Ifike mahala tumpe heshima yake uyu kiumbe,(Messi)

Mbona sifa hizo haziendi kwa mtu aliyekimbia na kijiji kutoka nyuma kwa kasi ya ajabu messi yy alimalizia tu mnakuja kumpa sifa messi,! acheni mahaba afadhali ungemsema mnyama Sanchez aliyemtoa machozi gadiola!
 
Kusema kweli Messi ni mchezaji bora kabisa duniani. Binafsi naona Messi ni bora sana kwa sababu.
>Ana ball controll na dribbling ability kubwa sana.
Anauwezo wa kukokota mpira muda mrefu na kupiga chenga kutoka mbali sana na kwa muda mrefu bila kuchoka wala mpira kumtoka mguuni. In general dunian hakuna mchezaji ambaye ni ngumu sana kumkaba km Messi. Hilo wengi wanalifahamu na jana amedhihirisha. Messi ana uwezo wa kuuchezea mpira anavyotaka na akaufanya chochote.
>Messi ana uwezo wa kubadilisha hali ya mchezo iwapo timu yake imezidiwa. Ana uwezo wa kufunga yeye mwenyewe iwapo timu yake imeelemewa pia ana uwezo wa kuichezesha timu. Hilo linawezekana kwa sababu Messi ana uwezo wa kucheza km kiungo mchezeshaji, mshambuliaji na kadhalika. HAHAHAAAA Messi ana uwezo wa kucheza namba zote pale mbele yaani namba 9, 10, 11 na 7.
>messi anacheza soka ambalo linafurahisha na kuburudisha sana kwa mtazamaji. Anafanya mambo ambayo ni full maajabu na mbwembwe kubwa. Messi ana natural talent so kila kitu kinafanywa ki autimatic.


Hata Pele ameshawah kusema " watu wengi wanadai mm ni mfalme wa soka, pia wanadai mm nina uwezo mkubwa. Ni kwel kabisa mm ni bora zaidi na hakuna mtu mwingine yeyote anayenifikia. Lakini nikimwangalia huyu messi anavyocheza mpira nimeamini ni ukwel anafanana na mm na pia ni ukweli tuna uwezo sawa"
 
Dk 180 na Juventus alikuwa anazurura tu...alafu achukue World cup kwanza
 
Ni vizuri tukapima mafanikio ya mchezaji ngazi ya club,timu ya taifa na makombe mbalimbali...mess ndiyo mchezaji mzuri saana ila akiwa Barcelona tu...teh teh
Hapo umesema kweli mkuu wisewriter. Ronaldo akiwa ameiwakilisha nchi yake kwenye Kombe la EUFA na nchi yake kuwa bingwa, akiwa pia mchezaji wa klabu ya RMA inayotetea kombe ili na uwezekeno ni mkubwa RMA kulichukua tena upo uku akiwa anasubiri kutawazwa bingwa wa Spain La Liga. Lakini Messi hajawai kuipatia nchi yake kombe lolote zaidi ya klabu yake ya Barca. Hii inampunguzia uzito na nadhani inamwuma sana moyoni akiona mpinzani wake anashinda makombe
 
Halafu sasa kwa hako ka mwili kake anaweza cheza hvyohivyo mpaka miaka 35 aisee...
 
Una uhakika
 
Pamoja na kwamba katiba inaruhusu uhuru wa maoni kwa kila mmoja, ni mlevi tu anaweza kutoa mawazo uliyoyatoa
 
mess ni mtu wa kutengenezewa kisha yeye anamalizia, hahangaiki kama ronaldo hiyo ndio tofauti yao ninayoiona
Mkuu! Kuna vitu vinaweza vikawa vinakuuwa taratibu bila wewe mwenyewe kujua.....moja wapo ni hili kumsemea uongo huyu jamaa khaaa!
 
Huyu kiumbe ni habari nyingine kiboko yao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…