Agrey998
JF-Expert Member
- Jul 8, 2019
- 417
- 550
Pamoja na uwekezaji mkubwa unaofanywa kuanzia kwenye usajili,maslahi ya wachezaji na hata miundombinu lakini bado wawekezaji na mashabiki hawapati kile kitu wanachotarajia kutoka Kwa Timu Yao , Kwa uwekezaji unaofanywa licha ya idadi ndogo ya mashabiki ukilinganisha na wale wakubwa wawili pale kariakoo lakini azam ilibidi awe anashindania na kushinda mataji , mwaka huu pamoja na usajili wote alioufanya lakini bado hajapata matokeo katika michezo miwili.
Unakaa unaangalia uwezo wa mchezaji mmoja mmoja pale Azam unaona wapo vizuri , bila kusahau hata program Yao ya vijana imekuza na kulea vijana wengi kimpira mfano metacha mnata,idi kipwagile na wengine wengi Tu lakini bado matokeo Yao yanasumbua na hawashindi mataji ya maana . Je Tatizo ni nini ?
Ukiangalia sajili zao unasema eeh kwel hii ni timu lakini bado hawakupi kilicho Bora uwanjani.
Nadhan wameshindwa kusoma vema alichofanya mamelodi sundown pale bondeni Kwa kuweza kuchomoza na kushinda mataji mbele ya mahasimu wa kihistoria wa pale Soweto Kaizer chiefs na Orlando pirates .
Lakini wapo wanasema kuwa Azam kuuwa Ile project ya kina Shomari, nyoni Kwa kuruhusu wachezaji wake wengi kuondoka pengine ndo imewaathiri , ukiangalia Kwa jicho Pana utaona wachezaji wao wengi walioachwa wameenda kuwa chachu ya mafanikio ya Simba Kwa miaka minne mfululizo.
TUJIULIZE je Tatizo ni nini Kwa Timu yenye uwekezaji mkubwa vile inaboronga ??
Au je mpira kwao si pesa Tu kuna vingine ??