IFAHAMU KARAMA YAKO NA UITUMIE KUISHI VYEMA DUNIANI

IFAHAMU KARAMA YAKO NA UITUMIE KUISHI VYEMA DUNIANI

Smile Digital Stationery

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2024
Posts
202
Reaction score
317
Hello Wana JF;
Leo nakuja na Mada hii inayohusu KARAMA au wengine huita KIPAWA/KIPAJI.
*
Ifahamike kuwa kila binadamu aliyepo hapa duniani, basi kaletwa kwenye uwanja wa mapambano, mapambano ambayo yamegawanyika katika makundi, kuna mapambano ya kiimani, kiuchumi, n.k.
Ila amini nakwambia hayo mapambano mengine yote hutoweza kuyapigana kama hutoshinda pambano la kiuchumi, yaan hapa namaanisha ushibe kwanza ndio mambo mengine yaendelee. Hutoweza kwenda kufanya ibada kwa usahihi ikiwa tumboni kuna njaa.
*
Sasa basi, kwa mantiki hiyo aliyetuleta hapa duniani hakutuacha tuu bure, kila mmoja wetu alimpatia silaha yake atakayoitumia ili impatie riziki (uchumi). Na hiyo silaha ndio hii tunayoiita KARAMA/KIPAWA/KIPAJI.
*
Katika maandiko Mwenyezi Mungu anatuambia kuwa ametupatia neema mbalimbali na atatuuliza namna tulivyozitumia.
Huenda ukawa unajiuliza 'sasa mimi nitajuaje kama ninayo/ninazo hizo karama?'
Nikweli, wengi wetu hatujui Karama zetu lakin amini kwamba zipo, na alotuumba anatupenda sana ila sisi ndo hatuna utaratibu wa kujifanyia uchambuzi yakinifu kujijua/kujitambua.
Ukijijua utajua unatakiwa ufanye nini na usifanye nini. Na wanasema kuwa ukishajijua basi utaona kila kitu kinaenda katika njia bila kutumia nguvu sana, yaan ukishaijua njia yako huwez kupotea. Wengi wetu tunapotea kwasababu tunapita njia ambazo sio zakwetu ktk utafutaji.
Inasemekana wenzetu Wazungu ktk malezi ya watoto wao wanawafuatilia sana kujua wanapendelea kuchezea au kucheza michezo gani sana wakiwa watoto, basi kile wanachokipenda zaidi wazaz wanajua hii/hizi ndizo karama za mtoto wetu, kisha nao huwalea kupitia karama ile mpaka ukubwani mwake, kama alikuwa anapenda sana kuchezea magari basi watamsomesha Uinjinia wa magari n.k
Ila kwetu Africa mtoto akiwa n mwenye kuchezea sana magari na kuyaunda basi mzaz akija anayatupa nje ya uzio wa nyumba na kumfokea mtoto kwa kumuona anamjazia mauchafu ktk nyumba yake, kumbe alitakiwa amsaport kwa kumuendeleza kupitia kwayo.
*
NJIA KADHAA ZA KUZIJUA KARAMA ZAKO:
***
1. Tazama zaidi kile unachokipendaaa, yaan kuna ile hali toka upo mdogo kuna jambo au fani ambayo unajikuta unaipenda mnoo na unatamani siku moja uifanye (ukubwani), na hata huku ukubwani unajikuta kuna shughuli flani unaipenda sana na ukiifanya unajikuta una enjoy kuifanya, yaan unaifanya ilihali viungo vyako na milango yako ya fahamu yote inafurahia kile unachokifanya.
Na mara nyingi kile unachokifanya wewe binafsi unakiona ni kazi rahisi saana ila mwengine anaiona ni kazi ngumu mnoo. Basi hcho unachokifanya unapaswa kujua kuwa hyo ni miongoni mwa karama zako.
*
2. Kwa kusikiliza/kuuliza kwa wale watu wako wa karibu unaowaamini;
Ikiwa hvyo unaweza kumuuliza mtu huyo, 'Hivi mimi nafanania kufanya kitu gani, au kazi gani, au shughuli gani?'
Watu wa pembeni wanao uwezo mkubwa wa kuziona karama zako kuliko wewe mwenyewe, Hujawahi kuwa unafanya shughuli flani kiutafutaji mfano; Biashara za masokoni, Ufundi ujenzi, n.k, halafu ukashangaa unakutana na Comments mtu tuu usomjua au unayemjua akakwambia ' Asee mbona huendani na hizi kazi?', akiendelea anaweza kukwambia ' Ahh wewe bana unafanania kukaa Ofisini hiv umetulia zako watu ndo wakufuate' Na waeza kutana na comments hizo kwa mtu zaid ya mmoja. Basi usiwachukulie kama wanakudharau kwa unachokifanya, bali unatakiwa uifungue akili na ufahamu wako kuwa umepita kwenye njia ya mtu mwengine na hyo sio njia yako, so hata mafanikio yako yatakuwa magumu sana hvyo unatakiwa ujijue kuwa "Natakiwa nifungue biashara ya kukaa Ofisini/Ndani ya duka (yaan biashara za kutulia kusubiri mteja) n.k.
*
3. Kwa kumuomba Mwenyezi Mungu akuonyeshe na akudhihirishie karama zako pindi unapofanya ibada.
Muomba Mola wako akuonyeshe na akufunulie karama zako alizokupa kusudi uweze kuzitumia ukuze uchumi wako.
Ukiwa unafanya kazi ya karama yako basi hutumii nguvu, yaan wew utajiona unaifanya kawaida tuu ila comments za wateja zikawa kubwa sana wakisifia kile unachokifanya na wateja wakaongezeka mnoo kuhtaji huduma zako, mfano, waeza ukawa karama yako ipo kwenye ufundi kapenta, unajikuta automatical ubunifu unakujia tuu kichwani unaunda farniture mpaka unakuja kuimaliza matokeo yake yanakuwa makuubwa sana, inaonekana inavutia mnoo na wateja wanaipenda na kuweka orders uwatengenezee kama hyo. Ila mafundi wenzako wanakuona kama unatumia ndumba kumbe sio kweli. Au wew n fundi wa kushona nguo, unajikuta ubunifu wa mitindo unakuja tuu akilini mwako, unautoa ktk nadharia unauleta ktk vitendo, nguo unayokuja kuitoa hapo kila mmoja anashangaa na kuisifia na wateja wanaigombania na kuweka orders, unajikuta unaaminika na wateja wanaitana hata kutoka nje ya mkoa uliopo kutokana na ufanisi wako, ila cha ajabu wewe unajiona umefanya kaz y kawaida tuu na wala hujatumia nguvu kubwa. Sasa huo mtindo Apelekewe fundi mwengne aushone uone atakavyohangaika nayo na huenda asiishone kama yako. Ni kwasababu wew unafanya kazi ya karama yako.
**
Hivyo Wakuu naamin haya ni baadhi ya mambo ambayo yanatukuta wengi huku mtaani, hivyo tuliabgalie hili suala na kulifanyia kazi.
Ahsanteni
 
Nina kipaji cha kula naweza kula chapati nyingi sana bila kushushia chai, maji au supu
Ni vizuri, basi angalia namna gani utakitumia ili kiwe sababu ya kuboresha uchumi wako. Namaanisha kiwe chanzo cha pesa. Mfano, unaweza tumia mitandao ya kijamii na hicho kipaji chako ukakitumia kama content.
 
Back
Top Bottom