Parabora
JF-Expert Member
- Jul 6, 2019
- 1,504
- 2,203
Kama nilivoahidi toka mwanzo kipindi hiki ambacho nipo lock-down nitakuwa na-share hapa taarifa mbalimbali za baadhi ya nchi nilizowahi kuishi na kufanya kazi ili kwa wale walio na ndoto za kufika wapate japo ufahamu kidogo kuhusu hizo nchi na fursa mbalimbali zinazopatikana katika mataifa hayo, na leo nitaizungumzia Japan.
Baada ya kumaliza masomo yangu ya "Bachelor of science in computer science engineering" pale Ghent University nchini ubelgiji kampuni iliyoniajiri ilinihamishia nchini Japan ambako nilitakiwa nikafanye kazi katika mji wa Nagoya na hii ni baada ya wiki 3 tu ya kufanya kazi ndani ya kampuni hii nikiwa nchini ubelgiji baada ya kuniajiri. Nagoya ni mji ambao uko umbali usiozidi 460km kwa barabara kutoka mji mkuu wa Japan Tokyo na ndio mji mkuu wa mkoa wa Chubu, ni mwendo wa dk(30 mpaka 60+) mpaka Tokyo kulingana na aina ya treni uliyopanda.
Wakuu,Ukisikia wenzetu wameendelea usidhani ni Kama majengo ya pale Ilala(posta) au kariakoo, kiukweli ukija Japan kwa mara ya Kwanza unaweza kutumia zaidi ya wiki kushangaa jinsi miji yake ilivyojengwa kwa uzuri na ustadi wa hali ya juu na namna inavyopendeza kabla ya kuyazoea mazingira na kuanza kuishi hali ya kawaida, wilaya za Japan zinavutia sana zimepangilika, mji ni tulivu, hewa ni safi, maji ya uhakika na ni safi hakika wilaya za Okamoto, Kamata, Kasuya na barabara ya Kamiyoga wilayani Setagaya ( hapa ndipo ubalozi wa Tanzania ulipo) panavutia mno.
Japan ni mji wenye viwanda vikubwa vikubwa vingi sana pamoja ya kwamba ni nchi iloyoundwa kwa muunganiko wa visiwa lakini unapozungumzia lugha ya viwanda Japan ni sehemu sahihi kwako kuja kutembelea na kujifunza kuna viwanda vikubwa mno vya utengenezaji magari, meli, ndege, simu na vingine, kwa wale wa ukanda wangu unapozungumzia kiwanda unaweza kukitaja Mutex na mwatex nikuambie tu hiyo picha ondoa kabisa hata parking ya magari tu ya viwanda hivi huwezi kuilinganisha na hivyo au TBL ya pale mwanza hizi ni big industries wakuu, Pale TOKYO barabara ya kashawai kuna jengo kubwa sana lililojengwa kwa ustadi ambalo ni makao makuu ya HITACHI karibu na NAKAMOTO hospital umbali mchache kuna jengo lingine kubwa ambalo ni makao makuu ya Kyocera pia kwa hapohapo Tokyo viwanda vinavyozalisha bidhaa ambazo zinatumika kwa wingi huko nchini ni Mitsubishi, Nikon, Sony, Toshiba na nyingine nyingi sana hivi ni baadhi tu ambavyo ni rahisi kwako kuvifahamu kwa matumizi ya bidhaa zake.
Tokyo ni jiji ghali sana kuishi kulinganisha na majiji mengine ya Japan kama Sapporo, Nara, Yokohama na Kyoto chumba kidogo unaweza kukipata kwa bei ya chini kuanzia $ 700 chini ya hapo ni tabu sana kupata na wengi wa wafanyakazi jijini humu huishi majiji ya karibu na Tokyo Kama kanagawa, Chiba na Saitama.
Baada ya kukaa siku kadhaa Tokyo na kukamilisha taratibu za kiajira kwa vile ndipo makao makuu ya kampuni yangu kwa nchini Japan, nikaanza safari kuelekea Nagoya kuripoti na kuanza kazi rasmi, Kama nilivoeleza hapo mwanzo Nagoya ni mji wenye viwanda vingi kwa nchini Japan na baadhi yao ni kiwanda kikubwa cha kutengeneza magari cha TOYOTA, HONDA, SUZUKI na mwendo wa dk 50 kwa treni ya kawaida ukiwa unaelekea Iwata barabarani kuna kiwanda kikubwa sana cha KUMAMOTO PRODUCT co.ltd ambacho moja ya bidhaa zinazotengenezwa hapo ni pikipiki za YAMAHA, kuna viwanda vingine vya meli vingi tu na vikubwa na pia Nagoya ndio mji wenye bandari kubwa nchini Japan ukifuatiwa na Tokyo, Yokohama, Osaka na Kobe hizi ni baadhi tu kwa vile Japan kuna bandari nyingi sana kulingana na ukubwa na wingi wa bidhaa zinazozalishwa viwandani na pamoja ya kuwa na viwanda vingi vikubwa nchini Japan maisha ya hapa yako chini kulinganisha na Tokyo.
Kwa mda niliokaa Japan sikuona tatzo la kiusalama ni mahali salama pa kuishi kwa wageni, kiwango cha uhalifu Kiko chini sana unaweza tembea usiku mda wowote na ukawa salama asilimia zote. Tatizo la Japan ni lugha, Wajapan wengi hawajui lugha za kigeni Kama kiingereza wao lugha yao kuu ni ki-japan na baadhi ya lugha zao za ndani, na ni watu walio busy sana sio watu wa stori kabisa ni wachache walio na hulka hiyo ya kupiga stori nadhani kwenye hili lugha pia inachangia na ukiwa unajua lugha zao vizuri kama ki-japan na kujua tamaduni zao kidogo itakuwa rahisi ku-interact nao.
Japan wana mtandao wa usafiri Bora kabisa kuliko nchi zote nilizotembelea na wa uhakika 24/7hrs uwe wa basi, treni ama ndege na usafiri wao mkuu unaotumiwa na watu wengi ni treni, nilipoanza kukaa huku nikawa najiuliza inakuaje raia wa huku anunue gari binafsi la kutembelea wakati karibia kila mtaa kuna stesheni ya treni na usafiri wake ni bora na uhakika na unafika kwa wakati, treni zinapishana Kama daladala pale kariakoo. Hawa jamaa wana nidhamu ya kazi na wanafanya kazi kwelikweli tena kwa masaa mengi sana mfululizo bila kuchoka na bado wao wanafurahia hiyo hali.
Kwenye suala la ajira kwa wageni hasa kutoka mataifa ya Africa wana sheria ngumu kidogo kwa wasio na ujuzi kuhamia nchini mwao na wanaruhusu high skilled workers kuingia na kufanya kazi nchini mwao, Pamoja na kwamba hawatilii maanani baadhi ya elimu zinazotolewa nchi za Africa lakini Kama ukiwa umeiva haswa kushindana kimataifa na wao wakajiridhisha hivo basi wanakuchukua haraka sana.
Ni waafrica wachache sana wanaofanya kazi nchini Japan, wageni wengi wanatoka mataifa ya jirani ya Urusi, China na Korea kusini pia kuna wa-vietnam na wa-brazil na kiukweli tatzo la ajira Japan ni Kama hakuna fursa ziko nyingi mno nadhani inachagizwa na viwanda kuwa vingi tena vikubwa na kwa mwafrica ukiweza kumudu lugha ya ki-japan vizuri na tamaduni zao za ki-hiragana, ki-katakana na ki-kariji na kupata chance ya kuingia basi kazi hutokosa kwa vile asilimia chache tu ya Wajapan wanazungumza kiingereza ama la sivyo uajiriwe kampuni za kimataifa.
Kwa wenye ujuzi wa lugha za kimataifa Japan wanahitajika sana Kama watafsiri wa lugha Hawa kazi zao ziko njenje, waalimu wa kiingereza, watu wa software engineering, chemical engineering, IT na telecommunication, maafisa masoko, walinzi na wasaidizi wa ofisi.
Kupata Elimu nchini Japan ni ghali sana kuanzia level ya chini mpaka juu na ni waafrica wachache wanaosoma huko, mfumo wa elimu wao ni 6yrs (msingi), 3yrs(secondary), 3yrs(high school) na 4yrs University, kuna vyuo zaidi ya 1000 nchini Japan lakini serikali inamiliki vyuo visivyozidi 100 tu na vingi ni vya watu binafsi na mashirika na hii ndio inafanya vinakuwa ghali Mfano Mji niliokuwa nakaa wa Nagoya kuna chuo cha Nagoya University ada tu kwa baadhi ya kozi ilikuwa zaidi ya $25,000+ kabla ya michango mingine kwa mwaka na kwa maisha ya Nagoya kwa mwanafunzi wa kawaida kula chakula duni, malazi, umeme, usafiri, gasi, maji na gharama zingine kwa siku angalau unatakiwa uwe na $100+ kwa kujua hili serikali inalipia raia wake elimu bure wa wasioweza kumudu gharama hizi kuanzia chini mpaka chuo.
Mitaa ya Japan haiitwi kwa majina, inatumia namba za utambulisho kwa mpangilio maalum vivyo hivyo na nyumba pia watu wa posta huku hawapati tabu barua wanaweza kukuletea mpaka mlangonu kwako.
Nimewahi pia kutembelea mara kadhaa mji wa Hiroshima na Nagasaki hii miji yote ilipigwa mabomu katika vita ya pili 1945 na marekani ni mbali kidogo kutoka Nagoya umbali wa masaa 2 mpka 8 inategemea na usafiri unaotumia kutoka Nagoya tu mpaka Hiroshima kwa treni ya kasi (Bullet train) utatumia masaa 2 na kwa basi utapanda linaloenda jijini Kobe kupitia jiji la Osaka unashuka hapo halafu unachukua linaloenda Hiroshima hapo utalala na kujifunza historian ya hapo kesho yake safari tena ya masaa 3 mpaka 6 mapaka Nagasaki kupitia Fukuoka na Kitakyushu ni miji mizuri kwa sasa na inapendeza na shughuli za maisha huko zinaendelea Kama kawaida na mambo mengine yote yaliyopita yamebaki historia tu.
Kwenye starehe huu mji ulinipa shida sana, lugha ilikuwa kikwazo kujichanganya katika Night club nyingi za Japan nikaishia kuwa naenda zile zenye mchanganyiko wa wageni wengi Kama Club JB's na Club Buddha za jijini Nagoya na Casablanca night club na Butterfly za jijini Tokyo pamoja na changamoto za lugha Japan ndio nchi pekee ambayo nimeacha damu yangu baada ya kuzaa na msichana wa huko.
Parabora
Geneva -Switzerland
Chukua hatua stahiki, Corona ipo na ni hatari.