Ifike mahali serikali ya Tanzania na hasa TCRA iwaheshimu watanzania

Ifike mahali serikali ya Tanzania na hasa TCRA iwaheshimu watanzania

Serikali kwamba inamwogopa ndugu Polepole kiasi Cha kupelekea kuuzima mtandao wa YouTube nchi nzima???.... Jameniii!!!
Huenda anayo ongea ni ukweli.. Kama ujuavyo ukweli unauma hasa kwa mtu ambae hata kubadirika kutokana na huo ukweli
 
Wakuu habari za muda huu?

Naandika hapa nikiwa nimefura kupitiliza. Imetosha sasa, hii serikali inabidi ifike mahali iheshimu raia.
Haiwezekani watu wawe wanajizimia zimia tu mitandao wanapojisikia.

Watu tumejiajiri huko YouTube, na leo jioni hii nilikuwa na darasa (huwa natrain watu mbali mbali ambao wanalipia), sasa mtu anatokea mtu sijui kala maharage ya wapi anazima network kisa Humphrey Polepole. Na hii si mara ya kwanza. Si mblock hiyo URL specific. Kwanini mnablock YouTube nzima? Ina maana hii nchi mambo yatakuwa yanasimama kila Polepole akiongea?

Mliblock X(zamani Twitter) hivi hivi, tukakaa kimya maisha yakaendelea. Na msivyo na haya wala aibu, na nyie wenyewe mnapost huko? Sasa mnampostia nani wakati mmeblock? Mnapost ili wananchi wa nchi gani waone?

Jipangeni, censorship haiwezi kuwa way of life. Badilikeni na mjiheshimu, hasa nyinyi TCRA. Tafuteni njia sahihi ya kudili na Polepole. Mtu mmoja hawezi kusimamisha nchi nzima kwa sababu ya incompetence yenu. Tunalipa kodi TRA FFS. 😡

View attachment 3434248
Anatoa pole za nini wakati alimshinikiza kujiuzulu uspika kama sio kumng'ong'a?
Serikali inatakiwa kushitakiwa kusababisha hasara kwa wananchi wanaotegemea mitandao kujipatia kipato kwa kuzima kwa muda wa saa zaidi ya nne kinyume na sheria.
@TLS fikirieni hili serikali inawanyanyasa sana wananchi kwa kutumia mbinu mbovu za kivita zilizokinyume na haki za binadamu (coercive starvation)
 
Huenda anayo ongea ni ukweli.. Kama ujuavyo ukweli unauma hasa kwa mtu ambae hata kubadirika kutokana na huo ukweli
Kabisa... Yatakuwa na ukweli aisee... Huwezi kuzima mtandao nchi nzima kwa kuogopa anachoongea huyu jamaa
 
Back
Top Bottom