bukoba boy
JF-Expert Member
- Jan 15, 2015
- 5,370
- 3,962
Moja kati ya mafanikio ya karne ya 19 yalikua ni hii ndege. Makubaliano ''concord" kati ya serikali mbili ya Uingereza na Ufaransa ndio yaliozaa wazo la kutengeneza hii ndege na wakakubaliana waipe jina la kifaransa la Concorde yaani maana yake makubaliano(concord).
Ilikua na uwezo wa kubeba abiria 92 mpaka 108. Gharama ya uundaji wa ndege hiyo kwa mwaka 1977 ilikua ni £23m sawa na £128m kwa mwaka huu. Jumla ya ndege 20 pekee ziliundwa, 6 zikiwa sio kwa ajili ya matumizi ya kiraia. Ilikua inaendeshwa na "marubani" watatu, huyu wa tatu alikua ni mhandisi wa ndege.
Spidi yake ilikua mara mbili ya spidi ya sauti na ilikua na uwezo wa kuvuka bahari ya Atlantic (Washington DC mpaka London) kwa muda wa masaa matatu wakati kwa ndege ya kawaida si chini ya masaa saba yalikua yanahitajika kufanya hivyo.
Ilikua ina pua ambayo inaweza kurekebishika ili kufanya marubani waone vizuri uwanja wakati wa kupaa.
Na mazuri yote hayo, Concorde ikaanza kupata upinzani mkali kutoka kwa watu mbalimbali, kwanza hiyo spidi yake kubwa ilikua inasababisha kelele sana kwa watu walio ardhini, hivyo safari zake nyingi zikawa juu ya bahari.
Ilipofika kipindi cha miaka ya 1970 kutokana na uhaba wa mafuta(economic crisis), nchi nyingi ziliacha kutoa oda ya ndege hizo. Watumiaji wakubwa wakabaki kuwa ni Ufaransa na Uingereza zenyewe.
Katika kipindi chake kuanzia imeanza kutoa huduma ilikua na rekodi nzuri ya usalama isipokua mwaka 2000 huko Ufaransa, ndege iliungua wakati wa kupaa, hii ilisababishwa na pancha ya tairi iliyolipua tank la mafuta.
Na hatimaye ilipofika mwaka 2003 ndege zote zilistaafishwa kutoa huduma na sasa hivi zimehifadhiwa makumbusho.