisho walicheza na Yanga na kuifunga Yanga kwa tabu pia kumbuka kipigo alichopata Simba jana dhidi ya As Vital kitawafanya Simba kujiuliza na kuongeza umakini
Pia kumbuka wanaocheza ni wachezaji sio hela, kwani kikosi cha Simba katika league kuu Tz Bara mbona kinakua challenged na timu zenye usajili wa bei nafuu mpira haupo hivyo
Nakushauri ukae chini uandike tena uchambuzi wako upya kwani hili andiko ni takataka katupe kwenye dustbin

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Upo vizuri kamanda, big up!
 
Mafisi FC wakibanwa lawama zote Yanga Je kwa sababu kocha msaidizi wa vita Raul Shungu aliwahi kuinoa Yanga na mara zote kuitwanga Simba ndiyo iwe nongwa? Basi bora Fisi Fc wakate rufaa Kamati ya masaa 72 ya CAF na wakishindwa waende FIFA!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…