DStv hununua haki za matangazo Premier League Production (PLP) ambayo imepewa idhini na Premier League. PLP yenyewe inashirikiana na IMG Studios kiutendaji. Sio tu DStv bali televisheni zote zinazouza maudhui. Ni sawa na Ligu Kuu kuwa na kitengo au taasisi iliyochini yake inayofahamika kama Ligi Kuu Productions ambayo yafaa kusimamia maudhui. uzarishaji. uchakataji na usambazaji kwa Azam TV, GoTV, Startimes, Wasafi and co. katika packages tofauti, kwa sasa anayefanya hivyo ni Azam Productions anayegawa Azam TV inayosambaza maudhui kupitia Azam Sports Channels.
TFF, TPLB na Ligu Kuu zinatakiwa kujitenga kiutendaji katika ligi na kufanya uwekezaji wa masuala kama haya! Hasa katika masuala maudhui yafaa uwekezaji kutoka TFF na TPLB na washirika/wadhamini kuwekeza ndani ya taasisi ya Ligi Kuu kufanikisha haya.