Ifahamu Cosmic energy ni nini

Ifahamu Cosmic energy ni nini

Rakims

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2014
Posts
5,002
Reaction score
4,571
Vipindi katika vipindi vilivyopita niliwaahidi kwamba nitafundisha kuhusu Cosmic energy hivyo katika makala na video hii nitakufundisheni mambo yafuatayo:
  • ni nini cosmic energy?
  • ina kazi gani?
  • ina faida gani?
  • ina msaada gani kwa mtu mwenye kuipokea?
  • kwa nini huitwa zawadi katika zawadi za meditation ambazo mtu akipokea hupanda rank yake kutoka sehemu moja kwenda nyingine?

Kwa kuanza:

Cosmic energy ni nini?​

Kwanza kabisa fahamu ya kwamba ubongo wako kazi yake sio pekee ya kutengeneza na kufikiria peke yake lakini pia kazi yake ni kupokea yaani hufanya kazi kama receiver vile vile.

Inategemea na unazungusha mawimbi wapi nao utapokea maelezo vema. Mathalani tunapokuja kwenye maelezo ya Cosmic Energy.

Kwanza kabisa fahamu ya kwamba cosmic energy, ni nguvu ambayo ipo kila sehemu ambapo yupo mwanadamu yaani kwa kiswahili rahisi ni nguvu ya roho ambayo ipo kila sehemu waliokufuru huita Mungu.

Lakini walioshukuru huita malaika wa Mungu ama betri za roho,

Roho yako ni sawa na simu iliyoishiwa charge muda mwingine hujicharge automatic lakini muda mwingine inategemea wewe mwenyewe unataka iwe na charge kwa asilimia ngapi.

Cosmic energy ni nguvu ambayo ipo kila sehemu aliyopo mwanadamu ambayo inamfanya atambue na ajue ya kwamba kila kitu kimeungana.

Na vyote huenda kwa hesabu na pia kwa mizani sawa na yeye anaweza kuwa ama kufika ama kusikia chochote pale pale alipo ikiwa atakuwa na maarifa.

Kila kitu kimeunganika na kimeungana yaani wewe, dunia, galaxy na kila kitu.

Jinsi tunavyoishi maisha yetu ya kila siku ni kutokana na haja na uthubutu tulionao na kile tulichopangiwa kwa mizani yake mwenyewe Roho ya kwanza ama chanzo cha roho,

Mara nyingi na watu wengi hupokea nguvu hizi kwa kupitia fikra yaani pale fikra chanya inapokuijia ya kufanya mabadiriko ya maisha yako ama watu wengine au mazungira yako kuwa vizuri basi huwa ni kama redio yenye kupokea transmition kutoka kwenye roho iliyo takasika ama zilizo takatika.

watu wengi hawatambui hili pale ambapo nguvu hii inapowashukia na mara nyingi watu wenye imani husema nimeongozwa na roho takatifu katika kufanya hili.

lakini pia wapigaji nao hudanganya watu kwa kusema hivyo na kinachobaki kwao ni kujideceive wenyewe tu.

Kuna ishara tofauti tofauti kwamba muda huo wewe unapokea cosmic energy katika maisha yako ambapo ya kwanza ni:

1: Msukumo wa ghafla​

Unapokukuta msukumo wa ghafla na ambao ni chanya wa kukusukuma ufanye kitu ama kuanza jambo na unajikuta unatamani ama kulipenda katika roho yako yaani kabla hujafanya unaanza kusikia raha rohoni.

Ambapo hii unakuta moja kwa moja inakuongoza kurudi katika makusudio ama sababu ya wewe kuwa hapa duniani.

2: Ndoto​

Hii ni kutokana na baadhi ya watu waliotangulia kabla yetu na mafunzo ya dini na mitume kufundisha kwamba Watu wengi hujicharge automatic yaani ile iliyokadiriwa pale tu wanapoingia kulala usiku.

maana kiimani usingizi ni nusu ya kifo yaani ukiingia kulala roho hutoka na kwenda anapopataka Mwenyezi Mungu haya mafunzo yapo kidini pia.

Ndio maana pale unapolala unaweza kupokea ujumbe kutoka katika mwili na roho yako. vile vile kuwa na ndoto ambazo kwa hakika hukuwahi kujua kabla mfano taarifa ama maarifa ya kitu mwanzo wa maarifa ya wengi ni kupitia mawazo na ndoto.

3: Subconscious mind​

Hii hutokea hata wakati wa kuangalia Video au Movie kisha inakupa majibu ambayo ulikuwa unajiuliza yaani kama vile wale characters wanakuwa wanakupa taarifa ya jambo ambalo unajiuliza muda mrefu kisha unakuwa umepata majibu pale.

Ama kuskia mziki ukiwa umebeba ujumbe ambao ulikuwa unataka kuusikia yaani ukisikiliza huo wimbo unasikia imani inapanda ama mlio ama Ayah ama vifungu vya Biblia.

Tena inakuwa inarelate na swali ambalo ulikuwa unajiuliza sana hupati majibu mfano mimi nitatajirika vipi kisha majibu yanafunguka pale pale na hii ni kutokana na roho zinakuwa zinaongea na wewe kupitia subconscious mind kukwambia purpose yako ni ipi ya kufanya,

4: Kuvutia kuelekea wazo moja​

Unaweza kujikuta kila unachofanya labda unaangalia movie na marafiki unakua na wazo limekuganda linakuvuta ulifanyie kazi, ukikaa unakuwa una waza hilo hilo jambo moja tu kutaka kulifanya.

basi hii ni cosmic energy inajaribu kukupa taarifa kwamba unachelewa muda wa kuanza.

5: Hesabu takatifu​

Kuna usemi usemao katika hesabu za fizikia kwamba "hesabu ni lugha ya ulimwengu" yaani ukitaka kuongea na ulimwengu mzima basi piga hesabu.
Ambapo kuna maumba ya dunia na ulimwengu na mwili wa mwanadamu ambayo yana ujumbe mkubwa sana kwake akiamua kusikiliza.

Ikiwa kuna umbile linakuijia mara kwa mara, ama kuna picha unapenda kuitizama mara kwa mara, ama eneo basi fahamu ya kuwa kuna ujumbe kwenye hilo hivyo wekeza hapo utapata purpose yako, kama utaona namba, umbo chochote kinachokuijia mawazoni pasipo wewe kukitaka basi kifanyie kazi.

6: Kuongezeka kwa hisia​

Mara nyingi cosmic energy pia humtembelea mtu pale anapokuwa na hisia kali na ghafla hisia hizo zinakata na anaanza kuhisi jambo lingine la ghafla lenye kumliwaza na kumpa picha kamili kwenye akili. Huo huwa ni ujumbe kutoka kwenye cosmic energy.
Mathalani; tuchukulie mfano ambao ni dhaifu japo utakupa picha cosmic Energy inakuja vipi kwenye hisia;

Unaweza kukuta mwanamke analia kwenye mahusiano yake yaani ndoa yake, kwamba mwanaume aliyenae anamtesa na kumpiga na kumnyanyasa bila sababu.
Sasa unakuta nafsi inampa kabisa kwamba hapa unapoteza muda na unaweza kutoka na ukaenda kuendelea na maisha yako.
kama ni mwanaume unaweza kupata mwingine ukaolewa ukaachana na shetani uliye nae. Lakini kama vile ilivyo kwa positive cosmic energy ilivyo ndivyo hivyo hivyo kuna negative cosmic energy.

Kwa hivyo isije kukuingia influence ya kishetani ukasema hii ni cosmic energy hapana..
Zipo nzuri na mbaya. Mfano kwa nzuri inaweza kukushauri chukua tahadhari na uondoke hapo unajiharibia maisha...

Kwa mbaya itakwambia subiri kalala tia moto kitanda au mchome kisu au mlishe sumu n.k

7: Kujihisi unapenda bila sababu​

Muda mwingine mtu humuingia upendo usiokuwa na sababu na kuanza kujihisi kupenda mazingira na watu wanaomzunguka,.

Kama ghafla tu kujiona umependa mtoto ama muonekano wa mtu mzima na kujihisi kutaka kumsaidia kujihisi unapenda kila mtu na kila kitu bila sababu nayo hutokea kwa muda mfupi.
Ama unajihisi kumuona mtu kabeba mzigo mzito unajihisi kutaka kwenda kumsaidia na unakuwa na kishawishi kikubwa.
Ama unakuwa na furaha kwa muda huo bila sababu yaani unajihisi raha rohoni, Mfano unapita sehemu unataka kupishana na mtu kisha unampisha yeye anapita halafu unahisi raha na amani yeye kupita.

Mtu akitaka kukufanyia fujo hata kama yeye ndio anamakosa unakuta unaskia raha unacheka unamuacha.

Hii ni alama kuwa kwa muda huo unakuwa unapokea cosmic energy na kama unaijua basi utakuta mtu hazubai na anaanza kujitahidi kukaa na kupokea zaidi na zaidi ukiinuka hapo wewe ni mtu mwingine.

Shida hii huwa inatokea ghafla na mtu unakuwa hujajiandaa unakuja kushtuka ghafla siku imepita nyingine na unabaki unashangaa nini kilipelekea jana yake ulikuwa na roho nzuri kupitiliza na furaha isiyo na kifani bila sababu.

Maelezo zaidi utayapata kwenye channel ya video hii YOUTUBE



Rakims
 
Tunachojua:
cosmic energy ni nadharia ya kisayansi ambayo inaamini kuwa kuna nishati inayozunguka ulimwengu mzima na inaweza kutumika kama chanzo cha nguvu za kiroho na kimwili. Hata hivyo, hakuna ushahidi wa kisayansi wa kuwepo kwa nishati hii, na hivyo inabidi kuzichambua hoja zake.

Kwanza, hakuna njia sahihi ya kupima uwepo wa nishati hii ya cosmic. Wanasayansi hawajaweza kuithibitisha kwa kutumia vifaa vya kisayansi na hivyo haijatambuliwa kama kitu cha kisayansi. Aidha, hakuna ushahidi wowote wa kuwa nishati hii ya cosmic ina uhusiano wowote na maisha yetu ya kila siku.

Pili, nadharia hii ina madai ya kisayansi ambayo hayaeleweki. Wale wanaoiamini nadharia hii husema kuwa nishati hii inaweza kutumiwa kwa madhumuni mbalimbali, kama vile kuponya magonjwa, kuondoa msongo wa mawazo, na hata kuwa na ushawishi kwenye matukio ya kila siku. Hata hivyo, hakuna uthibitisho wa kisayansi wa madai haya.

Tatu, wale wanaoamini nishati ya cosmic hutumia wazo la "vibrations" kuelezea jinsi nishati hii inavyofanya kazi. Wanasema kuwa nishati hii inatuma vibration ambayo ina athari kwa mwili na akili ya mtu. Hata hivyo, wazo hili halina misingi ya kisayansi na haijathibitishwa na tafiti yoyote ya kisayansi.

Kwa ujumla, nadharia ya nishati ya cosmic haina msingi wa kisayansi na haijathibitishwa kwa njia yoyote. Hakuna ushahidi wa kutosha wa kuwepo kwa nishati hii na madai yake ya kisayansi hayana maelezo ya kina na yamejaa tuhuma. Ni muhimu kuzingatia hoja za kisayansi na uthibitisho wa kisayansi kabla ya kuamua kuamini nadharia yoyote
 
Tunachojua:
cosmic energy ni nadharia ya kisayansi ambayo inaamini kuwa kuna nishati inayozunguka ulimwengu mzima na inaweza kutumika kama chanzo cha nguvu za kiroho na kimwili. Hata hivyo, hakuna ushahidi wa kisayansi wa kuwepo kwa nishati hii, na hivyo inabidi kuzichambua hoja zake.

Kwanza, hakuna njia sahihi ya kupima uwepo wa nishati hii ya cosmic. Wanasayansi hawajaweza kuithibitisha kwa kutumia vifaa vya kisayansi na hivyo haijatambuliwa kama kitu cha kisayansi. Aidha, hakuna ushahidi wowote wa kuwa nishati hii ya cosmic ina uhusiano wowote na maisha yetu ya kila siku.

Pili, nadharia hii ina madai ya kisayansi ambayo hayaeleweki. Wale wanaoiamini nadharia hii husema kuwa nishati hii inaweza kutumiwa kwa madhumuni mbalimbali, kama vile kuponya magonjwa, kuondoa msongo wa mawazo, na hata kuwa na ushawishi kwenye matukio ya kila siku. Hata hivyo, hakuna uthibitisho wa kisayansi wa madai haya.

Tatu, wale wanaoamini nishati ya cosmic hutumia wazo la "vibrations" kuelezea jinsi nishati hii inavyofanya kazi. Wanasema kuwa nishati hii inatuma vibration ambayo ina athari kwa mwili na akili ya mtu. Hata hivyo, wazo hili halina misingi ya kisayansi na haijathibitishwa na tafiti yoyote ya kisayansi.

Kwa ujumla, nadharia ya nishati ya cosmic haina msingi wa kisayansi na haijathibitishwa kwa njia yoyote. Hakuna ushahidi wa kutosha wa kuwepo kwa nishati hii na madai yake ya kisayansi hayana maelezo ya kina na yamejaa tuhuma. Ni muhimu kuzingatia hoja za kisayansi na uthibitisho wa kisayansi kabla ya kuamua kuamini nadharia yoyote
Umejitahidi kutoa hoja lakini hoja yako ni dhaifu kwa maana haina mashiko katika andiko husika....
Basically hapo nimeongelea zaidi upande wa kiroho na kabla ya kuweka Quote ulitakiwa uelewe kipande hiki kinamajibu kamili ya hoja yako...

Kwanza kabisa fahamu ya kwamba cosmic energy, ni nguvu ambayo ipo kila sehemu ambapo yupo mwanadamu yaani kwa kiswahili rahisi ni nguvu ya roho ambayo ipo kila sehemu waliokufuru huita Mungu.

Lakini walioshukuru huita malaika wa Mungu ama betri za roho,


Fahamu ya kwamba ungefikia hapo kama ni kweli ni mtu wa kuamini katika sayansi ungesema tu moyoni hii hainihusu na ungepita kushoto, kuliko kutoa hoja bila kujua muhusika kalenga nini?

Mwana sayansi gani kawahi kuthibitisha uwepo wa Mungu??? Malaika Je,??? Uwepo wa roho???

Hivyo ni vema kutokujadiri jambo ambalo unakubaliana nalo kwa mtizamo mmoja kwa watu ambao wana mitizamo miwili....
Ikifikia sehemu ubongo wako ukitanuka katika kuelewa na kuamini katika mitizamo miwili leta Hoja

Rakims
 
Elimu ya hekima kwa wenye hekima

Huhitaji sayansi kuthibisha uwepo au kitokuwepo kwa nguvu, bali yahitaji hekima kutambua uwepo wake..

We are only limited by our imaginations......
Wachache sana wenye kutambua hili katika mia ni asilimia 5% tu.
Ndio utaona mtu wa kwanza kabisa kupokea uzi anaquote brain washed ideas... Instead of dig deeper

Rakims
 
Maelezo ya kiswahili ila neno cosmic Bado Ni lugha ya kigeni.
Weka kwa kiswahili na Nini Maana yake halisi na dhana iliyo nyuma yake .
 
Maelezo ya kiswahili ila neno cosmic Bado Ni lugha ya kigeni.
Weka kwa kiswahili na Nini Maana yake halisi na dhana iliyo nyuma yake .
Thread nzima umeona hiyo ndio hoja ya kuanzisha?

Rakims
 
Usikwepe swali .
Jibu ulichoulizwa .
Maana huwa mnakwapua vitu na hamjui kioichopo nyuma ya hiyo dhana .
Ukijua wewe inatosha... wacha sisi tunaoandika vitu hatujui tuendelee kuandika.

Rakims
 
Can you elaborate a bit about cosmic rays in the air?
In which perspective would you prefer me to explain it to you? Because you have to understand firstly that the perspective I use here is based more on the spiritual side than physically...

Rakims
 
Even cosmic rays in the air nobody knows the sorce of it, something to be considered spiritually.
 
Cosmic rays ionize the gas molecules. The source of lightning and thunderstorm.
what is the reason to ask something if you consider yourself to be knows about it?
Also, what is the reason for using the English language in an article that written in Kiswahili?
Do you feel that Swahili is not enough to make someone understanding the discussed subject?
Or are you trying to showing others that you know English?
How funny is that?

Rakims
 
Back
Top Bottom