Ifahamu Long Range Identification Tracking (LRIT) System

Ifahamu Long Range Identification Tracking (LRIT) System

Offshore Seamen

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2018
Posts
5,489
Reaction score
14,091
Long Range Identification Tracking system ni mfumo ulioanzishwa kwa ajili ya kufuatilia mienendo ya meli ikiwa pwani ya bahari na nje ya eneo la nchi husika.

Huu mtambo hufungwa na nchi husika na kuna makubaliano ya kubadilishana taarifa Kwa wanachama au nchi zilizo sajili meli ambazo hutumia LRIT.

Ufanyaji kazi
LRIT hutumia satellite katika mawasiliano hivyo inaweza kutuma taarifa umbali mrefu ukilinganisha na AIS.

Taarifa zitolewazo
Hii uleta taarifa ya eneo ilipo meli,speed, uraia wa meli na wakati taarifa ilipotumwa.

Faida za mfumo wa LRIT
Mfumo huu umekuwa msaada katika masuala ya ulinzi wa bahari, kuratibu meli mlizosajili kama taifa ziwapo nje ya eneo lenu.

Nchi ya Canada ndio ilikuwa ya kwanza kutumia mfumo huu, baadae jumuiya ya Ulaya na nchi za America kusini,Panama nao wanatumia huu mfumo kufatilia meli zao walizosajili.

Huu mfumo ni muhimu sana na umekuwa msaada kwenye ufatiliaji meli mlizosajili na zile zitazopita kwenye eneo lenu la bahari zenye hiki kifaa.

Mfano: Unapoingia Marekani ukiwa nje umbali wa maili 40 meli yako uonekana na wao hupata taarifa zako, pia kama kuna katazo utapewa na Coast Guard wao.

"Sea never dry"

images (1).jpeg
 
Sawa nimekusoma mzee wa maerisk alabama
 
Samahani mkuu ntakuwa kama nipo nje ya mada ila napenda kufahamu Ni kweli Cooling system ya engine za meli maji yake huchukuliwa baharini/ziwani na kurudishwa tena si kama automobile nyingine ambazo maji au coolant huzunguka humo humo.
 
Samahani mkuu ntakuwa kama nipo nje ya mada ila napenda kufahamu Ni kweli Cooling system ya engine za meli maji yake huchukuliwa baharini/ziwani na kurudishwa tena si kama automobile nyingine ambazo maji au coolant huzunguka humo humo.

Mkuu meli injini zake zina cooling system za aina mbili
1. Air Cooling-
Hizi upozwa kawaida kwa hewa nyingi ni za boti ndogo na kuna za vivuko Deutz zilikuwa ni air cooling.

2. Water cooling
Hapa kwenye water cooling napo kuna aina mbili za upoozaji

I. Closed cooling system
Huu ni mfumo wa upozaji injini wa kutumia maji kama wa kwenye gari ambapo injini hupozwa na maji ya rejeta na coolant.
Hizi ni injini za meli ndogo na vivuko.

II. Open cooling system
Huu ni mfumo wa upozaji injini za meli kwa kutumia maji ya bahari/ziwa. Hii inakuwa kama closed cooling ambapo maji ya kawaida ya kwenye Heat Exchanger/Expansion Tank au mfumo wa rejeta upoza injini kama kawaida kisha maji hayo yaliyo zunguka kupoza injini nayo huja kupoozwa na maji ya ziwa/bahari kwa kuvutwa nje na pampu kisha kutupwa tena nje.

Hii utumika kwenye injini kubwa za meli.
 
Mkuu meli injini zake zina cooling system za aina mbili
1.Air Cooling- Hizi upozwa kawaida kwa hewa nyingi ni za boti ndogo na kuna za vivuko Deutz zilikuwa ni air cooling.

2.Water cooling
Hapa kwenye water cooling napo kuna aina mbili za upoozaji..
Asante Sana mkuu hii open cooling system ndo ilinipa hasa wakati mgumu kuielewa sisi tushazoea hizi medium speed large Diesel Engines za locomotives ni kweli kuna heat exchanger isipokuwa cooling ya maji ni katika Radiator kama ulivyoainisha pale juu katika closed cooling system.
 
Back
Top Bottom