Ex Spy
JF-Expert Member
- Jan 15, 2007
- 222
- 1,827
Idara ya Usalama wa Taifa (Tanzania Intelligence and Security Service) ndiyo idara maarufu na inayoogopwa sana na wananchi walio wengi. Kutokana na kutoifahamu vizuri idara hii, wananchi wengi wanaichukia na kuiogopa kwa kudhani kuwa hii ndiyo idara inayotumika katika kuwaua na kuwatesa watu wenye mlengo na mawazo tofauti ya kisiasa hususan viongozi wa vyama vya upinzani.
Kwa mfano, katika hali isiyo ya kawaida idara hii ilitajwa sana na kuhusishwa na vifo vya aliyekuwa katibu mkuu wa CCM, marehemu Horace Kolimba, aliyekuwa waziri wa mipango na uchumi wakati wa serikali ya wamu ya pili Profesa Kigoma Ali Malima, na hata mzee Mahimbo aliye fariki hivi karibuni kwa ajali ya gari. Hata hivyo hakuna ushahidi wowote unao onesha au kuthibitisha kwamba idara hii ilihusika kwa namna moja au nyingine na vifo hivyo.
Kuanzishwa kwa Idara ya Usalama wa Taifa
Idara ya usalama wa Taifa (TISS) imeundwa kwa sheria ya bunge namba 15 ya mwaka 1996 (Tanzania Intelligence and Security Service act No. 15 of 1996) iliyosainiwa na Rais Benjamin Mkapa tarehe 20 mwezi Januari mwaka 1997. Sheria hiyo ndio inayoipa mamlaka Idara ya Usalama wa Taifa kufanya kazi zake ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na pia ina ainisha majukumu, mamlaka na mipaka ya idara ya usalama wa Taifa. Kutokana na kuwepo kwa sheria hiyo siyo rahisi kwa idara hiyo kufanya mauaji ya raia wasio kuwa na hatia kwani idara itakuwa inavunja sheria na kukiuka mamlaka iliyopewa na Bunge.
Matumizi ya Nguvu ya ziada
Hata hivyo, kama ilivyo kwa jeshi la wananchi wa Tanzania na Jeshi la Polisi, kadhalika idara hii INARUHUSIWA kutumia nguvu ya ziada (Reasonable force) katika kuwazuia maadui kumdhuru Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, viongozi wengine na wananchi wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa msingi huo, maafisa wa Usalama wa Taifa wanaweza kutumia nguvu au silaha yoyote inayofaa (reasonable force) katika kuwazuia magaidi, majasusi au maadui wanaotaka kufanya hujuma.
Hata hivyo nguvu hiyo ni lazima iwe inayofaa na isiyozidi kupita kiasi (reasonable force). Endapo adui atakuwa na silaha, basi maafisa wa Usalama wa Taifa watatumia silaha kumkabili adui hiyo. Ndio maana mtu aliyempiga kibao Rais mstaafu Ali Hassan Mwnyi hakuuawa kwa kupigwa risasi, bali alikamatwa na kushitakiwa.
Kwanini ilianzishwa 1996?
Pamoja na idara hii kusajiliwa kisheria mwaka 1996, idara hii ilkuwepo tangu wakati wa utawala wa Mwalimu Julius Nyerere ambapo ilikuwa ikifanya kazi chini ya mwamvuli wa ofisi ya Rais. Pengine kitu kilichopelekea kusajiliwa kwa idara hii ki sheria ni mabadiliko ya mfumo wa kisiasa na uchumi yaliyotokea duniani mwishoni mwa miaka ya 1980 na kuingia Tanzania kwa kasi miaka ya 1990. Mabadiliko hayo na hasa kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi viliiweka idara hii katika hali ngumu ki utendaji kutokana na viongozi wengi wa vyama vya siasa kuamini kuwa idara hiyo ina kilinda chama tawala.
Baadhi ya wakurugenzi waliopata kuongoza idara hii ni marehemu Emilio Mzena (mkurugenzi wa kwanza) ambae alijipatia umaarufu mkubwa miongoni mwa wananchi kiasi cha kujulikana kwa jina la 'Mr Serikali'. Wengine ni marehemu Dr Laurence Gama, Mzee Hans Kitine, marehemu Luteni Jenerali Imran Kombe, na Colonel Abson. Wakati wa uongozi wake Colonel Abson aliiboresha idara ya usalama wa Taifa na kuhakikisha muswaada wa kuundwa kwa idara ya usalama wa Taifa kisheria unapelekwa bungeni na hatimae kusainiwa na Rais Mkapa. Kwa sasa, Idara ya Usalama wa Taifa inaongozwa na Rashid Othman (Mkurugenzi mkuu) akisaidiwa na wakurugenzi wengine wanao ongoza kurugenzi ndogo.
Majukumu ya idara ya Usalama wa Taifa

- Ni jukumu la idara hii kumchunguza mtu yeyote, kikundi cha watu au taasisi yoyote endapo idara hiyo inayo sababu ya kuamini (reasonable cause) kwamba mtu huyo anahatarisha au ni chanzo cha hatari kwa Usalama wa Taifa. Kwa sababu hiyo idara hii inaruhusiwa kuingia (kumchunguza) kwa mtu yeyote, idara yoyote ya serikali, mamlaka yoyote, polisi au 'policing organisation' yoyote.
- Kukusanya taarifa za ki intelejensia na ki usalama, kuzichambua na kuzitumia taarifa hizo kuzuia vitendo vyovyote vya ki adui vinavyoelekezwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kumshauri Rais na Mawaziri kuhusu maswala mbali mbali ya ki usalama. na kuvifahamisha vyombo vingine vya dola kuhusu uwezekano au kuwepo kwa vitendo vya ki adui katika jamhuri ya muungano wa Tanzania. Idara hii ndio iliyopewa jukumu la kuilinda jamhuri ya muungano wa Tanzania kutokana na vitendo vyote vya ki adui ikiwa ni pamoja na ujasusi (espionage), uhujumu (sabotage) ugaidi (terrorism) na uhaini na uzandiki (subversion)
- Kwa sababu hiyo, Idara ya Usalama wa Taifa inao wajibu wa kuilinda na kuitetea serikali ILIYOCHAGULIWA na wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili isiondolewe madarakani KINYUME cha sheria. Idara inatakiwa kuwadhibiti watu au kikundi cha watu wanaopanga mapinduzi, wanaotoa vitisho au maneno ya kuwashawishi wananchi kuipindua serikali (uzandiki) au namna nyingine yoyote ya kuiondoa serikali pasipo kupiga kura kama inavyoagizwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
- Aidha idara hii inao wajibu wa kuzuia vitendo vyote vya kigaidi (terrorism) vinavyopangwa kufanyika katika ardhi ya Tanzania bara, Zanzibar na sehemu nyinginezo ambazo ni mali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ( k.m balozi zetu). Idara inawajibika kufanya uchunguzi, kuwatambua magaidi, na kuvifahamisha vyombo vingine vya dola ili kupanga mikakati ya kuwakamata na kuwafikisha mahakamani.
- Idara hii pia inalo jukumu la kuchunguza, kugundua na kuzuia njama zozote zinazopangwa na mtu binafsi, kikundi cha watu, au nchi jirani zenye lengo la kuleta machafuko, mauaji au maangamizi ya aina yoyote kwa wananchi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa lengo la kujipatia mafanikio ya kisiasa, kiuchumi, au kijamii ndani au nje ya jamhuri ya muungano wa Tanzania. Idara ya usalama inatakiwa kuwatambua watu wanaopanga mipango hiyo na watu au serikali zinazo wasaidia katika kutekeleza mipango hiyo, Kuchunguza vitendo vinavyofanywa na serikali za nje, asasi zisizo za kiserikali na wageni ili kubaini njama zinazounga mkono au kusaidia vitendo vya kijasusi au hujuma katika nchi yetu.
- Aidha ni wajibu wa idara ya usalama wa Taifa kuhakikisha kuwa wananchi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania wanaendelea kuishia kwa utulivu, amani na mshikamano kwa kuchunguza na kubaini matatizo mbali mbali yanayo wakabili wananchi na kuishauri serikali iliyopo madarakani namna ya kuondoka kero zinazo wakabili wananchi.
- Idara hii pia ndio yenye jukumu la kuwalinda viongozi wote wa kitaifa ikiwa ni pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Makamu wa Rais, Rais wa serikali ya baraza la mapinduzi Zanzibar, na wengineo ambao idara kwa sababu moja au nyingine itaona wanafaa kupewa ulinzi.
- Aidha idara ya usalama wa Taifa inawajibika kukusanya taarifa zote za kiusalama ndani na nje ya nchi na kuishauri serikali (Rais) kufanya maamuzi mazuri na yenye faida kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.