Ifahamu Cosmic energy ni nini

Ifahamu Cosmic energy ni nini

Nachojua mimi nguvu iliyoenea ulimwenguni kote ni Nguvu ya Mungu. Nguvu hiyo ndiyo iliyovishikamanisha vitu vyote. Imeenea kote na kwa wakati wote.

Nguvu hii sayansi haitaki kuamini kwamba ndiye Mungu. Kwa sababu ya kutokuonekana kwake katika hali ya mwili, na kihalisia ubongo wa binadamu ni kupokezi taarifa kutoka katika Nguvu hizo na kuzifikisha katika mchakato wa nia ili kuamua kufanyia kazi au kutofanyika.

Ni makosa kusema waliyo kufuru huiita Mungu. Bila shaka wenye utambuzi ujua kwamba hizo ni Nguvu za Mungu.
Mungu ni Roho (hali ya kutothibitika kwa umbo la mwili ila matokeo ya kazi anayoifanya inaonekana dhahiri) nao (wanadamu) wamwaminio imewapasa kumuanimi katika roho na kweli (kujua uwepo wa Mungu bila kumuona na kuwa na hakika kwamba yupo)

Ikumbukwe Imani ni kuwa na uhakika wa jambo ambalo hujaliona.
Nguvu hiyo haina taarifa hasi inataarifa chanya pekee.

Taarifa hasi ni matokeo ya maamuzi mabaya yaliyofanywa na wanadamu na kuhifadhiwa kumbukumbu ndani ya ubongo.

Sent from my TECNO B1g using JamiiForums mobile app
 
Vile tu umesema unachojua wewe basi itoshe kubakia kwa upande unaojua wewe...
Kuna mengi ya kujifunza kabla ya kupitisha jambo. Hata hivyo ukielewa au usipoelewa sifaidiki na chochote in fact hili suala nimeweka kwa watu wanaolifahamu linahusu nini nyie wengine mkibaki gizani wala hamna atakae athirika na maono yenu.

Cha kukusaidia tu ukiamini hii ni nguvu inatoka kwa Mwenyezi Mungu utakuwa upo sawa...
Lakini kuamini kuwa ni Mungu nina mashaka na Imani yako kuhusu Mungu aliyekuumba. Mfuatilie zaidi kwenye vitabu vyake, Muombe idhini yake ya kumjua zaidi utafaidika.
Mwisho wa siku usije kuabudu mwanadamu mwenzio na kuita MUNGU au shetani kuita Mungu kisa tu unaamini kila kilichotoka kwa Mungu ni Mungu.

Rakims
 
Yeah Cosmic energy exist,kwa jamaa zangu wafanya yoga wanaelewa hili.
 
Vipindi katika vipindi vilivyopita niliwaahidi kwamba nitafundisha kuhusu Cosmic energy hivyo katika makala na video hii nitakufundisheni mambo yafuatayo:
  • ni nini cosmic energy?
  • ina kazi gani?
  • ina faida gani?
  • ina msaada gani kwa mtu mwenye kuipokea?
  • kwa nini huitwa zawadi katika zawadi za meditation ambazo mtu akipokea hupanda rank yake kutoka sehemu moja kwenda nyingine?

Kwa kuanza:

Cosmic energy ni nini?​

Kwanza kabisa fahamu ya kwamba ubongo wako kazi yake sio pekee ya kutengeneza na kufikiria peke yake lakini pia kazi yake ni kupokea yaani hufanya kazi kama receiver vile vile.

Inategemea na unazungusha mawimbi wapi nao utapokea maelezo vema. Mathalani tunapokuja kwenye maelezo ya Cosmic Energy.

Kwanza kabisa fahamu ya kwamba cosmic energy, ni nguvu ambayo ipo kila sehemu ambapo yupo mwanadamu yaani kwa kiswahili rahisi ni nguvu ya roho ambayo ipo kila sehemu waliokufuru huita Mungu.

Lakini walioshukuru huita malaika wa Mungu ama betri za roho,

Roho yako ni sawa na simu iliyoishiwa charge muda mwingine hujicharge automatic lakini muda mwingine inategemea wewe mwenyewe unataka iwe na charge kwa asilimia ngapi.

Cosmic energy ni nguvu ambayo ipo kila sehemu aliyopo mwanadamu ambayo inamfanya atambue na ajue ya kwamba kila kitu kimeungana.

Na vyote huenda kwa hesabu na pia kwa mizani sawa na yeye anaweza kuwa ama kufika ama kusikia chochote pale pale alipo ikiwa atakuwa na maarifa.

Kila kitu kimeunganika na kimeungana yaani wewe, dunia, galaxy na kila kitu.

Jinsi tunavyoishi maisha yetu ya kila siku ni kutokana na haja na uthubutu tulionao na kile tulichopangiwa kwa mizani yake mwenyewe Roho ya kwanza ama chanzo cha roho,

Mara nyingi na watu wengi hupokea nguvu hizi kwa kupitia fikra yaani pale fikra chanya inapokuijia ya kufanya mabadiriko ya maisha yako ama watu wengine au mazungira yako kuwa vizuri basi huwa ni kama redio yenye kupokea transmition kutoka kwenye roho iliyo takasika ama zilizo takatika.

watu wengi hawatambui hili pale ambapo nguvu hii inapowashukia na mara nyingi watu wenye imani husema nimeongozwa na roho takatifu katika kufanya hili.

lakini pia wapigaji nao hudanganya watu kwa kusema hivyo na kinachobaki kwao ni kujideceive wenyewe tu.

Kuna ishara tofauti tofauti kwamba muda huo wewe unapokea cosmic energy katika maisha yako ambapo ya kwanza ni:

1: Msukumo wa ghafla​

Unapokukuta msukumo wa ghafla na ambao ni chanya wa kukusukuma ufanye kitu ama kuanza jambo na unajikuta unatamani ama kulipenda katika roho yako yaani kabla hujafanya unaanza kusikia raha rohoni.

Ambapo hii unakuta moja kwa moja inakuongoza kurudi katika makusudio ama sababu ya wewe kuwa hapa duniani.

2: Ndoto​

Hii ni kutokana na baadhi ya watu waliotangulia kabla yetu na mafunzo ya dini na mitume kufundisha kwamba Watu wengi hujicharge automatic yaani ile iliyokadiriwa pale tu wanapoingia kulala usiku.

maana kiimani usingizi ni nusu ya kifo yaani ukiingia kulala roho hutoka na kwenda anapopataka Mwenyezi Mungu haya mafunzo yapo kidini pia.

Ndio maana pale unapolala unaweza kupokea ujumbe kutoka katika mwili na roho yako. vile vile kuwa na ndoto ambazo kwa hakika hukuwahi kujua kabla mfano taarifa ama maarifa ya kitu mwanzo wa maarifa ya wengi ni kupitia mawazo na ndoto.

3: Subconscious mind​

Hii hutokea hata wakati wa kuangalia Video au Movie kisha inakupa majibu ambayo ulikuwa unajiuliza yaani kama vile wale characters wanakuwa wanakupa taarifa ya jambo ambalo unajiuliza muda mrefu kisha unakuwa umepata majibu pale.

Ama kuskia mziki ukiwa umebeba ujumbe ambao ulikuwa unataka kuusikia yaani ukisikiliza huo wimbo unasikia imani inapanda ama mlio ama Ayah ama vifungu vya Biblia.

Tena inakuwa inarelate na swali ambalo ulikuwa unajiuliza sana hupati majibu mfano mimi nitatajirika vipi kisha majibu yanafunguka pale pale na hii ni kutokana na roho zinakuwa zinaongea na wewe kupitia subconscious mind kukwambia purpose yako ni ipi ya kufanya,

4: Kuvutia kuelekea wazo moja​

Unaweza kujikuta kila unachofanya labda unaangalia movie na marafiki unakua na wazo limekuganda linakuvuta ulifanyie kazi, ukikaa unakuwa una waza hilo hilo jambo moja tu kutaka kulifanya.

basi hii ni cosmic energy inajaribu kukupa taarifa kwamba unachelewa muda wa kuanza.

5: Hesabu takatifu​

Kuna usemi usemao katika hesabu za fizikia kwamba "hesabu ni lugha ya ulimwengu" yaani ukitaka kuongea na ulimwengu mzima basi piga hesabu.
Ambapo kuna maumba ya dunia na ulimwengu na mwili wa mwanadamu ambayo yana ujumbe mkubwa sana kwake akiamua kusikiliza.

Ikiwa kuna umbile linakuijia mara kwa mara, ama kuna picha unapenda kuitizama mara kwa mara, ama eneo basi fahamu ya kuwa kuna ujumbe kwenye hilo hivyo wekeza hapo utapata purpose yako, kama utaona namba, umbo chochote kinachokuijia mawazoni pasipo wewe kukitaka basi kifanyie kazi.

6: Kuongezeka kwa hisia​

Mara nyingi cosmic energy pia humtembelea mtu pale anapokuwa na hisia kali na ghafla hisia hizo zinakata na anaanza kuhisi jambo lingine la ghafla lenye kumliwaza na kumpa picha kamili kwenye akili. Huo huwa ni ujumbe kutoka kwenye cosmic energy.
Mathalani; tuchukulie mfano ambao ni dhaifu japo utakupa picha cosmic Energy inakuja vipi kwenye hisia;

Unaweza kukuta mwanamke analia kwenye mahusiano yake yaani ndoa yake, kwamba mwanaume aliyenae anamtesa na kumpiga na kumnyanyasa bila sababu.
Sasa unakuta nafsi inampa kabisa kwamba hapa unapoteza muda na unaweza kutoka na ukaenda kuendelea na maisha yako.
kama ni mwanaume unaweza kupata mwingine ukaolewa ukaachana na shetani uliye nae. Lakini kama vile ilivyo kwa positive cosmic energy ilivyo ndivyo hivyo hivyo kuna negative cosmic energy.

Kwa hivyo isije kukuingia influence ya kishetani ukasema hii ni cosmic energy hapana..
Zipo nzuri na mbaya. Mfano kwa nzuri inaweza kukushauri chukua tahadhari na uondoke hapo unajiharibia maisha...

Kwa mbaya itakwambia subiri kalala tia moto kitanda au mchome kisu au mlishe sumu n.k

7: Kujihisi unapenda bila sababu​

Muda mwingine mtu humuingia upendo usiokuwa na sababu na kuanza kujihisi kupenda mazingira na watu wanaomzunguka,.

Kama ghafla tu kujiona umependa mtoto ama muonekano wa mtu mzima na kujihisi kutaka kumsaidia kujihisi unapenda kila mtu na kila kitu bila sababu nayo hutokea kwa muda mfupi.
Ama unajihisi kumuona mtu kabeba mzigo mzito unajihisi kutaka kwenda kumsaidia na unakuwa na kishawishi kikubwa.
Ama unakuwa na furaha kwa muda huo bila sababu yaani unajihisi raha rohoni, Mfano unapita sehemu unataka kupishana na mtu kisha unampisha yeye anapita halafu unahisi raha na amani yeye kupita.

Mtu akitaka kukufanyia fujo hata kama yeye ndio anamakosa unakuta unaskia raha unacheka unamuacha.

Hii ni alama kuwa kwa muda huo unakuwa unapokea cosmic energy na kama unaijua basi utakuta mtu hazubai na anaanza kujitahidi kukaa na kupokea zaidi na zaidi ukiinuka hapo wewe ni mtu mwingine.

Shida hii huwa inatokea ghafla na mtu unakuwa hujajiandaa unakuja kushtuka ghafla siku imepita nyingine na unabaki unashangaa nini kilipelekea jana yake ulikuwa na roho nzuri kupitiliza na furaha isiyo na kifani bila sababu.

Maelezo zaidi utayapata kwenye channel ya video hii YOUTUBE

Rakims

Hii hatari kwa watoto.mm hunijia namba 51 kila mahali nkiangalia saa ghafla naona 51 .nikiangalia salio 105,890.51 .kwa siku naweza iona mara 30.ikiwemo nkistuka usiku nakutana nayo mefatilia maana meshindwa
 
Vile tu umesema unachojua wewe basi itoshe kubakia kwa upande unaojua wewe...
Kuna mengi ya kujifunza kabla ya kupitisha jambo. Hata hivyo ukielewa au usipoelewa sifaidiki na chochote in fact hili suala nimeweka kwa watu wanaolifahamu linahusu nini nyie wengine mkibaki gizani wala hamna atakae athirika na maono yenu.

Cha kukusaidia tu ukiamini hii ni nguvu inatoka kwa Mwenyezi Mungu utakuwa upo sawa...
Lakini kuamini kuwa ni Mungu nina mashaka na Imani yako kuhusu Mungu aliyekuumba. Mfuatilie zaidi kwenye vitabu vyake, Muombe idhini yake ya kumjua zaidi utafaidika.
Mwisho wa siku usije kuabudu mwanadamu mwenzio na kuita MUNGU au shetani kuita Mungu kisa tu unaamini kila kilichotoka kwa Mungu ni Mungu.

Rakims
Umejibu Kwa hekima kubwa mno
 
Hii hatari kwa watoto.mm hunijia namba 51 kila mahali nkiangalia saa ghafla naona 51 .nikiangalia salio 105,890.51 .kwa siku naweza iona mara 30.ikiwemo nkistuka usiku nakutana nayo mefatilia maana meshindwa
Angalia kwenye list ya contact zako mtu anaeishia na namba 51...

Rejea kwenye quotes za forum unayoipenda angalia quote ya 51..

Angalia ndugu zako mwenye umri wa miaka 51...

Angalia siku ya 51 mwanzo wa mwaka huwa kinakutokea nini...

Kisha baada ya hapo fuatilia jambo kwa siku 51 na kama ni mcheza kamari cheza kwa sh. 510 au elfu 51000 bet moja...

Utakuja kunishukuru baadae..

Tumia saa 5 na dakika moja kuanza jambo lako..

Au dakika 51 kufanya jambo lako...

Kama unatumia usafiri wa gari tembea speed 51..

Mwisho kabisa makinika na umri wako ukifika miaka 51

Ushauri:

Hakuna kinachomtokea mwanadamu bila sababu hivyo fuatilia utatuletea majibu

Rakims
 
Back
Top Bottom