isajorsergio
Platinum Member
- Apr 22, 2018
- 4,143
- 6,560
Premier League, ligi kuu soka ya Uingereza ikifahamika vyema hapo awali kama BPL kabla ya mabadiliko mnamo mwaka 2015 toka BPL iliyokuwa ikiuza kupitia chapa ya Barclays Premier League chini ya mkataba wa udhamini kutoka kampuni maarufu inayoshughulika na masuala ya kiuchumi, fedha, uwekezaji na mabenki - Barclays. 2015 urasimishaji uliipatia uhuru ligi kuu hii na kutengeneza chapa ya upekee isiyohitaji ununuliwaji. Ni muda sasa duniani kote kumekuwa kukishuhudiwa urushwaji wa matangazo ya kandanda kupitia televisheni na redio, matangazo murua yenye muonekano ang'avu, sauti imara na ubunifu wa upekee.
Chapa ya Premier League katika mitindo na muonekano tofauti.
Premier League hapo awali haikuwa na nguvu kama chapa na ndio maana baada ya mkataba wa muungano baina ya PL na Barclays, Premier League iliamua kuanza kutengeneza picha yake yenyewe katika jamii. Ubinifu akinifu kutoka kwa taasisi, kampuni na wabunifu mbalimbali ndio waliowezesha kutengeneza chapa unayoishuhudia kila wiki. Ni ushirika baina ya DesignStudio wale waliokuletea chapa za Airbnb, Deliveroo, GAP na Treatwell na DixonBaxi waandaaji chapa na mifumo ya picha mchocheo 'Graphics System' unazoziona leo, kuanzia maneno ya ufunguzi (Opening Titles), picha mchocheo (Graphics), video mchocheo (Animations), bao zenye kukutanisha timu (Hand Shake Boards), masuala ya uchapaji (Printing Collateral) na tiketi (Tickets).
Bao za kukutanisha timu.
Ushirika baina ya DesignStudio na DixonBaxi.
Ubunifu huu ulizingatia desturi, asili na kutofungamana baina ya PL na vilabu. Ndio mwanzo wa rangi zilizotanabaishwa kuwa za 'kike' na wafuasi wengi wa kandanda ulemwenguni lakini muda ulivyojongea uhalisia ukabaki mahala pake, na sasa ni wazi mvuto umezidi kuipa dili mbalimbali PL. Amewahi kueleza Bw. Maxence Melo
Mfumo wa machapisho ya Premier League.
Je Premier League Production ufanyaje kazi? - Premier League Production ni shirika linalohusika moja kwa moja katika shughuli za uaandaji, uchakataji na urushaji matangazo kwa ushirikiano mkubwa na IMG kupitia PLP. Mechi 380, Magazine Shows na Televisheni inayorusha vipindi na matangazo 24/7 ikiwa inasaidiwa na vituo washirika. Urushaji wa matangazo umefikia ubora 4KHD, huku PLP ikiwa nyuma ya teknolojia ya VAR Live (Checking) inayoandaliwa moja kwa moja kutoka Stockley Park - IMG Studios.
Premier League Production husimamia uchukuaji maudhui katika viwanja 20 kwa kutumia ungamuaji wa IP Networks, Nevion VS 902, Nevion nSure FCS 1000 Plus kwa uchache, hapa urushwaji uanza kuendelezwa kupitia VideoIPath - Management and Orchestration hadi kuingia ndani ya jengo lenye ghorofa tatu IMG Studios. Kabla ya kufika IMG Studios, PLP hutumia wastani wa kamera 15 katika kila kiwanja wakati wa uchukuaji maudhui mubashara. Kamera nyingi zinazotumika ni Arri, GoPro, Leica na Pentax.
Maudhui yafikapo IMG wataalamu mbalimbali uanza uchakataji na urushaji wa matangazo hayo mubashara. Uchakataji huu wa maudhui uzingatia kanuni na muongozo ya chapa husika PL. Kwa kutumia muundo uliondaliwa tayari na DesignStudio na DixonBaxi.
Muonekano wa muongozo kabla ya kuchanganywa na maudhui kutoka uwanjani.
Muundo wa muda kabla ya kuchanganywa na maudhui kutoka uwanjani.
Uchanganyaji picha hufanyika.
Baada ya uchanganyaji maudhui.
PLP na IMG zimekuwa nyuma ya ligi nyingine vilevile. La Liga, Bundesliga na Seria A zimekuwa zikiishirikisha PLP na IMG kusaidia mambo baadhi katika mifumo ya urushaji matangazo.
Chapa ya Premier League katika mitindo na muonekano tofauti.
Premier League hapo awali haikuwa na nguvu kama chapa na ndio maana baada ya mkataba wa muungano baina ya PL na Barclays, Premier League iliamua kuanza kutengeneza picha yake yenyewe katika jamii. Ubinifu akinifu kutoka kwa taasisi, kampuni na wabunifu mbalimbali ndio waliowezesha kutengeneza chapa unayoishuhudia kila wiki. Ni ushirika baina ya DesignStudio wale waliokuletea chapa za Airbnb, Deliveroo, GAP na Treatwell na DixonBaxi waandaaji chapa na mifumo ya picha mchocheo 'Graphics System' unazoziona leo, kuanzia maneno ya ufunguzi (Opening Titles), picha mchocheo (Graphics), video mchocheo (Animations), bao zenye kukutanisha timu (Hand Shake Boards), masuala ya uchapaji (Printing Collateral) na tiketi (Tickets).
Bao za kukutanisha timu.
Ushirika baina ya DesignStudio na DixonBaxi.
Ubunifu huu ulizingatia desturi, asili na kutofungamana baina ya PL na vilabu. Ndio mwanzo wa rangi zilizotanabaishwa kuwa za 'kike' na wafuasi wengi wa kandanda ulemwenguni lakini muda ulivyojongea uhalisia ukabaki mahala pake, na sasa ni wazi mvuto umezidi kuipa dili mbalimbali PL. Amewahi kueleza Bw. Maxence Melo
"...English Premium League kabla ya changes ikiwa inaitwa Barclays wao walibadili kabisa hadi rangi zao. Watu walijiapiza hawataangalia EPL wengine wakidai ni rangi za kike!" - @Maxence Melo
Mfumo wa machapisho ya Premier League.
Premier League Production husimamia uchukuaji maudhui katika viwanja 20 kwa kutumia ungamuaji wa IP Networks, Nevion VS 902, Nevion nSure FCS 1000 Plus kwa uchache, hapa urushwaji uanza kuendelezwa kupitia VideoIPath - Management and Orchestration hadi kuingia ndani ya jengo lenye ghorofa tatu IMG Studios. Kabla ya kufika IMG Studios, PLP hutumia wastani wa kamera 15 katika kila kiwanja wakati wa uchukuaji maudhui mubashara. Kamera nyingi zinazotumika ni Arri, GoPro, Leica na Pentax.
Muonekano wa muongozo kabla ya kuchanganywa na maudhui kutoka uwanjani.
Muundo wa muda kabla ya kuchanganywa na maudhui kutoka uwanjani.
Muongozo mkuu wa yapi yafanyike wakati wa uchakataji na urushaji matangazo.
Uchanganyaji picha hufanyika.
Baada ya uchanganyaji maudhui.