Mbwa dume
JF-Expert Member
- Jan 15, 2014
- 5,934
- 10,206
Asilimia kubwa wabongo ndio starehe yao kubwa ni ngono na kula na kunywaKama hakuna mambo ya bia na kufyatuana ni bure kabisa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Asilimia kubwa wabongo ndio starehe yao kubwa ni ngono na kula na kunywaKama hakuna mambo ya bia na kufyatuana ni bure kabisa
Wivu at it's finestKabisa kabisa.
Je, waifahamu nchi ya Bhutan iliyopo kati ya China na India? Nchi hii ya kipekee kabisa ilipiga zuio la utalii mpaka ilipofika mwaka 1974. Ni nchi pekee Duniani iliyoweza kupima National Happiness!
Zifuatazo ni sifa 16 za nchi ya Bhutan zitakazokuacha kinywa wazi na kutamani kufika huko kufanya utalii:
16. Hakuna omba omba/au watu wasio na makazi (Homeless)-kama mtu atapoteza makazi yake basi anaripoti kwa mfalme na atampatia kipande cha ardhi kuanzisha makazi yake mapya
15. Huduma za afya bure-kila raia wake yupo intitted na huduma za afya bure, Bhutan ni nchi ambayo inatoa huduma bora kabisa za afya. Mtu ataamu kupata tiba za kienyeji au za kisasa na zote ni bure.
View attachment 1152423
14. Matumizi ya teknolojia-Bhutan imeruhusu hivi karibuni matumizi ya internet, TV na radio, kwani ni nchi ambayo imejizatiti kulinda tamaduni zake.
View attachment 1152426
13. Vazi la Taifa- raia wake wanavaa mavazi maalumu ya kitamaduni tokea miaka 400 iliyopita. Pia ni rahisi kugundua hali ya mtu kama ameoa au la kupitia mavazi yake maana wanavaa skafu maalumu kwenye bega la kushoto ili kuonesha hali ya mtu.
View attachment 1152427
12. Hakuna kuvuta sigara- mnamo mwaka 2010 mfalme alipitisha sheria inayozuia ulimaji na uingizwaji wa zao/malighafi ya tumbaku. Hili limeifanya kuwa nchi ya kwanza Duniani kuweka zuio la tumbaku/sigara. Watalii wanatakiwa kulipia kiasi kikubwa cha fedha ili kuingiza sigara nchini humo na ukiingiza kimagendo utapigwa faini au hata kufunguliwa mashtaka ya jinai.
11. Ikolojia- hii ni nchi ambayo 70% ya eneo lake limefunikwa na uoto mbalimbali, hakuna uharibifu wa mazingira. Kwa mwaka 2015 iliweka rekodi kwa watu wake kupanda miti 50,000 kwa saa moja! Hii ni nchi pekee ambayo haina hewa ya ukaa (carbon negative).
10. Pilipili- asilimia kubwa ya vyakula vyao vina pilipili nyingi hili kwa wageni ni tatizo kidogo kwani vyakula vyao vyote ni spiced.
View attachment 1152429
9. Utalii- huwezi kwenda Bhutan kwenye kundi la zaidi ya watu wawili au zaidi, maanake waweza kwenda kwenda mwenyewe ama couple! Pia malipo yote ya visa, usafiri, malazi, tour guide n.k yanalipwa in advance na utakuwa na tour guider wako wakati wote wa safari na utaruhusiwa tu kutembelea maeneo makhususi kwa utalii.
8. Ladies first- wanawake wanaheshimiwa sana Bhutan, urithi wote unaenda kwa mabinti na si kwa watoto wa kiume ilivyozoeleka!
7. 100% organic- ni kosa la jinai kuingiza kemikali yoyote Bhutan, kila kinachotumiwa kinalimwa nchini mwao na ni asilia.
6. Wanahifadhi vyakula juu ya paa-chakula chao kikuu ni mchele na pilipili... Na kipindi cha joto ndipo vyakula huwekwa juu ya paa na kukaushwa ili kulisha familia zao. Kwani kwa kipindi kirefu kuna kuwa na hali ya baridi.
View attachment 1152430
5. Marubani bora pekee ndio wanaruhusiwa kusafirisha watu kwenda Bhutan-hili si kulinda tamaduni zao bali ni swala la kiusalama zaidi! Kwani safari ni juu ya safu za milima ya Himalayans, kuna muonekano mzuri ila ni hatari kuliko. Si kila rubani anaeweza kupita kwenye milima hiyo na kutua salama, kwani kuna pepo kali na inaruhusiwa kuland mchana tu. Marubani 8 pekee duniani ndio wanaweza hili na wasafirisha takribani watu 30,000 kwa mwaka.
View attachment 1152432
4. Sheria za ndoa/harusi- ukifika Bhutani ni rahisi kudondokea kwa ardhi yao nzuri kuliko binti zao! Ni kosa kuolewa na mgeni.. Baada ya kuoana mwanaume huenda kuishi kwa mwanamke mpaka pale atakapokuwa na kipato kizuri na kuhamia makazi mapya.
3. Wizara ya Furaha[emoji4][emoji4] - wengi wanatamani hili lingetokea Bongo kwenye stress za kila aina... Mnamo mwaka 2008 Gross National Happiness (GNH) ilizaliwa Bhutan kuhudumia furaha za watu wake, ndio nchi pekee duniani yenye wizara maalumu ya masuala ya furaha na GNH ni muhimu kama ilivyo GDP. Mnamo mwaka 2015 walifanya savei kwa watu wake kujua ni jinsi gani wamejawa na furaha... Walipata matokeo ya kushangaza... 91% ya watu wake wana furaha! Na 43% furaha yao imezidi[emoji3]! So well being ni kati ya happiness na financial indicators.
View attachment 1152434
2. Barabara zake hazipo busy (less traveled)...alama zote za barabarani zimechorwa kwa mkono na mji mkuu pekee Thimpu ndio mji ambao hauna taa za barabarani na nchi nzima... Traffic wanafanya kazi manually. Kuna city boith ambazo kwa mtalii yoyote yule ni muhimu kujionea hivyo vibanda.
View attachment 1152435
1. Nyumba za kipekee (Gingerbread like houses)-raia wa Bhutan wanapenda kupamba nyumba zao sana. Wanachora ndege na wanyama mbali mbali kwenye nyumba zao. Nyumba zao ni ndogo za level tatu tu, huku level ya chini wanaweka wanyama, watu wanaishi level ya pili na level ya tatu hifadhi ya nafaka zao
View attachment 1152436
Pamoja na hayo yote Bhutan watu wake ni safi na wanaushirikiano mzuri na wageni na wakarimu sana... Kama unapenda kusafiri basi ni unforgettable travel!
Relief Mirzska
britanicca
Pilipili ikiungwa uzuri ni wazimu
pilipiliNini chanzo cha pato la taifa (kiuchumi)?
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]Kuolewa na mgeni kosa - tatizo hili,..ila unaweza pata kasichana kwa muda wa utalii ?
Ndio lakini siyo kwa ukubwa kama inavyotarajiwa.. Pilipili zina element inaitwa capsaicin ambayo ndio ina muwasho na kuunguza (burning sensation)...wataalam wanasema matumizi kwa wingi yanaweza kupunguza au kuongeza risk ya cancer hasa tumboni, mdomoni au kwenye koo..Hivi pili pili haina madhara ukila kwa wingi?