sembo
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 4,350
- 3,451
Mnamo 08.08.2016 katika uwanja wa Taifa, kutakua na pambano la kukata na shoka baina ya miamba miwili ya Soka barani Africa, ambayo ni Simba S.C dhidi ya Interclube toka nchini Angola.
Pambano hili litakua ni kilele cha kusherekea Simba Week [Simba Day 2016] pia ni ufunguzi wa Sherehe kubwa na za kihistoria za kuadhimisha Miaka 80 tangu Simba S.C ianzishwe.
Je hawa "Miamba" Interclube ni kina nani?
Interclube ni moja kati ya timu bora kabisa kwa sasa nchini Angola. Ilianzishwa 1976. Ina uwanjani wake inaotumia kwa ajili ya mechi zake za nyumbani.
Kocha Mkuu wa timu hii ni Zdravko Logarušić ambaye ana heshima kubwa sana nchini kwao Croatia na hii ni kutokana na aina ya soka analofundisha. Ikumbukwe huyu Kocha alishawahi kuifundisha Simba S.C.
Hawa jamaa ni Wakimataifa kweli [Achana na wale Wakimataifa "Uchwara"] maana katika michuano ya Kimataifa wana "kiti" chao huko.
Mfano;
1. Katika CAF Confederation Cup;
2006 – Group Stage
2008 – Group Stage
2011 – Semi-finals
2012 – Group Stage
2. Katika CAF Champions League
2008 – Third Round
2011 – Second Round
3. Katika CAF Cup Winners' Cup
1987 – First Round
2001 – Finnalist
08.08.2016 itakua ni siku maalumu kwa;
1. Wanasimba kuja kushuhudia silaha zetu mpya kama vile "Kiboko ya Mabeki Visiki" Blagnon, "Beki Kisiki" Method Mwanjala n.k ambao watatambulishwa kwa mara ya kwanza.
Pia kutakua na utambulishwaji wa jezi tutakazotumia msimu ujao.
2. "Matomaso" kuja kushuhudia, je hivi vipigo vizito vizito tunavyovitoa mfululizo mkoani Morogoro, ni kwa hizi timu za "mchangani" tu au hata kwa timu za "kimataifa" [achana na "wakimataifa'' uchwara]?
Karibuni wote.. Simba S.C, NGUVU MOJA.