Ifahamu sayari ya Mars...

Ifahamu sayari ya Mars...

pluto ni ya ngapi kwa udogo?
dadawazungu wahuni sana miaka yote tulikuwa shule tunajifunza kuwa pluto ni sayari ila kufika chuo wakasema haina sifa ya kuwa sayari ,sasasiku wakisema yule Yesu sio tuliyemkusudia si tutaamini
 
Sio uhuni wa wazungu mkuu

Sayansi sio kama vitabu vya dini ambavyo huwezi kuvikosoa

Sayansi inaruhusu kukosolewa na huo ndio uzuri wake

Kwenye newtonian mechanics tunaambiwa mwanga ni mionzi
Lakini quantum physics utaambiwa ni particle/punje

Kwahio usishangae
 
Bila shaka nitakuwa nazeeka kwa kasi sana, maana sijakupata kabisa japo nimerudia mara 7 kusoma.
Maana yake ni kwamba kilogram ni SI unit ya Mass kwa Kiswahili ni tungamo. Na mass/tungamo ni kiasi cha maada kinachounda kitu, hivyo hakibadiliki hata ukienda wapi. Ila uzito ambao ni weight kwa kiingereza SI unit yake ni Newton ambapo uzito ni zao/product ya mass/tungamo na acceleration due to gravity "g" ambayo ni 9.8 m/s^2. Hiyo "g" ndiyo inayobalika na ndiyo maana uzito unabadilika ila tungamo halibadiliki. Kwa mfano kwenye mbalamwezi "g" ya huko ni 1/6 ya hapa duniani. Ukiwa na uzito wa 60N hapa duniani basi kwenye mbalamwezi itakuwa ni(1/6×9.8)×60.
 
Haya yooooooooooooooooooote nayajua na mimi kushangaa hivo lengo langu ni kuona akinielezea ili nione nipo na watu kwa kiasi gani na ni wafuatiliaji wa kiwango gani,lakini kuonyesha nakielewa alichokieleza nikaleta link yenye kuonyesha tofauti ya hivo vitu kwa undani zaidi. Lakini nashukuru kwa uwepo wako na kushiriki,haya sasa jazia vitu vingine vinavyoihusu sayari ya Mars.
 
Natumai mko poa wakuu.

Leo tunaendelea tena na kufahamishana juu ya madude yaliyo ktk mfumo wetu wa jua, hebu tuiangalie sayari ya Mars kwa undani zaidi.

1. Sayari ya Mars ni ya nne (4) kutoka umbali wa jua.

2. Ni sayari ya 2 kwa udogo baada ya sayari ya Mercury.

3.Ina miezi (moons) 2 ambayo ni midogo,ambapo mkubwa unakisiwa kuwa km 11 na mwingine km 6.2.

4. Mars ni terrestrial planet. (yaani ina ardhi kama yetu duniani)

5. Nguvu yake ya uvutano (gravity) ni sawa na kusema ukiwa Mars hatua yako ya kawaida huku duniani, ukiwa kule Mars inakuwa zaidi ya mara tatu na nusu. ( kwahiyo utakuwa kama unarukaruka)

6. Kilo zako za duniani unazipunguza kwa 38. (kwa mfano ukiwa na kilo 65 huku, kule utakuwa na kilo 27.)

7. Mars ulizunguuka jua kwa siku (days) 687,na hivi ndio inavyolizunguuka jua.

170px-Marsorbitsolarsystem.gif

8. Ni sayari iliyotembelewa na vyombo vingi sana kutoka duniani.

Na hapa ni jinsi miezi yake miwili,phobos na deimos inavyoizunguuka Mars.

Orbits_of_Phobos_and_Deimos.gif

Haya sasa ONGEZEENI AU PUNGUZENI NA KAMA VIPI REKEBISHENI ILI TUELIMISHANE ZAIDI.

Ahsante Mkuu kwa darasa zuri
 
Umesema nirekebishe,lakini ujaniambia niweke ngapi ......... lakini isiwe kesi hii hapa tebo inayoonyesha kwenye kila planet utakuwa na uzito kiasi gani, wewe naona umeshindwa kuleta.

weight-on-other-planets-infographic-110627c-02.jpg
Your mass is the same wherever you are--on Earth, on the moon, floating in space--because the amount of stuff you're made of doesn't change.
mass is a measurement of how much matter is in an object; weight is a measurement of how hard gravity is pulling on that object.
 
Jamaa yupo sahihi tofautisha mass na weight hiyo table uliyoweka hapo inaendana na weight na siyo mass, mass kizio ni kg, gram na weight ambayo SI unit yake ni Newton(N). Kwa mfano we mass yako ni 100kg basi weight yako ni 1000. Weight=mass*gravity, kwa hiyo gravity inatofautiana kutoka sayari moja hadi nyingine ambayo dunia kimakadirio ni 10.

Nyie wanasayansi bwana mnatuletea mbwembwe ...sasa sisi 'ma-nguin' tutaelewaje hapo???? mnatuchanganya bwana....tehtehtehteh Ndiyo maana Archimedes alitoka uchi kutoka bafuni na kukimbia ovyo mitaani(na kupiga kelele eureka, eureka, eureka) baada ya kugundua 'the volume of the water displaced is equal to the mass of the object immersed into water' (sijui nimepatia hapa ni physics yangu ya Form Four)....alikuwa ana
 
_93865332_794c7868-6746-4412-ab46-14466ca6e284.jpg

Haki miliki ya pichaNASA
Picha hii ya kwanza kabisa ya Mars ilipigwa na chombo kwa jina Viking 1 mwaka 1976
Sayari ya Mars imekuwa ikiwashangaza, kuwasisimua na kuwavutia binadamu kwa miaka mingi.

Maelfu ya miaka iliyopita, binadamu walikuwa wakishangaa na kujiuliza nini kinapatikana katika sayari hiyo inayopatikana umbali wa kilomita milioni 54.6 kutoka kwa dunia (maili milioni 34).

Sana, kutokana na muonekano wake wa rangi nyekundu sawa na ya chuma iliyoshika kutu, binadamu waliihusisha na moto au damu.

Jina Mars linatokana na mungu wa vita wa Warumi.

Kutokana na ufanisi wa kisayansi, binadamu kwa sasa amefanikiwa kufahamu mengi kuhusu sayari hii.

Sayari hii ina mandhari ya kushangaza: utayapata maeneo sawa na ya nyika duniani, maeneo ya jangwa kutokana na upepo mkali, mashimo makubwa yanayotokana na volkano, milima ya volkano na maeneo ya ukubwa sawa na taifa la Luxembourg yaliyojaa milima (machungu) ya mchanga.

Haya yote yamefunikwa na vumbi ya rangi moja.
_93866396_a885ad0b-7b53-4061-9da6-d28cf9437c8e.jpg

Haki miliki ya pichaNASA/JPL-CALTECH/UNIVERSITY OF ARIZONA
Mars ina milima (machungu) ya mchanga ya kupendeza
Ni eneo ambalo huwa hakuna mvua kamwe. Hakuwezekani kuwa na mvua kwani maji, iwapo yangekuwepo, hufusha na kuwa mvuke mara moja.

Katika sayari ya Mars, wakati sawa na wa kutua kwa jua duniani, anga hujaa rangi ya buluu. Dunia huonekana tu kama nukta tu miongoni mwa nyota angani.

Ni mandhari ya kupendeza sana hasa kwa wanaopenda utalii - ikizingatiwa kwamba binadamu hajatalii sana sayari hiyo, kuna uhakika kwamba iwapo utafanikiwa kufika huko, kila utatapoenda utakuwa binadamu wa kwanza kufika huko.

Utakuwa kama Wazungu waliokuwa wanatalii Afrika karne ya 19, ambapo walikuwa Wazungu wa kwanza kutazama milima, mito, nyika na misitu ya kupendeza barani. Lakini kumbuka kwamba hakuna oksijeni.

Utafikaje huko
Kwa karne nyingi, imekuwa ndoto tu lakini inakaribia kutimia. Iwapo mambo yote yatakwenda sawa, mjasiriamali mmiliki wa Space X Elon Musk anapanga kutuma kundi la kwanza la watalii kwenye sayari hiyo kufikia 2022.

Lakini gharama yake itakushangaza pengine. Tiketi ni $10bn! Lakini iwapo huwezi kupata pesa nyingi kiasi hiki, usife moyo. Kuna njia nyingine ya kiteknolojia ambayo taasisi ya safari za anga za juu ya Marekani Nasa inatafakari - kutumia miwani ya kisasa na roboti. Roboti ndiyo itakuwa Mars, wewe uwe papa hapa duniani lakini itakuwa ikikupeperushia picha za uhalisia kutoka sayari hiyo.

Vivutio sayari ya Mars
Kivuti kikuu ni mlima wa Olympus Mons. Mlima huu una urefu wa maili 14 (kilomita 22), na ndio mlima wa volcano mrefu zaidi katika Mfumo wa Jua. Kwa kulinganisha tu, urefu wa mlima huu ni mara tatu urefu wa mlima mrefu zaidi duniani, Mlima Everest.

Sawa na ilivyo kwa milima mirefu ya volkano duniani, mlima huu kilele chake kimefunikwa na mawingu - lakini si ya maji, bali ni ya vumbi.

Haijabainika iwapo mlima huu bado hulipuka, lakini inakadiriwa kwamba wakati mmoja ulilipuka na kurusha matope na mawe makubwa ya moto angani.

Ukisafiri kusini magharibi kutoka kwa mlima huu, utapata Valles Marineris.

Hili ni bonde kubwa kwenye ikweta ya sayari ya Mars. Bonde hili linakadiriwa kuwa na umbali wa kilomita 4,000 ambao ni karibu na upana wa taifa la Marekani kutoka mashariki hadi magharibi.

Katika baadhi ya maeneo, bonde hili lina kina cha karibu kilomita saba (futi 23,000) - karibu mara nne kina cha bonde maarufu la Marekani ambalo kwa Kiingereza hufahamika kama Grand Canyon.

_93865334_65fe9bce-4ad7-4565-bb75-d2e74002a065.jpg

Haki miliki ya pichaNASA/JPL-CALTECH/UNIVERSITY OF ARIZONA

Milima mingi Mars ina mito midogo ambayo inadhaniwa kuwa inatokana na michirizi ya maji yenye chumvi
Kufikia sasa, haijabainika bonde kubwa kiasi hiki liliundwa.

Bonde hili la Valles Marineris lina mchanga wenye marangi mbalimbali ya kupendeza ambao umejipanga kwa safu mbalimbali. Inadhaniwa kwamba huenda mchanga huu ulitokana na mashapo au machenga ambayo yalijikusanya chini ya ziwa au mto wa barafu, au kutokana na kujikusanya kwa majivu ya volcano.

Kinyume na bonde la Grand Canyon Marekani, ambalo liliundwa na mmomonyoko uliochota mchanga na kuyachonga mawe, kuna uwezekano kwamba bonde hili la Mars lilitokana na kutengana kwa maeneo mawili makubwa ya 'ardhi' ya Mars. Kila upande wa bonde hilo unaweza kuingia kwa ule mwingine, kana kwamba mtu anajaza mchezo wa fumbo.

Rangi ya anga
_93865331_41dec621-13f6-45a4-bc45-7d7eee46b153.jpg
Haki miliki ya pichaNASA
Image captionWakati wa kutua kwa jua, anga huwa la rangi ya samawati
Ukafanikiwa kujipata kwenye bonde hili, na uwe unataka kuangalia kutua kwa jua, utashangaa kugundua kwamba anga lake halitakuwa ya rangi nyekundu - bali ya samawati. Hii inatokana na wepesi wa anga la sayari ya Mars, ambalo ni asilimia moja tu ya uzito wa anga la Dunia.

Anga la Dunia huwa rangi ya samawati mchana kutokana na miali ya jua kutawanywa na molekuli za hewa. Hili huwa halitendeki sana sayari ya Mars, hivyo mchana anga huwa la rangi ya manjano iliyokaribia hudhurungi. Lakini jua linapotua, ambapo miali yake huwa haina nguvu sana ndipo anga la Mars hugeuka na kuwa rangi ya buluu.

Sayari ya Mars pia ina jambo jingine la kushangaza. Katika maeneo mengi, chini ya vumbi lake jekundu, kuna mawe ya rangi ya samawati na kijani kutokana na madini kama vile chuma. Vumbi hilo linapobebwa na upepo au kutokana na kupita kwa sayari ndogo, huwa kunafichuliwa mandhari ya kupendeza ya mikolezo tofauti ya rangi ya samawati.

Hali ya hewa
Kiwango cha joto cha kadiri katika sayari ya Mars ni nyuzi joto takriban -56C (-69F). Hii ni sawa na hali ya baridi maeneo ya ndani kabisa ya Antarctica, anasema mtaalamu wa biolojia na anga za juu katika Chuo Kikuu cha Washington, David Catling.

Ndipo uweze kufurahia, itakubidi kukaa karibu na ikweta ya Mars, ambapo huko kiwango cha joto kinaweza kufikia takriban 35C (95F), na hakuna upepo sana. Kutokana na wepesi wa anga lake, upepo mkali huko utahisi kana kwamba ni upepo tu Ingawa huwa kuna unyevu na ukungu usiku katika sayari hiyo, mchana hali ni kavu sana.

Kutokana na hali kwamba sayari hiyo inapatikana karibu mara moja unusu mbali na jua ukilinganisha na Dunia, hakuna haja ya kuvalia miwani ya kukinga dhidi ya mwanga wa jua.

Huko, kuwasha moto pia ni ngoma kwani hakuna mimea na anga lake asilimia 96 ni kaboni daoksaidi - kemikali inayotumiwa kwenye mitambo mingi ya kuzima moto.

Tofauti na Dunia, ambapo mawingu na anga hufanya kazi kama blanketi na kuzuia joto kuondoka usiku, sayari ya Mars hakuna mawingu na anga lake ni jepesi sana. Matokeo yake ni kwamba, sawa na inavyofanyika jangwani, usiku huwa kuna baridi kali sana. Baridi hii inaweza kufikia nyuzi -73C (-99F) usiku karibu na ikweta kwenye sayari hiyo.

Kuna viumbe walio hai?
_93866398_486ff79c-e090-43a8-9581-fdfa84c62d84.jpg
Haki miliki ya pichaNASA/JPL
Image captionRoboti hii ilipiga picha ya kwanza ya kujipiga (almaarufu selfie) katika Mars
Viumbe wote walio hai duniani huwa wana maji ndani yake. Hivyo, wataalam wamekuwa wakiamini kwamba iwapo kuna viumbe Mars, lazima wawe kwenye maeneo yaliyo na maji.

Kwa miongo mingi, wanasayansi walitafuta ishara za kuwepo maji Mars bila mafanikio.

Lakini mwaka 2011, walifanya ugunduzi huo. Waligundua michirizi ya maji yaliyokuwa yakitiririka kutoka kwa milima na mabonde ya Mars. Inadhaniwa kwamba huenda mito, yenye maji yenye chumvi labda huchipuza kutoka chini ya 'ardhi' kwenye hazina kubwa ya maji.

Binadamu hubadilika?
Kutokana na kiwango cha chini ya nguvu mvuto, uzani wa vitu huwa tofauti sayari ya Mars. Binadamu wa kilo 100 hivi, uzani wake Mars unaweza kuwa karibu na kilo 38 hivi.

Ukafanikiwa kutua kwenye Mars, utakuwa ukiitazama Dunia na kuiona kama tone au kituo angani. Dunia utaiona ikiwa sawa na tunavyoiona sayari ya Zuhura mapema asubuhi, au jioni angani, anasema Catling.

Chanzo: BBC
 
Mimi nna swali mkuu je kutokana na hiyo mito iliyogundulika kutakuwa kuna viumbe?
 
Mars ni ngumu kwa kiumbe hai kuishi maana hakuna oxygen ndio maana hakuna mawingu wala ozone lay uwwezekano wa kuwa na mvua ni mdogo maana hakuna Maji ila utafiti unaendelea maana inaonekana sehemu kubwa ni bahari Maji yameganda
 
Sayari ya Mars imekuwa ikiwashangaza, kuwasisimua na kuwavutia binadamu kwa miaka mingi.

Maelfu ya miaka iliyopita, binadamu walikuwa wakishangaa na kujiuliza nini kinapatikana katika sayari hiyo inayopatikana umbali wa kilomita milioni 54.6 kutoka kwa dunia (maili milioni 34).

Sana, kutokana na muonekano wake wa rangi nyekundu sawa na ya chuma iliyoshika kutu, binadamu waliihusisha na moto au damu.

Jina Mars linatokana na mungu wa vita wa Warumi.

Kutokana na ufanisi wa kisayansi, binadamu kwa sasa amefanikiwa kufahamu mengi kuhusu sayari hii.

Sayari hii ina mandhari ya kushangaza: utayapata maeneo sawa na ya nyika duniani, maeneo ya jangwa kutokana na upepo mkali, mashimo makubwa yanayotokana na volkano, milima ya volkano na maeneo ya ukubwa sawa na taifa la Luxembourg yaliyojaa milima (machungu) ya mchanga.

Haya yote yamefunikwa na vumbi ya rangi moja.

Ni eneo ambalo huwa hakuna mvua kamwe. Hakuwezekani kuwa na mvua kwani maji, iwapo yangekuwepo, hufusha na kuwa mvuke mara moja.

Katika sayari ya Mars, wakati sawa na wa kutua kwa jua duniani, anga hujaa rangi ya buluu. Dunia huonekana tu kama nukta tu miongoni mwa nyota angani.

Ni mandhari ya kupendeza sana hasa kwa wanaopenda utalii - ikizingatiwa kwamba binadamu hajatalii sana sayari hiyo, kuna uhakika kwamba iwapo utafanikiwa kufika huko, kila utatapoenda utakuwa binadamu wa kwanza kufika huko.

Utakuwa kama Wazungu waliokuwa wanatalii Afrika karne ya 19, ambapo walikuwa Wazungu wa kwanza kutazama milima, mito, nyika na misitu ya kupendeza barani. Lakini kumbuka kwamba hakuna oksijeni.

Utafikaje huko

Kwa karne nyingi, imekuwa ndoto tu lakini inakaribia kutimia. Iwapo mambo yote yatakwenda sawa, mjasiriamali mmiliki wa Space X Elon Musk anapanga kutuma kundi la kwanza la watalii kwenye sayari hiyo kufikia 2022.

Lakini gharama yake itakushangaza pengine. Tiketi ni $10bn! Lakini iwapo huwezi kupata pesa nyingi kiasi hiki, usife moyo. Kuna njia nyingine ya kiteknolojia ambayo taasisi ya safari za anga za juu ya Marekani Nasa inatafakari - kutumia miwani ya kisasa na roboti. Roboti ndiyo itakuwa Mars, wewe uwe papa hapa duniani lakini itakuwa ikikupeperushia picha za uhalisia kutoka sayari hiyo.

Vivutio sayari ya Mars

Kivuti kikuu ni mlima wa Olympus Mons. Mlima huu una urefu wa maili 14 (kilomita 22), na ndio mlima wa volcano mrefu zaidi katika Mfumo wa Jua. Kwa kulinganisha tu, urefu wa mlima huu ni mara tatu urefu wa mlima mrefu zaidi duniani, Mlima Everest.

Sawa na ilivyo kwa milima mirefu ya volkano duniani, mlima huu kilele chake kimefunikwa na mawingu - lakini si ya maji, bali ni ya vumbi.

Haijabainika iwapo mlima huu bado hulipuka, lakini inakadiriwa kwamba wakati mmoja ulilipuka na kurusha matope na mawe makubwa ya moto angani.

Ukisafiri kusini magharibi kutoka kwa mlima huu, utapata Valles Marineris.

Hili ni bonde kubwa kwenye ikweta ya sayari ya Mars. Bonde hili linakadiriwa kuwa na umbali wa kilomita 4,000 ambao ni karibu na upana wa taifa la Marekani kutoka mashariki hadi magharibi.

Katika baadhi ya maeneo, bonde hili lina kina cha karibu kilomita saba (futi 23,000) - karibu mara nne kina cha bonde maarufu la Marekani ambalo kwa Kiingereza hufahamika kama Grand Canyon.

Kufikia sasa, haijabainika bonde kubwa kiasi hiki liliundwa.

Bonde hili la Valles Marineris lina mchanga wenye marangi mbalimbali ya kupendeza ambao umejipanga kwa safu mbalimbali. Inadhaniwa kwamba huenda mchanga huu ulitokana na mashapo au machenga ambayo yalijikusanya chini ya ziwa au mto wa barafu, au kutokana na kujikusanya kwa majivu ya volcano.

Kinyume na bonde la Grand Canyon Marekani, ambalo liliundwa na mmomonyoko uliochota mchanga na kuyachonga mawe, kuna uwezekano kwamba bonde hili la Mars lilitokana na kutengana kwa maeneo mawili makubwa ya 'ardhi' ya Mars. Kila upande wa bonde hilo unaweza kuingia kwa ule mwingine, kana kwamba mtu anajaza mchezo wa fumbo.

Rangi ya anga

Ukafanikiwa kujipata kwenye bonde hili, na uwe unataka kuangalia kutua kwa jua, utashangaa kugundua kwamba anga lake halitakuwa ya rangi nyekundu - bali ya samawati. Hii inatokana na wepesi wa anga la sayari ya Mars, ambalo ni asilimia moja tu ya uzito wa anga la Dunia.

Anga la Dunia huwa rangi ya samawati mchana kutokana na miali ya jua kutawanywa na molekuli za hewa. Hili huwa halitendeki sana sayari ya Mars, hivyo mchana anga huwa la rangi ya manjano iliyokaribia hudhurungi. Lakini jua linapotua, ambapo miali yake huwa haina nguvu sana ndipo anga la Mars hugeuka na kuwa rangi ya buluu.

Sayari ya Mars pia ina jambo jingine la kushangaza. Katika maeneo mengi, chini ya vumbi lake jekundu, kuna mawe ya rangi ya samawati na kijani kutokana na madini kama vile chuma. Vumbi hilo linapobebwa na upepo au kutokana na kupita kwa sayari ndogo, huwa kunafichuliwa mandhari ya kupendeza ya mikolezo tofauti ya rangi ya samawati.

Hali ya hewa

Kiwango cha joto cha kadiri katika sayari ya Mars ni nyuzi joto takriban -56C (-69F). Hii ni sawa na hali ya baridi maeneo ya ndani kabisa ya Antarctica, anasema mtaalamu wa biolojia na anga za juu katika Chuo Kikuu cha Washington, David Catling.

Ndipo uweze kufurahia, itakubidi kukaa karibu na ikweta ya Mars, ambapo huko kiwango cha joto kinaweza kufikia takriban 35C (95F), na hakuna upepo sana. Kutokana na wepesi wa anga lake, upepo mkali huko utahisi kana kwamba ni upepo tu Ingawa huwa kuna unyevu na ukungu usiku katika sayari hiyo, mchana hali ni kavu sana.

Kutokana na hali kwamba sayari hiyo inapatikana karibu mara moja unusu mbali na jua ukilinganisha na Dunia, hakuna haja ya kuvalia miwani ya kukinga dhidi ya mwanga wa jua.

Huko, kuwasha moto pia ni ngoma kwani hakuna mimea na anga lake asilimia 96 ni kaboni daoksaidi - kemikali inayotumiwa kwenye mitambo mingi ya kuzima moto.

Tofauti na Dunia, ambapo mawingu na anga hufanya kazi kama blanketi na kuzuia joto kuondoka usiku, sayari ya Mars hakuna mawingu na anga lake ni jepesi sana. Matokeo yake ni kwamba, sawa na inavyofanyika jangwani, usiku huwa kuna baridi kali sana. Baridi hii inaweza kufikia nyuzi -73C (-99F) usiku karibu na ikweta kwenye sayari hiyo.

Kuna viumbe walio hai?

Viumbe wote walio hai duniani huwa wana maji ndani yake. Hivyo, wataalam wamekuwa wakiamini kwamba iwapo kuna viumbe Mars, lazima wawe kwenye maeneo yaliyo na maji.

Kwa miongo mingi, wanasayansi walitafuta ishara za kuwepo maji Mars bila mafanikio.

Lakini mwaka 2011, walifanya ugunduzi huo. Waligundua michirizi ya maji yaliyokuwa yakitiririka kutoka kwa milima na mabonde ya Mars. Inadhaniwa kwamba huenda mito, yenye maji yenye chumvi labda huchipuza kutoka chini ya 'ardhi' kwenye hazina kubwa ya maji.

Binadamu hubadilika?

Kutokana na kiwango cha chini ya nguvu mvuto, uzani wa vitu huwa tofauti sayari ya Mars. Binadamu wa kilo 100 hivi, uzani wake Mars unaweza kuwa karibu na kilo 38 hivi.

Ukafanikiwa kutua kwenye Mars, utakuwa ukiitazama Dunia na kuiona kama tone au kituo angani. Dunia utaiona ikiwa sawa na tunavyoiona sayari ya Zuhura mapema asubuhi, au jioni angani, anasema Catling.
8ceb56629f6744f1ef0f91c9e0b80309.jpg
7eca70dd23072b7e84d74fa36c95e36e.jpg
5aaa216a6f1b215a1d9471c309438d2c.jpg
 
Back
Top Bottom