Ifahamu biashara ya spea za pikipiki na bajaji (Sehemu ya Saba...)

Ifahamu biashara ya spea za pikipiki na bajaji (Sehemu ya Saba...)

Jvei

Member
Joined
Jul 13, 2025
Posts
42
Reaction score
69
BIASHARA YA SPEA ZA PIKIPIKI, UZOEFU, MAHITAJI NA MIHEMKO YA JAMIII.

Habari ndugu msomaji,
Siku za karibuni kumekua na muamko mkubwa sana watu wengi wakivutiwa sana na biashara biashara ya spea za pikipiki na bajaji.

Hata hivyo mvuto huo unekuwa na changamoto kadhaa, mafanikio kwa wenye kujituma na wenye nia ya dhati, Ila imekuwa majuto na maumivu kwa waliofwata mkumbo.

Biashara ya spea za pikipiki kama zilivyo viashara nyingine, ni mchakato. Mchakato huu una sehemu kubwa tano, Yaani;
1. Wazo
2. Msukumo wa ndani binafsi.
3. Maarifa
4. Umuhimu/Uhitaji/Soko
5. Kuanza Biashara.

Unaweza usipitie hatua zote tano, lakini walau Tatu ukawa nazo.

🎯Hakikisha kabla ya kuanza biashara ya Spea za pikipiki, Umechuja hilo wazo kwa umakini mkubwa na limekufaa.

🎯Hakikisha una msukumo wa ndani, unaiona fursa kwenye kuuza spea za pikipiki na sio kuhadithiwa tu na mentor wako au kuangalia machapisho na Videos za mainfluesa.

🎯Hakikisha unapata maarifa sahihi kutoka kwa watu sahihi (Watu wengi hupenda kupewa elimu za bure). Tafadhali, lipia elimu. Uwekezaji na mtaji mkubwa ni maarifa, hakikisha maarifa unayopewa uneyalipia ni sehemu ya mtaji.

🎯Maarifa haya yatakufungua kuona kama Kuna umuhimu au Uhitaji wa spea. Utaliona soko kupitia kwenye maarifa utakayopewa. Au utaweza kulitafuta soko baada ya kupata maarifa sahihi ya biashara.
Watu wengi wanafikiri ukishakuwa na Mtaji, frem na mzigo basi umemaliza kazi. Biashara hii inahitaji jicho la kuona wateja na jinsi ya kutengeneza wateja wengi zaidi.

🎯Mwisho baada ya mambo manne ya mwanzo, sasa unaweza kuanza biashara yako na kupanga mipango na mikakati ya uendeshaji.

Biashara ni sawa na mtoto wako uliyemzaa, hakikisha unajua namna ya kumlea na sio kutegemea influencer wakulelee. Au ajiri mtaalamu akuendeshee biashara yako.

📍Je, Nilazima niwe na uzoefu?
Hapana, si lazima. Hakuna aliyezaliwa na uzoefu, wote tunapata uzoefu tukishajiingiza tayari na kujihusisha na biashara fulani.

Hata hivyo ni vema na busara kubwa kuwa na mru mzoefu wa kukuongoza, NDIO unahitaji mtu mwenye uzoefu kwaajili ya kukuongoza ili kuounguza hasara.

Uzoefu sio Elimu, unaweza kupatiwa maarifa kwaajili ya kuzijua A,B,C.. za biashara. Lakini huwezi kupatiwa uzoefu, uzoefu utapata kwa Kadri utakavyokuwa unajifunza kwa vitendo siku hadi siku.

🎯Kwa wafanyakazi, waajiriwa, watu walioko busy, wakati sahihi wa kuanza biasharahii ni kipindi cha likizo. Hii itakupq nafasi ya kuhusika kwenye michakato ya uanzishwaji na uendeshwaji wa biashara yako na kukufanya uwe mzoefu.

Hata hivyo, si lazima kukihusisha moja kwa moja, unaweza kuajiri watu wenye ujuzi wakafanya kila kitu kwaajili yako ukawa unawalipa.

🎯Biashara hii inalipa kiasi gani?
Biashara ya spea za pikipiki ikiwa imepangwa vizuri na ikafanyiwa uwekezaji dhabiti basi inalipa vizuri....(Itaendelea...)

Wasiliana nasi kwa ,
Whatsapp +255787942757
 
Back
Top Bottom