ILAN RAMON
JF-Expert Member
- Sep 10, 2013
- 9,698
- 4,488
Umefika babati kweli wewe?Makao Makuu ya Mkoa ni maamuzi tuu ya Serikali maana hata Babati,Lindi,Bariadi nk ni Makao Makuu ya Mikoa lakini ni Vimji vidogo kushinda Kasulu.
Babati ni Bush tuu sema hapo Mjini ndio Kuna tulami mitaani twa kuzidiUmefika babati kweli wewe?
Uko sahihi,Mbu wanaogopa wanaumeMwanaume unaogopa mbu
Mkuu ngoja na declare interest sitetei babati kwa sababu ni kwetu lakin naamini babati imezidi kasulu kwa kila kitu na huduma zote kasoro ardhi yenye afya.. hata muhaya akamua kujenga mjengo babati hahahaha 😆 🤣 😂 maana palimvutiaBabati ni Bush tuu sema hapo Mjini ndio Kuna tulami mitaani twa kuzidi
Babati ni Bush tuu sema hapo Mjini ndio Kuna tulami mitaani twa kuzidi
Umenikumbusha NgalangeSijawahi kufika Kasulu. Ila nimeishi Ifakara na Wilaya za Kilombero, Mlimba, Malinyi, na Ulanga kwa miaka mingi! Hakika Ifakara imebakia kuwa ndiyo kitovu cha biashara kwa hayo maeneo yote.
Sema pana mbu pale mahali! Na joto kali miezi ya mwishoni mwa mwaka. Ila ukija kwenye chakula, samaki na mchele ni bwelele.
Hatari sana. Na hao ngalange siku zote huliwa wakiwa bado ni wa moto.Umenikumbusha Ngalange
Umeeleza vizuri lakini mimi kwa jinsi ulivo eleza mimi naona bado nikikaa kasulu napata pesa.Nenda Ifakara utengeneze pesa kupitia kilimo mkuu.
Nimekaa Miji yote miwili Kasulu mazingira ya utafutaji ni magumu labda uwe umeajiriwa lkn hustling za mtaani ni ngumu. Kama umesoma pale Kasulu ndio Makao ya UNHCR na kuna NGO za Kimataifa zaidi ya 50 kamji kaamejaaa LANDCRUISER za UNHCR na Mashirika washirika wa UNHCR. Kuna Udongo mwekunduuu na utelezi wa kutosha wakati wa Mvua.
Ifakara ni bondeni, mafuriko anytime tu, wakati wa mvua tope kama lote kitaa.
Vibarua vyaa mashambani wakati wa kilimo hata kiangazi kwa siku hukosi elfu 30.
Kazi kwako
Huwezi linganisha Kasulu na vijiji vinavyotegemea majaruba 😂😂😂👇👇Umeeleza vizuri lakini mimi kwa jinsi ulivo eleza mimi naona bado nikikaa kasulu napata pesa.
Ukakae chaka na hauna hela, wazungu wanakaa mahali popote kwa sbb wanakuja na pesa maana hata kilimo kama huna pesa hutokiwezaHizi ndio mentality zetu,Wageni hasa wazungu wanakuja wanajichimbia mapolini huko wanapiga pesa vilivyo sisi wazawa tumekomaa na mijini tunataka tuwe tunaona lami masaa yote, tunaamini pesa ipo mjini, Mapori tumewaachia wageni wajaipimia wenyewe
Kasulu huwezi ilinganisha na Babati. Kasulu ni mji mkubwa SANA wa kibiashara. Kwa Mkoa wa Kigoma KASULU ndo mji mkubwa na wenye biashara kubwa kuliko hata Ujiji KigomaMkuu ngoja na declare interest sitetei babati kwa sababu ni kwetu lakin naamini babati imezidi kasulu kwa kila kitu na huduma zote kasoro ardhi yenye afya.. hata muhaya akamua kujenga mjengo babati hahahaha 😆 🤣 😂 maana palimvutia
Ifakara kuna barabara ya lami pia kuna treni ya TAZARA.Pesa inapatikana kule ambako ni less competitive.
Ifakara ni kama unaenda kujitumbukiza shimoni harafu unaishia njia ya kuingia na kutoka ni Moja.
Mkuu kasulu ni mji mkubwa au ina watu wengi sababu waha wanazaa sana?? Binafsi sijawahi tembe lasulu nimeangalia kwenye ndege 2013 palikuwa pa hovyo sana?!!Kasulu huwezi ilinganisha na Babati. Kasulu ni mji mkubwa SANA wa kibiashara. Kwa Mkoa wa Kigoma KASULU ndo mji mkubwa na wenye biashara kubwa kuliko hata Ujiji Kigoma
KASULU mjini Waha wa kihesabu. Pale pana watu wa kila kabila. Wachanga wanamiliki maduka na Hotels Kwa kwenda mbele. Mji ukishakuwa na Wachanga usihofu kwenda kufanya maisha na biasharaMkuu kasulu ni mji mkubwa au ina watu wengi sababu waha wanazaa sana?? Binafsi sijawahi tembe lasulu nimeangalia kwenye ndege 2013 palikuwa pa hovyo sana?!!
Hahahhaha lakin mashaka yangu ni vile kigoma bado ni mkoa uko mkiani mkiani kiuchumiKASULU mjini Waha wa kihesabu. Pale pana watu wa kila kabila. Wachanga wanamiliki maduka na Hotels Kwa kwenda mbele. Mji ukishakuwa na Wachanga usihofu kwenda kufanya maisha na biashara
Uchumi wa Kasulu mkubwa sana. Ile Lami ya Nyakanazi-Kakonko-Kibondo-Kasulu-Kigoma imekamilika. lakini pia Lami ya Kasulu-Uvinza ipo tayari. Kipande kinachoendelea ni cha Uvinza-Magarasi Mpanda. Pia Lami ya Kasulu-Uvinza-Urambo-Tabora bila bado vipande tu. Kasulu pamefunguka. Pia pana miradi mikubwa sana ya Kilimo ipo kwenye pipelines (Washaurielekezi wapo site) ukiwemo mradi mkubwa wa ujenzi wa umwagiliaji bonde la mto Malagarasi na mradi wa umeme.Hahahhaha lakin mashaka yangu ni vile kigoma bado ni mkoa uko mkiani mkiani kiuchumi