JINSI YA KUFANYA BIASHARA YA SPEA ZA PIKIPIKI NA BAJAJI REJAREJA REJAREJA
⚙Mambo Muhimu zaidi ya Kuzingatia kabla ya kuanzisha Biashara ya spea za pikipiki na bajaji rejareja🎯
Ukitaka kuanzisha biashara ya spea za pikipiki na bajaji ni rahisi sana, ila inahitaji msingi thabiti na msimamo mahirI.
Biashara hii kama moja ya biashara zinazokuwa kwa kasi zaidi Tanzania na nje ya mipaka ya Tanzania, imekuwa na ushawishi mkubwa. Hata hivyo watu wengi hujikuta wakifunga biashara zao ndani ya miezi 6 hadi 12. Kwa sababu mbali mbali.
Kabla hujaamua kufanya biashara hii ni muhimu zaidi kuzingatia mambo ya fuatayo:
1. Kufanya tafiti ya kina kuhusu soko.
a. Wengi wanafikiri biashara hii inaweza kufanyika popote tu, si kweli. Mfanyabiashara anatakiwa kutafiti soko lake vizuri. Biashara ya spea ni biashara-huduma, hivyo ni muhimu kupima uhitaji wa huduma hii katika eneo husika kabla ya kuweka mtaji wako.
b. Utafiti huu unatakiwa kuhusisha pia kiwango na uwezo wako wa kuhudumu na ubora wa huduma unayotaka kuitoa (mfano: eneo lina maduka mengi ya spea lakini wanachelewa kufungua, wanawahi kufunga, Kuna spea za aina flani hawana, hanauza garama kubwa sana, customer service mbaya, hawana mafundi wazuri, n.k).
Ni muhimu kuona nafasi ambayo wengine hawajaona, ama upenyo ambao bado haujafikiwa.
Ukitaka kuanzisha biashara hii ni lazima uwe na vitu vyakwenda kutibu/changamoto za kwenda kutatua. Maana hiki ndio kitakufanya upokelewe vizuri soloni.
2. Unapaswa kuwa na uelewa wa ujumla kuhusu biashara ya Spea za pikipiki na bajaji.
Uelewa wa jumla ni muhimu sana, yaani unapaswa kuwa na ABC... hii itakusaidia sana kwenye usimamizi wa biashara yako. Si lazima uwe mjuzi sana, unaweza kubobea taratibu ukiwa umekwisha kuanza.
3. Unapaswa kuwa na Mtaji, eneo zuri la biashara, pamoja na Kujua Machimbo ya kufungashia mzigo:
Mjadala uliopita ulijikita sana kwenye mtaji hivyo sitajadili sehemu hiyo, badala yake nitajadili eneo kwa udogo, na Machimbo.
a. Eneo la biashara,
Spea za pikipiki na bajaji zinahitaji eneo zuri, yaani la wazi, linalofikika, na linaloonekana na liwe karibu na barabara kubwa (main road). Lengo kuu ni kujitega sehemu amabayo ina movement ya watu mbali mbali na kupeleka huduma hii ambayo kwako ni biashara. Frem inapaswa kuwa na eneo la ziada kwaajili ha mafundi, angalau kuwe na nafasi ya kupaki pikipiki 10, na bajaji walau 2 kuendelea.
b. Fahamu Machimbo ya spea,
Hii ni mada pana sana, ila nitawapitisha kwa udogo tu. Tukipata nafasi tutachimba zaidi,.
Ni muhimu sana kujua machimbo ya spea kabla hujaamua kufanya biashara hii. Kwani ndio huamua faida katika biashara yako na ushindani dhidi ya wafanyabiashara wengine wa rejareja.
Wapi umenunua mzigo, itaamua uuze bei gani na kuleta bei shindani mtaani.
Si hivyo tu, Bali hata ubora wa spea zenyewe huamuliwa na machimbo. Hivyo hili ni eneo muhimu sana kuzingatia.
Rai yangu ni kwamba, ni vema kuingia ukishajua japo kwa uchache, kwakuwa huwezi kujua kila kitu ukiwa nje ya circle ya biashara husika, ukitaka kujua mengi inabidi uingie ujifunze kwa vitendo, sio stori za mitandaoni na vijiweni.
4. Unapaswa kuwa na fundi/mafundi,
Kwenye duka la spea za pikipiki na bajaji za rejareja ni muhimu sana kuwa na fundi, wakati mwingine ni muhimu zaidi umpate na msaidiane kupanga mipango na kuandaa oda (vitu vya kununua) kabla ya kufungua. Uzoefu wake utakusaidia sana.
Fundi mzuri na si fundi tu, anahitajika sana kwaajili ya kutengeneza pikipiki/bajaji na kufanya service pale wateja wanapohitaji.
Kuna muda fundi ni kama kondakta wa daladala, yeye ndio huita wateja. Na huduma za fundi+bei za dukani zitafanya wateja warudi tena na tena au waende sehemu nyingine.
Malipo ya fundi, (mada hii itajadiliwa sehemu inayofuata).
5. Unapaswa kuacha biashara za mtandaoni, na kuingia mtaani kupambana.
Jambo hili limekuwa halisemwi na watu wengi, hili ndio jambo muhimu zaidi. Kama una mtaji, umepata elimu kiasi kuhusu biashara hii, na umehamasika kuifanya. Basi ni vema ukaingia mtaani, kufanya research zaidi na kupambana na mazingira halisi.
Hakuna biashara yoyote unaweza kuelekezwa mtandaoni, kufundishwa faida na hasara, fundi utatoa wapi, mfanyakazi umlipe kiasi gani wala atoke mkoa gani, ufungue wapi, shelves utoe wap n.k.
Huku mtandaoni tunatoa basics za biashara peke yake, na si kila kitu. Mfano tunaweza kujuelekeza vitu muhimu vya kuanza navyo, machimbo kafhaaa na hata kukufungia mzigo n.k.
Ila Unatakiwa ku control na ku manage biashara yako ya 85% na kuwa na maarifa mengi kuhusi biashara yako na mapato yako, unless kama unataka kufanya partnership.