Ifahamu USSR (Urusi) iliyokuwa dola-himaya na miliki kuu ya saba ya dunia

Ifahamu USSR (Urusi) iliyokuwa dola-himaya na miliki kuu ya saba ya dunia

Mkuu Comred Mbwana Allyamtu,
Mbona umenakiri uzi wangu (Naomba kujua historia ya Urusi) na kuandika kama mali yako bila kuomba idhini yangu wala kufanya Acknowldegement yoyote??

mtembea kwa miguu , born again pagan , Kabaunyeri , Paw , jay-millions , Gide MK , semper saratoga , MALCOM LUMUMBA , pyramid , maalimu shewedy
Kazi za uandshi usipo kuwa na uekewa nazo zutakuoa shida kidogo kuwa na ufahamu mpana.

Katika uandshi kuna kitu kinaitwa "some written but not equal" neno Hili Lina maana pana kwa mwenye uelewa wa maandiko

Maana yangu nini hata waje watu 100 awawezi badilisha maneno ya maadiko Juu ya historia furani (mfano: historia ya Tanzania hata iandikwe na watu rukuki Bado wote wanafanana ila watapishana mapito na maneno).

Mimi nimeandika historia ya USSR katika kuandika nimepita mapito Mengi ili nikusanye andiko moja iliyokamilifu na nzuri
 
Wakuu kwa mapenzi yote mwenye story ya USSR atupie hapa nasi tupate kuisoma vyema.
Hasa ambae anayo iliyo chambuliwa vizuri kwa laugha yetu Adhim ya Kiswahili.

Mwanzo hadi mwisho wake.

Nawasilisha

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Nakupa shauri nenda Wikipedia ndo Wana information ambazo Nazi trust Huku kila mtu ana lake na elimu yake utapotezwa
 
Urusi ya kale

Mababu wa Urusi na Ukraine walikuwa sehemu ya nchi ya slavic iliyoitwa Kieven Russia. Ilianzishwa na Viking Oleg katika karne ya tisa.

Faith Hillis, Profesa wa historia ya Urusi kutoka Chuo Kikuu cha Chicago, anasema kwamba eneo la bahari ya baltic na bahari nyeusi, ilipo sasa Ukraine, iliishi jamii ndogo karibu miaka elfu iliyopita.

"jamii hizi ziliamua kuungana na kuunda nchi mpya chini ya uongozi wa wafanyabiashara wa Scandinavia wanaosafiri kutoka Scandinavia kwenda Byzantium kupitia mto Nipro. Nchi hii mpya iliitwa Kieven Uussia na mji mkuu wake ulikuwa unaitwa Kiev ambao ni mji mkuu wa Ukraine sasa. Watu hawa wa Slavic hawakuwa raia wa Ukraine wala Urusi. Pia ilijumuisha jamii zisizo za Kislavoni kama vile jamii za makabila, Mongolis, Waislamu na wayahudi."

Jamii tofauti za eneo hili ziliunganishwa na imani ya kidini ya orthodox, wakiunganishwa na himaya ya mashariki ya waroma. Wengi hapa walibadilika kuwa Wakristo wa orthodox, ingawa pia kulikuwa na jamii tofauti za rangi.

Katika karne ya 13, jamii ya Mongols walivamia Kieven Russia. Idadi kubwa ya watu wa 'Slavic' hapa iligawanywa katika sehemu tatu kubwa. Baadae mgawanyo huu ulizaa Urusi, Ukraine na Blarus ya sasa.

Katika karne ya 14, wakati Mongols inaanguka, kulikuwa na tishio jingine uvamizi wa Kiev. Poland ilikuwa inajiandaa kupanua mipaka yake na uongozi wake ulikuwa mikononi mwa wakoloni wa kirumi.

Faith Hillis anasema, "Poland na Lithuania waliungana mikono, na katika karne ya 16 walianza kuelekea eneo la kusini. Kiev ikawa chini ya utawala wa Poland-Lithuania.

Historia ya Urusi na Ukraine iliingia katika sura mpya katika karne ya 17. Jamii ya Kiev, chini ya Poland, na jamii ya warusi wakiongozwa na tsar (kama mfalme) wa kirusi wakaunda kitu kinaitwa muungano wa Kikristo wa Orthodox.

Faith Hillis anaelezea, "hii ilikuwa hatua kubwa ya mambo kuanza kugeuka ambapo majadiliano juu ya masuala ya utaifa yalianza na yanaendelea mpaka katika zama za sasa.

Katika karne ya 18, ulikuwa wakati Urusi ilipounda himaya ya warusi ikijumuisha sehemu ya mashariki ya Ukraine. Ikawa na utamaduni wake, utawala wake wa uhuru na viongozi wake.

Jina la Ukraine ya mashariki sasa ilikuwa Novorasia yaani Urusi mpya. Wakati huo huo, sehemu ya upande wa magharibi ilibaki kwanza kuwa chini ya Austria na kisha baadaye chini ya utawala wa nasaba wa himaya ya Austro-Hungarian.

Mvutano huu himaya barani Ulaya ulisababisha vita vya dunia mwaka 1914. Miaka minne baadaye, wakati vita vilipomalizika, hakuna aliyebaki salama, si Austro-hungary wala himaya ya Warusi iliyonusurika.

Muungano wa Soviet
Sarhi Ploughti, Profesa wa historia kutoka Chuo Kikuu cha Harvard na Mkurugenzi wa Taasisi ya utafiti wa wa-Ukraine, anasema kwamba machafuko yaliyoibuka baada ya vita vya kwanza vya dunia na mapinduzi ya urusi yalibadilisha ramani ya bara la Ulaya. Wa-Ukraine wakaunda kuunda nchi yao huru. Mwaka 1917 Ukraine ikawa Jamhuri ya ujamaa ya soviet. Lakini haikuchukua muda mrefu.

Mwaka 1921, mkataba wa 'riga' ulisainiwa ili kumaliza vita vya Poland-Soviet, ambapo baadhi ya maeneo ya Ukraine yakawa sehemu ya Poland, Czechslovakia na Romania, wakati baadhi ya Jamhuri za Ujamaa za Soviet zilikuja kwenye umoja wa Soviet ulioongozwa na Vladimir Lenin na Bolshevik.

Rais wa sasa wa Urusi Vladimir Putin analichukulia hilo lilikuwa kosa la kihistoria. Kwa mujibu wake, Jamhuri ya Soviet yaani Ukraine ya Mashariki, Donetsk na Luhansk zilikuwa sehemu ya Urusi.

"Mwaka 1939, Hitler (kiongozi wa Ujerumani aliivamia Poland, iliyokuwa na kundi kubwa la wachache wa wenye asili ya Ukraine. Raia wa Ukraine walishirikiana na wanjeshi wa nazi. Aliona Poland kama ya ya ukandamizaji na ujerumani kama mshirika. Harakati za kizalendo za raia wa Ukraine wakaweka ushirika na wanazi. Lakini ushirika huo haukudumu.

"Wakati Jeshi la Ujerumani lilipoingia Ukraine, wazalendo walitangaza uhuru wa Ukraine. Wakakamatwa na Ujerumani. Mwishoni mwa 1941, mashirika yote ya wazalendo wa kiukreni yalikuwa ya kupambana na nazi, na wakati wanazi walipohamia sehemu nyingine za ukraine, mamilioni ya ukraini walijiunga na vita hivyo."

Uhuru wa Ukraine
Disemba 1991, viongozi waaandamizi wa Urusi, Belarus na Ukraine walikutana huko Belarus. Pande zote tatu zilikubali kuondoka katika Umoja wa Sovieti. Zama za Soviet zikafika mwisho. Ukraine ilikuwa tayari kuwa taifa huru.

Margarita Bameseda, Profesa katika Chuo kikuu cha Seaton nchini Marekani, anasema Ukraine ikawa huru, lakini maisha hapa yalikuwa magumu kwa watu wa kawaida.

Margarita anaelezea, "wakati huo, ilisemwa kwamba siasa za Ukraine zinatoka Kiev lakini pesa zinatoka Donetsk. Hii ina maana kwamba Donetsk ilikuwa na mchango mkubwa katika uchumi wa nchi, waheshimiwa hapa walikuwa wameacha mambo ya siasa kabisa kwa kiev."

Mwaka 2004 Ukraine iliingia tena katika mzozo. Kulikuwa na mapigano kati ya Viktor Yanukovych inayoungwa mkono na Urusi na Viktor Yuschenko, anayeungwa mkono na nchi za magharibi, katika uchaguzi wa rais.

Yanukovych alitangazwa mshindi, lakini alishutumiwa kwa wizi wa kura na maandamano dhidi yake yalianza. Maandamano hayo yalijulikana kama mapinduzi ya machungwa. Rangi ya chungwa ilikuwa rangi ya kampeni ya uchaguzi wa Yuschenko.

Margarita anasema, "watu kwa mara nyingine tena walitaka uchaguzi ufanyike upya na Yuschenko akashinda na kuwa rais. Ilikuwa hatua kubwa ya mabadiliko makubwa ya kidemokrasia. Baada ya hapo uchumi wa Ukraine ukaanza kupaa.

Mwaka 2010, Viktor Yanukovych alipata uungwaji mkono kutoka sehemu za mashariki na kushinda uchaguzi. Hapa mapinduzi mengine Ukraine yalikuwa yanaanza.

Harakati za viunga vya Midan
Mambo yalizidi kuwa magumu mwaka 2013. Yanukovych alipaswa kuchagua kati ya Ulaya au Urusi. Kabla ya kuingia makubaliano na umoja wa ulaya, akasitisha uamuzi huo na kuishutumu Urusi kwa shinikizo lake la kutaka Ukraine isijiunge na Umoja wa Ulaya

Kwa upande wa magharibi mwa nchi hiyo, watu walihisi kwamba uamuzi wa Yanukovych ulikuwa umevunja ndoto zao za kuwa na maisha bora ya baadaye. Karibu watu 100 waliuawa katika maandamano katika uwanja wa Midan mjini Kiev. Yanukovych ikabidi akimbilie kujificha Urusi.

Rais wa Urusi Vladimir Putin akaingilia hali ya mambo Ukraine, akatangaza Crimea kuwa sehemu ya Urusi na kuanza kudhibiti maeneo ya Luhansk na Donetsk.

Tangu mwaka 2014, mgogoro katika maeneo ya mpaka wa Urusi na Ukraine haujawahi kwKabla ya Urusi, iliyokuwa ikiongeza idadi zaidi ya wanajeshi kwenye mpaka wake na Ukraine kwa miezi kadhaa, ikaivamia Ukraine mnamo 24 february 2022.
 
Back
Top Bottom