KAMA UNA MTAJI NA UNATAFUTA BIASHARA YA KUFANYA?
Umeshawahi kufikiri kuhusu biashara ya spea za pikipiki na bajaji?
Hii ni moja kati ya biashara zinazokua kwa kasi sana, kwani maelfu ya vijana wamejiari kwenye boda boda na bajajiIdadi hii inaongezeka siku hadi siku, hivyo kufanya idadi ya pikipiki na bajaji kuongezeka mara dufu siku hadi siku.
Jambo hili limepelekea uhitaji wa vipuli kuwa mkubwa zaidi. Na hii imekuwa ni fursa kwa watu wengi wenye uwezo wa kuuza spea kwa jumla ama rejareja.
Biahsara ya spea za pikipiki huhusisha kuuza vipuli vya pikipiki jumla au rejareja.
(Sehemu ya pili ya chapisho hili itafafanua zaidi)
KWANINI TUWEKEZE KWENYE BIASHARA YA SPEA ZA PIKIPIKI NA BAJAJI?
1. Inahitaji mtaji wa kawaida sana, na ni biashara inayokua kwa kasi zaidi, na ni future (bado inahitajika sana maana pikipiki na bajaji kila siku vinazidi kuongezeka hivyo itazidi kuwepo).
2. Bidhaa nyingi haziharibiki kabisa, kuisha muda wa matumire (expire) wala kupitwa na wakati. Spea Zina uwezo wa kukaa miaka kadhaa hata zisipouzika. Bidhaa inayoharibika/isha muda wake kwa wepesi ni oil ambayo ina life span ya miaka mitano.
3. FAIDA, biashara hii ina faida nzuri. Faida hii hufikia kari ya 35% mapka 70% ya mauzo ya bidhaa, kulingana na bidhaa husika.
Faida hii ni ya uhakika kabisa ukipata eneo zuri.
ENEO GANI HUFAA ZAIDI KUFUNGUA BIASHARA HII.
Ikiwa unataka kuanza biashara ya Spea za pikipiki na bajaji kwa Jumla, maeneo ya mijini human zaidi. Hata hivyo eneo la kando ya mji linaweza kuwa rafiki kama lina msongamono ama ni njia ya kuelekea mji mwingine.
Eneo hili ni muhimu liwe la wazi ili iwe rahisi kuonekana na wateja, pamoja na kufikika.
Biashara ya rejareja hutegemea zaidi eneo lenye msongamano na uhitaji wa spare, kama idadi ya watumiaji wa pikipiki ni wengi basi unaweza kufungua.
BIASHARA HII HUHITAJI ZAIDI MAMBO YAFUATAYO
1. Utafiti wa kutosha kuhusu aina ya pikipiki kwenye eneo husika.
2. Mahitaji ya eneo husika na wateja gani unawalenga zaidi (target customers).
3. Bei nzuri, ukilinganisha na wauzaji wengine.
4. Ma/fundi mzuri.
MTAJI
1. Biashara ya spea za pikipiki na bajaji huhitaji mtaji wa kawaida sana kuanzia milioni 4 (avarage) hadi milioni 30 na kuendelea (Rejareja). Hata hivyo mtaji mkubwa zaidi hukupatia faida zaidi kwani Kuna punguzo kwa Kadri unavyofungasha bodhaa nyingi zaidi.
2. Kwa Duka la jumla huanzia milioni 25, hata hivyo hakuana kiasi rasmi hivyo kiasi hicho ni makadirio. Kwa kiwango hicho cha fedha unaweza kuchagua kuuza bidhaa za aina filani tu, kutokana na mahitaji ya eneo lako. Lakini kupata duka zuri la Jumla lenye bidhaa nyingi na toshelevu kunahitaji zaidi ya milioni 100...
Itaendelea sehemu ya pili...