Ifike mahala vijana wenzangu tukue na tujifunze kuvikubali vilivyo vyetu na tuvipende

Ifike mahala vijana wenzangu tukue na tujifunze kuvikubali vilivyo vyetu na tuvipende

Kalaga Baho Nongwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2020
Posts
9,953
Reaction score
23,150
Juzi nimesikitika mnoo. Koloz wameolewa lakini kiunaume, mnajidanganya wazee kuolewa kuolewa tu. Hongereni pia kuiwakilisha Afrika Mashariki ma kati na kwa hatua ile mliyofikia Kyle Moroko. Nina hakika hata hili la NbC hapa kwetu mtalisikia kwenye Bomba.

Leo nina machache sana ya kushea, Moja ni hili la vijana kuigiza. Kuna jamaa angu mmoja hivi Toka apate kibarua huko Mikocheni kawa mbogo, haelezeki na hataki ushauri. Na mara kadhaa amekuwa mtu ambaye anajua Kila kitu. Katika harakat zake amekuwa mtu mwenye kudai kuwa na machaguo mengi katika maisha na kuhitajika na makampuni mengi iwezekenavyo kutokana na uwingi wa akili zake.

Juzijuzi Kuna msanii mkubwa tu aliyewahi kutolewa na Ommy dimpoz alitaka kumuajiri kuwa sehem ya menejiment ya mziki wake. Hapohapo fomu ya kuomba kazi za sensa niliijaza mmi kimakosa lakini alidai alichaguliwa kwenda kwenye ile kazi ila alikataa tu.

Leo ndo katoa Boko kabisaaaa. Anadai kampuni inayofanya kazi na kampuni Yao inamtaka yeye. Yani wamvue Kule ili wamuajiri wao. Anadai wakitaka hivyo alipwe laki 7+ maana hapo alipo analipwa laki 4. Na kasahau kabisa boss wao hapo alipo sasa, alitaka kutuajiri sisi casual labour wao Kwa malipo ya laki 3 tu.. Tena laki 3 hii na midigrii yetu. Yeye form foo?. Na Kila mwezi tareh 20-29 lazima nimsaidie hela ya kula mana hela anayolipwa hatoboi mwez.

Sasa kijana mwenzangu unaigiza ili iweje? Unaniongopea mwanaume mwenzako nikupe makalio yangu au nifanyeje? Kama upon humu una shida sema mzee wanaoweza kukusaidia wapo.. kitu huna usijikweze kama unacho. Kijana be real! Usichokuwa nacho huna. Yangu ni hayo wakuu.

Cc. Extrovert , Antonnia Tate Mkuu DR HAYA LAND Mkulungai Santos06 Kilimbatz Kalpana cocastic
 
Back
Top Bottom