Ifahamu ndege aina ya Concorde

Ifahamu ndege aina ya Concorde

Asante kwa kutujuza mkuu...ndege za aina yake kupata kutokea
 
Wakuu hizi klm 400 sawa na umbali wa kutoka wapi had wap mfano wake
 
Hii inavutia nadhani mbeleni watazirudisha kwa kigezo cha muda zaidi.
 
Unamaanisha kabla haijapaa ilibidi ikate hizo klm kwanza au?
Huo uwanja utakua ni kisanga
no haiwi hivyo.

hapo kwenye kuchochea inatumia distance fupi mno mpaka kufikia speed hiyo, kama viwanja 13 tu vya mpira, lakini mpaka kufika hapo inakuwa inakimbia kuliko chombo chochote cha ardhini labda train za umeme huko japan.

Sent from my G3226 using JamiiForums mobile app
 
Concorde - ilikuwa ndege ya abiria yenye spidi ya juu sana.

Concorde - mradi wake ulianza mapema miaka ya 1950, wakati Arnold Hall, mkurugenzi wa kampuni la Royal Aircraft Establishment (RAE), kumuomba mtaalamu mwenzake Morien Morgan kuunda kamati ya kutafiti dhana ya "usafiri wa kasi kubwa" (SST). Kikundi hicho cha watafiti kilikutana kwa mara ya kwanza mnamo Februari 1954 na kutoa ripoti yao ya kwanza mnamo Aprili 1955...hatimae baadae Concorde kuzaliwa.

Concorde - iliundwa kwa makubaliano ya serikali mbili za Ufaransa na Uingereza.

Concorde - maana yake ni makubaliano, maelewano au ushirikiano (jina hili waundaji wa ndege waliipa ndege hiyo kutokana na makubaliano ya serikali hizi mbili kama nilivosema hapo juu. Neno concorde ni la kifaransa likimaanisha hicho nilichoeleza juu lakini pia concorde ni mkabala na neno la kiingereza 'concord' ambalo lina maana hiyohiyo.

Concorde - ilitoa huduma hadi mwaka 2003.

Concorde -
ilikuwa na kasi ya juu zaidi ya kasi ya sauti (mara mbili), kwa kiwango cha Mach 2.04 (1,354 mph au 2,180 km / h ikiwa katika usawa wa kusepa 'cruise altitude').

Concorde - ilikuwa na uwezo wa kupakia abiria 92 hadi 128.

Concorde - ilirushwa kwa mara ya kwanza mnamo 1969, Concorde iliingia kwenye operesheni rasmi 1976 na kuendelea kuruka kwa miaka 27 iliyofuata.

Concorde - Ni moja kati ya ndege mbili za kipekee za abiria kuwahi kuundwa zenye spidi ya juu sana; nyingine ni Tupolev Tu-144 iliyojengwa na wa-Soviet, ambayo ilifanya kazi mwishoni mwa miaka ya 70.

Concorde - ni ndege iliyotumiwa sana na abiria tajiri ambao wangeweza kumudu bei kubwa ya nauli iliyotokana na kasi kubwa ya ndege na huduma za kiwango cha juu ndani ya ndege...... Kwa mfano, mnamo 1997, bei ya tiketi za safari ya kutoka New York kwenda London ilikuwa $ 7,995 (ambayo ni ulinganifu wa $ 12,700 kama nauli hiyo ingelipwa mwaka 2019), gharama ambayo ni mara 30 ya gharama ya nauli kwa usafiri wa ndege ya bei chee! kuruka njia hiyo hiyo.

Concorde - iliruka njia za baharini zaidi, kuzuia usumbufu wa 'Sonic boom' sound kwa raia ikiwa ingepita kwenye nchi kavu maeneo yenye watu...Boom sound ni ile sound ya mlipuko yenye makelele inayozalishwa na ndege zinazolala mbele kama hiyo. (Hii ilikuwa moja miongoni mwa sababu za kuistaafisha mbali na sababu nyingine za kiusalama)

Concorde - ruti zake zilikuwa chache zaidi ni kutoka Uwanja wa ndege wa Heathrow wa London na Uwanja wa ndege wa Charles de Gaulle wa Paris Ufaransa hadi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa John F. Kennedy huko New York, Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Washington Dulles huko Virginia na Uwanja wa ndege wa Grantley Adams huko Barbados; iliruka na kufika viwanja hivi chini ya nusu ya muda wa kuruka wa mashirika mengine ya ndege...yaani kama boeing anatumia saa 5 concorde angeruka 2.5hrs.

Concorde - ilirushwa na marubani wawili na injini wa ndege ambao wote kwa pamoja walishirikiana kulirusha dubwana hili matata!!.

Concorde -
pua lake lilikuwa na uwezo wa kujibinua ili kuwawezesha marubani kuona vizuri wanapotua na kupaa kwa sababu ya urefu wa pua lake.

Concorde - ilistaafu mnamo 2003, miaka mitatu baada ya ajali ya ndege ya Air France 4590, ambayo abiria wote na wafanyakazi walipoteza maisha...ajali hiyo ilisababishwa na bast ya tairi wakati wa kupaa ambapo mwako ulisababisha moto kwenye mojawapo ya injini.

Mbali na ajali hiyo kama sababu ya kustaafishwa kwa safari za Concorde...pia... kuanguka kwa biashara ya usafiri wa anga baada ya shambulio la Septemba 11 mnamo 2001 na kukoma kwa usaidizi wa matengenezo ya Concorde kutoka kampuni la Airbus (ambalo ndio mrithi wa Aérospatiale kampuni lililounda ndege hizi) pia kulichangia kustaafishwa kwa mwamba huyu wa anga ktk usafiri wa abiria.

Concorde - Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu Wa Za Banga anadai kwamba Concorde iliwahi kutua Congo huko kwenye uwanja wa ndege wa kijijini kwao Gbadolite ambako kulikuwa na kasli lake la kifahari...Kuku alipanda sana hili dege akienda kufanya shopping na kikazi huko ng'ambo.

Concorde: Mnamo, Aprili 1, 2019, Shirika la ndege la Emirates lilitangaza kwamba watazindua tena ndege hii maarufu, ili ianze tena kutumika ifikapo 2022.

PICHA: Concorde yenye kimkia chekundu: British Airways Concorde ikiwa na logo mpya ya BA mapema kwenye uwanja wa Ndege wa London-Heathrow, mwanzoni mwa 1980
250px-British_Concorde.jpg

220px-02.03.69_1er_vol_de_Concorde_(1969)_-_53Fi1931_-_cropped.jpg

PICHA (Black & white) Safari ya kwanza ya Concorde 001 mnamo 1969.

220px-Concorde_Ramp.jpg
Mfumo wa kuchota upepo wa Concorde.

fire-flight-Air-France-engine-Paris-plane-July-25-2000.jpg

PICHA: Mnamo Julai 25, 2000, Concorde ikiruka kutoka Paris kwenda New York City ilipata hitilafu kwneye injini muda mfupi baada ya kuruka wakati vipande vya mabaki ya tairi iliyopasuka viliposababisha tanki la mafuta kupasuka hatimae kuanzisha moto uliosababisha ajali ya ndege hiyo maarufu. Concorde iliangukia hoteli ndogo na mgahawa ambapo watu wote 109
main-qimg-6cce37444a7275f466882ae8e1529f41.jpg
waliokuwamo, ikiwa ni pamoja na abiria 100 wafanyakazi wa ndege 9, walikufa; watu wengine wanne ardhini waliuawa pia.

PICHA: Moja miongoni mwa mambo muhimu yanayoonyeshwa kwenye eneo la maonesho ya Concorde huko Hayes Way, Patchway, Bristol BS34 5BZ, Uingereza ni chumba cha marubani cha Concorde ambacho kinatajwa kuwa chumba chenye mfumo ulioshikana sana tofauti na mifumo mingine ya uongozaji ndege kwenye ndege nyingine. Mfumo huu kwa asilimia kubwa ni wa analojia na ulisukwa kwa umakini mkubwa.
 
Attachments

  • 220px-Concorde_landing_Farnborough_Fitzgerald.jpg
    220px-Concorde_landing_Farnborough_Fitzgerald.jpg
    7.9 KB · Views: 3
Subiri tupate mustakabali wa watia Nia Dodoma tutakuja kuchangia hii mada.
 
Concorde - ilikuwa ndege ya abiria yenye spidi ya juu sana.

Concorde - mradi wake ulianza mapema miaka ya 1950, wakati Arnold Hall, mkurugenzi wa kampuni la Royal Aircraft Establishment (RAE), kumuomba mtaalamu mwenzake Morien Morgan kuunda kamati ya kutafiti dhana ya "usafiri wa kasi kubwa" (SST). Kikundi hicho cha watafiti kilikutana kwa mara ya kwanza mnamo Februari 1954 na kutoa ripoti yao ya kwanza mnamo Aprili 1955...hatimae baadae Concorde kuzaliwa.

Concorde - iliundwa kwa makubaliano ya serikali mbili za Ufaransa na Uingereza.

Concorde - maana yake ni makubaliano, maelewano au ushirikiano (jina hili waundaji wa ndege waliipa ndege hiyo kutokana na makubaliano ya serikali hizi mbili kama nilivosema hapo juu. Neno concorde ni la kifaransa likimaanisha hicho nilichoeleza juu lakini pia concorde ni mkabala na neno la kiingereza 'concord' ambalo lina maana hiyohiyo.

Concorde - ilitoa huduma hadi mwaka 2003.

Concorde -
ilikuwa na kasi ya juu zaidi ya kasi ya sauti (mara mbili), kwa kiwango cha Mach 2.04 (1,354 mph au 2,180 km / h ikiwa katika usawa wa kusepa 'cruise altitude').

Concorde - ilikuwa na uwezo wa kupakia abiria 92 hadi 128.

Concorde - ilirushwa kwa mara ya kwanza mnamo 1969, Concorde iliingia kwenye operesheni rasmi 1976 na kuendelea kuruka kwa miaka 27 iliyofuata.

Concorde - Ni moja kati ya ndege mbili za kipekee za abiria kuwahi kuundwa zenye spidi ya juu sana; nyingine ni Tupolev Tu-144 iliyojengwa na wa-Soviet, ambayo ilifanya kazi mwishoni mwa miaka ya 70.

Concorde - ni ndege iliyotumiwa sana na abiria tajiri ambao wangeweza kumudu bei kubwa ya nauli iliyotokana na kasi kubwa ya ndege na huduma za kiwango cha juu ndani ya ndege...... Kwa mfano, mnamo 1997, bei ya tiketi za safari ya kutoka New York kwenda London ilikuwa $ 7,995 (ambayo ni ulinganifu wa $ 12,700 kama nauli hiyo ingelipwa mwaka 2019), gharama ambayo ni mara 30 ya gharama ya nauli kwa usafiri wa ndege ya bei chee! kuruka njia hiyo hiyo.

Concorde - iliruka njia za baharini zaidi, kuzuia usumbufu wa 'Sonic boom' sound kwa raia ikiwa ingepita kwenye nchi kavu maeneo yenye watu...Boom sound ni ile sound ya mlipuko yenye makelele inayozalishwa na ndege zinazolala mbele kama hiyo. (Hii ilikuwa moja miongoni mwa sababu za kuistaafisha mbali na sababu nyingine za kiusalama)

Concorde - ruti zake zilikuwa chache zaidi ni kutoka Uwanja wa ndege wa Heathrow wa London na Uwanja wa ndege wa Charles de Gaulle wa Paris Ufaransa hadi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa John F. Kennedy huko New York, Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Washington Dulles huko Virginia na Uwanja wa ndege wa Grantley Adams huko Barbados; iliruka na kufika viwanja hivi chini ya nusu ya muda wa kuruka wa mashirika mengine ya ndege...yaani kama boeing anatumia saa 5 concorde angeruka 2.5hrs.

Concorde - ilirushwa na marubani wawili na injini wa ndege ambao wote kwa pamoja walishirikiana kulirusha dubwana hili matata!!.

Concorde -
pua lake lilikuwa na uwezo wa kujibinua ili kuwawezesha marubani kuona vizuri wanapotua na kupaa kwa sababu ya urefu wa pua lake.

Concorde - ilistaafu mnamo 2003, miaka mitatu baada ya ajali ya ndege ya Air France 4590, ambayo abiria wote na wafanyakazi walipoteza maisha...ajali hiyo ilisababishwa na bast ya tairi wakati wa kupaa ambapo mwako ulisababisha moto kwenye mojawapo ya injini.

Mbali na ajali hiyo kama sababu ya kustaafishwa kwa safari za Concorde...pia... kuanguka kwa biashara ya usafiri wa anga baada ya shambulio la Septemba 11 mnamo 2001 na kukoma kwa usaidizi wa matengenezo ya Concorde kutoka kampuni la Airbus (ambalo ndio mrithi wa Aérospatiale kampuni lililounda ndege hizi) pia kulichangia kustaafishwa kwa mwamba huyu wa anga ktk usafiri wa abiria.

Concorde - Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu Wa Za Banga anadai kwamba Concorde iliwahi kutua Congo huko kwenye uwanja wa ndege wa kijijini kwao Gbadolite ambako kulikuwa na kasli lake la kifahari...Kuku alipanda sana hili dege akienda kufanya shopping na kikazi huko ng'ambo.

Concorde: Mnamo, Aprili 1, 2019, Shirika la ndege la Emirates lilitangaza kwamba watazindua tena ndege hii maarufu, ili ianze tena kutumika ifikapo 2022.

PICHA: Concorde yenye kimkia chekundu: British Airways Concorde ikiwa na logo mpya ya BA mapema kwenye uwanja wa Ndege wa London-Heathrow, mwanzoni mwa 1980View attachment 1541977

View attachment 1541978
PICHA (Black & white) Safari ya kwanza ya Concorde 001 mnamo 1969.

View attachment 1541981 Mfumo wa kuchota upepo wa Concorde.

View attachment 1541983
PICHA: Mnamo Julai 25, 2000, Concorde ikiruka kutoka Paris kwenda New York City ilipata hitilafu kwneye injini muda mfupi baada ya kuruka wakati vipande vya mabaki ya tairi iliyopasuka viliposababisha tanki la mafuta kupasuka hatimae kuanzisha moto uliosababisha ajali ya ndege hiyo maarufu. Concorde iliangukia hoteli ndogo na mgahawa ambapo watu wote 109 View attachment 1541990waliokuwamo, ikiwa ni pamoja na abiria 100 wafanyakazi wa ndege 9, walikufa; watu wengine wanne ardhini waliuawa pia.

PICHA: Moja miongoni mwa mambo muhimu yanayoonyeshwa kwenye eneo la maonesho ya Concorde huko Hayes Way, Patchway, Bristol BS34 5BZ, Uingereza ni chumba cha marubani cha Concorde ambacho kinatajwa kuwa chumba chenye mfumo ulioshikana sana tofauti na mifumo mingine ya uongozaji ndege kwenye ndege nyingine. Mfumo huu kwa asilimia kubwa ni wa analojia na ulisukwa kwa umakini mkubwa.
Halafu tunaendelea kuwaita hawa watu ni mabeberu. Tumeshindwa kuendeleza kiwanda chetu cha magari pale kibaha. Hongera sana mleta mada nimepata cha kuelezea kijijini kwetu. Barikiwa
 
no haiwi hivyo.

hapo kwenye kuchochea inatumia distance fupi mno mpaka kufikia speed hiyo, kama viwanja 13 tu vya mpira, lakini mpaka kufika hapo inakuwa inakimbia kuliko chombo chochote cha ardhini labda train za umeme huko japan.

Sent from my G3226 using JamiiForums mobile app
Vipi kuhusu ndege hi ya mrusi Antonov 225 inaaminika hii ndo ndege kubwa na yenye nguvu zaid ulimwenguni, suala lake la speed lipoje? Au speed ya kawaida Kama zingine
FB_IMG_1597836552740.jpg
 
Wakuu hizi klm 400 sawa na umbali wa kutoka wapi had wap mfano wake
400km/h ni speed ambayo inatakiwa kufikia ili Concorde iweze kuinuka na kupaa sio umbali lkn pia inaweza kutafsriwa zaidi kwa umbali hv km hakutakuwa na kikwazo chochote hii ndege inaweza kwenda umbali wa km 400 ndani ya saa 1!
 
Hii inavutia nadhani mbeleni watazirudisha kwa kigezo cha muda zaidi.

Kweli! Kigezo kikiwa kuokoa muda popote pale kitashinda!

Ila I hope wataziboresha zaidi ya zilivyokua kwenda sambamba na uhitaji. Bado zinaumuhimu wake !
 
Back
Top Bottom