dunstech
New Member
- Jun 14, 2020
- 2
- 19
Kama wewe ni mtumiaji wa Instagram na hukijui kitu kinaitwa "TWO FACTORS AUNTHETICATION"
basi ni vizuri ukasoma hapa.
Ni kitu ambacho kiko wazi kwamba Instagram ni moja ya mitandao ya kijamii ambayo inakuwa kwa kasi sana.
Ukuaji huu umepelekea wadukuzi wengi kuweka nguvu zao huko kushambulia account za watumiaji wa huo mtandao.
Zipo sababu nyingi za wadukuzi kushambulia account za watumiaji, moja ya sababu ni kuichukua account ya mtumiaji na kuibadilisha kama sehemu ya biashara zao, wakati mwingine hata kuziuza hizi account kwa watu wengine.
Na watumiaji wengi wamekuwa wanadukuliwa kwa sababu hawana uelewa mkubwa juu ya ulinzi wa mtandao.
Mfano, wengi wamekuwa wanaweka passwords(nenosiri) rahisi sana, passwords zenye majina yao, majina ya wazazi, mwaka wa kuzaliwa na vitu vinavyoendana na hivyo. Ni hatari sana kutumia password za aina hii kwa sababu zinatoa maelezo ya kutosha kuhusu wewe na ni rahisi kutabirika.
Lakini Instagram wana sehemu ya ulinzi ndani ya application yao ambayo inaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kuzuia wadukuzi
kuchukua account yako hata kama mdukuzi akafanikiwa kuipata password yako. Hii sehemu ya ulinzi inaitwa "Two-factors authentications".
Hii two-factors authentication ipo katika mitandao mingine pia kama vile facebook, lakini hapa nitailezea ya Instagram.
Kama two-factors authentication iko ON, instagram itazuia account yako kutumika kama mtu ataingia kwa kutumia kifaa kipya (simu, computer, tablet ambayo haijawahi kutumia account yako). Mtu akiingiza nenosiri (password) ili aingie kwenye account yako kwa kutumia kifaa kipya, instagram watakutumia code kwa kutumia SMS ambayo itatakiwa ijazwe tena ili afanikiwe kuingia.
Kwa sababu wadukuzi hawana simu yako na hawawezi kupata SMS zako, basi itakuokoa. Na wamechagua njia hii ya kukutumia code kwa kutumia number yako kwa sababu wakati mwingine mdukuzi anadukuwa mpaka email yako.
Kuwezesha "two factors aunthentication" kwenye account yako ya instagram basi unatakiwa kufanya hivi.
1. Ingia sehemu ya setting ya instagram kisha chagua sehemu waliyoandika "Security".
2. Kwenye security utachagua sehemu waliyoandika "Two-factors Authentication
3. Ukifungua hiyo sehemu ubonyeza sehemu palipoandikwa "Get started"
4. Utafuata maelekezo baada ya hapo ambayo utatumiwa message kwenye number yako
yenye code ambazo unatakiwa kuziingiza.
KUMBUKA:
Kama kwenye account yako haukujaza namba ya simu na ikathibitishwa(confirmed) , utahitajika kuingiza number kwanza ili kutumia
Two-factors authentications.
Ahsante.