JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
SHERIA YA USALAMA BARABARANI YA 1973 INAELEZA NINI KUHUSU MWENDOKASI?
Kifungu cha 51 (8) kinatamka pamojanna mambo mengine
(a) Katika maeneo ya makazi mwendokasi usizidi kilomita 50 kwa saa
(b) Katika maeneo ambayo si makazi, mwendokasi utadhibitiwa kwa alama za barabarani
(c) Magari yanayozidi tani 3500 hayatazidisha kilomita 80 kwa saa
AJALI SHERIA YA BARABARANI, SURA YA 168 YA MWAKA 1973 INA MAPUNGUFU
(a) Sheria inatambua maeneo machache sana katika kuzuia mwendokasi. Kuna maeneo mengi hayajatambuliwa wazi na sheria hii
(b) Sheria imetambua baadhi tu ya magari kamavile magari ya biashara ,magari yenye uzito mkubwa na yale yanayotumika kama usafiri kwa umma
(c) Sheria haijatambua aina (class) maalum ya barabara kwa ajili ya mwendokasi
JE, WADAU WANAPENDEKEZA NINI KUHUSU SHERIA YA USALAMA BARABARANI YA 1973
(a) Sheria inatakiwa kutambua maeneo yote na si yale ya mjini au maeneo ya makazi, sheria itamke wazi kuhusu maeneo ya shule
(b) kwa ajili ya kuzuia mwendokasi sheria izingatie aina zote za magari na si magari ya biashara, yenye uzito mkubwa na yale yatumikayo kwa usafiri wa umma pekee
(c) kwa ajili ya utekelezaji na utendaji; sheria iweke mawanda mapana ya kupunguza mwendokasi katika sheria kuu na sio kupitia kanuni zinazotungwa chini ya mamlaka ya waziri.
(d) Sheria itambue aina maalum ya barabara zilizotengwa kwa mwendokasi maalum (specific speed limit)
Upvote
0