Ifahamu: Mzumbe Special School and The So called THE TOP FIFTEEN 15)

Ifahamu: Mzumbe Special School and The So called THE TOP FIFTEEN 15)

MoroGent

Senior Member
Joined
Jan 10, 2018
Posts
149
Reaction score
473
Salam Wanjukwaa,
UTANGULIZI
Nchini Tanzania katika maendeleo ya kitaalum ni pamoja na kupitia shule za secondary. Kuna kafeelings flani kazuri sana unapomaliza primary na kujiunga na secondary hasa shule hizi zinazoitwa shule za vipaji maalum za boys ikiwemo Mzumbe, Tabora, kibaha, Ilboro na Kisimili. Shule za girls sizifaham sana zaid ya Kilakala, Msalato, Weluwelu you name it.

Binafsi nimesoma Mzumbe Secondary enzi za juzi juzi tu za Mkuu wa shule Seme na Njawa, HP Mnubi Simba na vice wake Nelson Ng’oboko. Kuna mambo mengi sana nimeyakumbuka mojawapo ni issue ya Uongozi shuleni. Viongozi huchaguliwa wa njia ya kidemokrasia ambayo ni nzuri sana na yenye kuvutia sana.

UPATIKANAJI WA VIONGOZI
Kwanza position 15 hutangazwa na Mwalimu wa Malezi, kasha wagombea hujitokeza sina uhakika kama kuns kuchukus fomu. Baada ya kutambulika wagombea, hutambulishwa kwenye mkutano maalumu wa kila asubuhi pale tunauita PARADE japo shule zingine huita ASSEMBLE. Baada ya utambulisho kampeni huruhusiwa kwa siku kadhaa zisizozidi 5 kisha huandaliwa kitu kinaitwa General Campaign amabayo ni kampeni ya kufunga, siku hiyo wanafunzi wote huitwa na kukusanyika mahali panapoitwa Assembly Hall. Walimu wote wanakuja na wagombea wanaitwa one by one position zote, na kupewa nafasi ya kujinadi na kuulizwa maswali.

GENERAL CAMPAIGN DAY
Th very interesting part of election huwa ni siku hii ya General Campaign,
Kwanza kujinadi, kujibu mna kuuliza maswali ni kwa ENGLISH, kama unavojua wengi wa wanafunzi wa vipaji maalum wanatokea kayumba na kimombo huwa ni shida japo kuna vijana wa magari ya njano, Kwahiyo, anayejua ngeli sana hupta kura nyingi, na pia unfortunately mtu anayepiga broken ya kupitiliza huwa kichekesho lakini huleta furaha na mwiho wa siku hupita kwa kura nyingi sana. Kwa kipindi change nakumbuka Deogratius Nagu, Paul Mpokwa na Paul Israel walikuwa mabingwa wa ngeli sana. Kisha wabovu wa ngeli walikuwa ni Berius Kyekaka na Kishoka kra zao ziliuwa za kucheba.

Pili, walimu wote wapo kwahiyo unaulizwa swali la kichokozi kuona kama utawaponda au kuegemea kwa walimu kituc amabacho huwa ni challenge sana, kuna wanaharakati ambao walikuwa hawaogopi na walikuwa wanawapa walimu michano mbel ya wanafunzi mpaka walimu kuwadiss, hii ilikuwa inafurahisha sana.

Mwisho siku ya General Campaign huwando siku ya kufunga kampeni na kesho yake uchaguzi hufanyika madarasani na viongozi kupatikana, kasha inafuata parade the same day na viongozi kutangazwa, siku chache huapishwa na kuanza kazi.

THE TOP FIFTEEN (15)
Hii huwa timu ya viongozi walipatikana amabo kwa idadi huwa wapo kumi na Tano kama ifuatavyo:

Head Prefect: Kiongozi Mkuu huheshimika na walimu na wanafunzi, usiombe kesi yako ikafika kwake

Vice HP: Humsaidia HP majukum yake hutoka olevo na HP hutoka Advance
Discipline Prefect: Hushughulika na nidham kiujumla
Security Prefect: Ulinzi wa jumla
Self-Reliance: Ni miradi ya shule, kilimo na ushuru,(cheo change), nimeania rushwa apa
Cleanliness and Environmnt Prefect; Mzee wa mazingira kiujumla
Academic prefect: taaluma kiujumla
Dining hall prefect: Huyu ni kiongozi wa chakula, lazima umpend na ujipendekeze
IPP prefect: Huyu ni Information press and publicity, mambo ya computer room na habari shuleni
Area Captain; tunaita AC, ni viongo wa mabwani 4 (mirambo, mkwawa, karume na Shaab Robert)
Kama hawafika 15 nimesahau vyeo vingine ongezea

BENEFITS OF TOP 15 LEADERS​
  • Hutengewa bweni maalum na ni lazima uhamie uko, hilo bweni linaitwa FEDERATION AU Fede​
  • Ukiwa parade hukai mstarini kuna sehem maalum ya viongozi nyuma ya wanafunzi​
  • Sio rahisi kuadhibiwa, mind you, Mzumbe hakuna VIBOKO, labda kosa kubwa upigwe Paa au kazi​
  • Mudawa chakula unaingia direct jkoni, chakula kinapikwa special separately, hugombanii na unakula Top-Layer, usiome utam yah ii kitu babu​
  • Unavaa sharti la mikono mirefu tofauti na wanafunz wengine​
  • Unaheshimika sana, maana mwanafunz akikuzingua, akaitwa Fede, kesi ikafika kwa HP utajuta​
  • Unapata cheti cha uongozi ukimaliza shule​
  • Haufanyi kazi yoyote Zaidi ya kusoma ukia uongozini na ukistaafu pia​
  • Unakuwa na zamu ya kuongoza parate kwa ngeli, na kusimamia majukum yako freely​
  • Unapata muda wa kusoma vizuri, kula vizuri na kupumzika, ivo unapiga one​
KUMBUKUMBU ZISIZOSAHAULIKA​
  • Kuna kikundi kinaitwa MUFA (Mzumbe Ukoko Fighters) waviziaji siku ya wali wapewe ukoko​
  • Kwenda MONGWE ni kuishiwa pesa za matumizi au kufulia​
  • Kila mwaka kuna ziara ya kupanda mlima ulugulu mpk kijijikinaitwa MONGWE​
  • Chatu zone ni sehemu kuna mianzi chatu huonwa regulary akikatisha, so usiku ni risk​
  • Msuli tembo ni kusoma sana kwa style ya triangle (darasani, jikoni na bwenini)​
  • Wazee wa TOBO au kutoboa ni wanafunzi wanosoma jioni mpk asubuhi​
  • Ugali huitwa ngama, uji ni NYUJI wali ni Nyali​
  • Kuna sehemu ya SARO , saro ni mbogamboga na kachumbali zinauzwa ukichoka maharage​
  • Darasani mnapangwa ki-AKILI, A1 ni majinius, A2 akili wastani, A3 ni vilaza au LUPANGO​
  • Wengi wanaotoka nglish medium hufeli au kupafom poor, maana msuli ni mgumu, kujitegemea​
  • Stamsahau jamaa naitwa GWAMAKA NJOBERO alikuwa TO yeye kila somo ni A, watu wana akili​
  • KUGONGEA ni kuomba sukari, mkate au pinut butter kwenye trunker akiwa natumia​
  • Ukisoma Mzumbe lazima uwe PCM au PCB otherwise we kilaza, na lazma uende UD au MUHAS​
  • Uswazi au vibandani ni chini pale tunaponunua mahitaji karibu na chuo​
  • Jioni lazma kwenda kuzurura Mzumbe University kusoma MAGAZETI na kushangaa NYASH​
  • Kabla ID hazijaanza tulikuwa tunakodiwa MU kuwafanyia Mathematics hasa set na statistics​
  • Kwenda Changalawe usiku kwenye VIGODORO au kwenda kilimahewa​
  • MZUKILA NA MZUMORO ni disco la watoto wa kilakala au morosec, pia Dakawa GIRLS​
  • Nawakumbuka Mama Kimolo, Mama Igosha, Minja, Mwaijande, Komba, Said, Dave, Ongezea..​
Nawasilisha.
​
JE UNAKUMBUKA NINI KUHUSU MZUMBE SECONDARI? AU SHULE ZINAZOFANANA NA HII?
 
Oyaa ni kweli kabsa bizo, nimesoma kipindi hiko cha kina Mnubi Simba, tumekula sana ngama, nyuji piia tumepiga sana maso, me nilikua mtu wa Chatuzone, nimekaa Mkwawa 4 pale karibu na kwa mwalimu Temba, baada ya mgomo 2013 tukabadllishiwa mabweni nimekaa Karume 6 ,
Determination is our Motto.!
 
Nakumbuka kwenda usiku kwa mkuu wa mkoa kupitia nyuma ya chuo..
Ukimya mkuu ilikua tarehe 29 May 2013 niko form 5 hapo usiku usiku siku kabla tulikaa kikaa kikao na Njawa na cabinet yake hadi asubuhi wakaishia kututukana tu na HP wetu EMILY MAYANI. nakumbuka mengi sana Hakika sisi ni Wazumbe
 
Pori kwa pori yah mitandao ilizagaa taarifa nyumbani sim kama zote
Mkuu naomba nikutambue aisee kipindi hiko sisi ndio tulianzisha mgomo huo, tukiwa form five, form 6 watarajiwa, EMILY MAYANI, ALI NGUA, PASCAL AKA AGUERO, ADO NYOTOKA,
 
Back
Top Bottom