Ifike mahali tujiulize tatizo ni nini pale Azam

Agrey998

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2019
Posts
417
Reaction score
550
Pamoja na uwekezaji mkubwa unaofanywa kuanzia kwenye usajili,maslahi ya wachezaji na hata miundombinu lakini bado wawekezaji na mashabiki hawapati kile kitu wanachotarajia kutoka Kwa Timu Yao , Kwa uwekezaji unaofanywa licha ya idadi ndogo ya mashabiki ukilinganisha na wale wakubwa wawili pale kariakoo lakini azam ilibidi awe anashindania na kushinda mataji , mwaka huu pamoja na usajili wote alioufanya lakini bado hajapata matokeo katika michezo miwili.

Unakaa unaangalia uwezo wa mchezaji mmoja mmoja pale Azam unaona wapo vizuri , bila kusahau hata program Yao ya vijana imekuza na kulea vijana wengi kimpira mfano metacha mnata,idi kipwagile na wengine wengi Tu lakini bado matokeo Yao yanasumbua na hawashindi mataji ya maana . Je Tatizo ni nini ?

Ukiangalia sajili zao unasema eeh kwel hii ni timu lakini bado hawakupi kilicho Bora uwanjani.

Nadhan wameshindwa kusoma vema alichofanya mamelodi sundown pale bondeni Kwa kuweza kuchomoza na kushinda mataji mbele ya mahasimu wa kihistoria wa pale Soweto Kaizer chiefs na Orlando pirates .

Lakini wapo wanasema kuwa Azam kuuwa Ile project ya kina Shomari, nyoni Kwa kuruhusu wachezaji wake wengi kuondoka pengine ndo imewaathiri , ukiangalia Kwa jicho Pana utaona wachezaji wao wengi walioachwa wameenda kuwa chachu ya mafanikio ya Simba Kwa miaka minne mfululizo.

TUJIULIZE je Tatizo ni nini Kwa Timu yenye uwekezaji mkubwa vile inaboronga ??

Au je mpira kwao si pesa Tu kuna vingine ??
 
Ili Azamu aweze kufanikiwa anatakiwa aondoe wale viongozi wote pale aweke wapya ikiwezekana wanaotoka nje ila wale waliopo pale ni wazee wa 10% kiasi kwamba wachezaji wanakuja gundua wanachukua mshahala mdogo huku madalali wanachukua zaidi yao
 
Inaonekana hukupata bahati ya kupita shule japo za awali ukawa na bahati ya kujua kuandika tu.

Reasoning yako iko chini sana kiasi kwamba hata kichwa ulistahili kuwa nacho kama cha mende.

Azam kufungwa na polisi ili huo usimba na uyanga ufaidikeje?
Usimba ndio sumu. Refer msemaji wao alivyokuwa analalamika kuwa ikifika match na Yanga jinsi viongozi wa Simba wanavyowashinikiza wafanye wawezavyo kuwafunga Yanga.
 
Kwa hiyo wewe umejiona ndio umeandika madini yote yaliyopo kichwani mwako, Kwanza umemuelewa mleta mada hapo,kataja match ya leo? Halafu uache umbumbumbu,bashite wahedi wewe
 
Mpira wa nchi hii ni extension ya siasa. Hauko independent kama tunavyodhani. Swali la kujiuliza kwanini tuliua Taifa Cup!?

Taifa Cup ilileta ushinda wa kweli, na spirit ilikuwa juu sana. Na kama ingeendelea premier league ingepoteza kabisa mashiko... Na Hilo lingeleta ugumu kwenye namna ya kucontrol interests, ..too many variables.. maana anybody can be anything anything... Literally kusingekuwa na uwezo wa kulazimisha timu ya mkoa huu ishindwe for any interest(s).

Kwa namna ilivyo Sasa, ni kuwa tunachoangalia ni maigizo... Ya Simba na Yanga.. wangawiana miaka ya utawala na kwakuwa nchi nzima Haina options... Wote tuko makundi mawili tuu..they have control over that.. and can be manipulated for influence gains..

Mwaka huu Yanga Bingwa.. mark my words.
 
Mtoa mada, Azam nayo ni timu kama ilivyo kwa Polisi Tanzania. Aliyejiandaa vizuri, ndiye anaye stahili kuondoka na point 3 muhimu.

Kinachotakiwa ni kujipanga tu na kupambana uwanjani ili kupata ushindi. Ingawa hii timu ina viashiria vyote vya kufungamana kwa siri na ile timu ya yule Mhindi.
 
Ivi taifa cup inayo chezwa wiki tatu utafanisha na league kweli!!! Madhumuni ya taifa cup ni kuweka platform ya wachezaji wasiofahamika kutokea Ligi daraja lanne, wachezaji wa mashuleni na vyuoni walio itwa timu za mkoa kuonekana. Na kwa watendaji wampira waliopo Sasa ukiweka Taifa cup Ligi itaisha mwezi wa 12 Mwakani
 
Tatizo Azam ni endelevu bro sijataja Tu mechi ya leo
 
Ivi taifa cup inayo chezwa wiki tatu utafanisha na league kweli!!! Madhumuni ya taifa cup ni kuweka platform ya wachezaji wasiofahamika kutokea Ligi daraja lanne, wachezaji wa mashuleni na vyuoni walio itwa timu za mkoa kuonekana. Na kwa watendaji wampira waliopo Sasa ukiweka Taifa cup Ligi itaisha mwezi wa 12 Mwakani
Kwahiyo unachotaka kusema tukiomba TFF kuanzishwe ligi ya timu za mikoa na iwe ya kudumu.. ichezwe kama B league unahakika watakubali!?

Hata hivyo kwanini haikuendelea ... Na kwanini waliokuwa wakishiriki ni wale wale wa ligi zilizopo!? Majina makubwa mengi yalikuwa yakishiriki...

Ile ligi watu walileta ushindani wa kweli kwenye michuano. Ushabiki ulioanzia ndani ya moyo.. watu walikuwa wanaumia kweli wakiona mikoa yao imeshindwa.. nani wa musoma anaumia kisa biashara imefungwa na yanga!? Au mgogo anayeumia kisa dodoma jiji wamefungua na Simba!?
 
Usimba ndio sumu. Refer msemaji wao alivyokuwa analalamika kuwa ikifika match na Yanga jinsi viongozi wa Simba wanavyowashinikiza wafanye wawezavyo kuwafunga Yanga.
Mtendaj wao was sasa so alikuwa katibu mkuu yanga au na wewe no wale aliowasema Eymael
 
Kwahiyo unachotaka kusema tukiomba TFF kuanzishwe ligi ya timu za mikoa na iwe ya kudumu.. ichezwe kama B league unahakika watakubali!?

Hata hivyo kwanini haikuendelea ... Na kwanini waliokuwa wakishiriki ni wale wale wa ligi zilizopo!? Majina makubwa mengi yalikuwa yakishiriki...

Ile ligi watu walileta ushindani wa kweli kwenye michuano. Ushabiki ulioanzia ndani ya moyo.. watu walikuwa wanaumia kweli wakiona mikoa yao imeshindwa.. nani wa musoma anaumia kisa biashara imefungwa na yanga!? Au mgogo anayeumia kisa dodoma jiji wamefungua na Simba!?
Mashabiki wengi wa Simba tuliishia kushabikia ilala....
( kulikuwa na wachezaji wengi wa simba).
Ilikufa nadhani tatizo ni wadhamini.
 
Tatizo La Azam ni Kumtumia Msukule Kuwa Balozi Wa Maji Uhai ilhali Zaka Zakazi Yupo....! Afu Tena Utopolo Wanatangaza Maji Ya Afya ..Msukule Yeye Kwa Kukosa Weledi Kang'ang'ania Maji Uhai....Lazima Timu Ifungwe! Zaka Roho inamuuma ndo Mana Simsikii Mwaka huu AKISEMA tuna Jambo Letu..!
 
Back
Top Bottom