Ifike mahali Vodacom na Airtel waige mfumo wa Yas kwenye Merchant Account

Vien

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2020
Posts
8,508
Reaction score
15,276
Kuna wakati ushindani unatakiwa ukubali ukweli.

Sio kila kitu unachotengeneza lazima kiwe tofauti. Kuna muda unatakiwa ujifunze kutoka kwa aliyefanya vizuri zaidi.

Nimekuwa nikitumia Merchant Account za Yas, Vodacom na Airtel kwa biashara zangu, na kwa uzoefu wangu, upande wa Merchant Account, Yas wamewapita mbali sana hawa wawili.

Kitu cha kwanza walichofanya vizuri ni usajili.

Una line yako ya kawaida ya Yas? Basi hiyo hiyo unaweza kuitumia kufungua Merchant Account kupitia Mixx by Yas. Hakuna usumbufu wa kuambiwa utafute line nyingine, hakuna kuanza upya mchakato wa usajili.

Dakika chache unakuwa tayari unaanza kupokea malipo.

Lakini ukifika Vodacom...

Hapo ndipo utakapojua maana ya neno complicated.

Hatua ni nyingi, mfumo hauko rafiki, na mara nyingi unajikuta unazungushwa mpaka unaanza kujiuliza kama kweli wanataka watu watumie Merchant Account zao au la.

Badala ya kufanya mambo yawe rahisi, wameyafanya yaonekane kama unafungua akaunti benki.

Kwa Airtel nako hali sio tofauti sana.

Airtel Merchant App imekuwa ikinisumbua mara kadhaa. Kuna nyakati ina shida za kuingia, nyakati nyingine ku-link Merchant Account si jambo la moja kwa moja, na matumizi yake hayatoi ule urahisi ambao mfanyabiashara anautegemea.

Sasa swali la kujiuliza ni hili...

Yas wameweza kufanya mfumo uwe mwepesi, rahisi na unaoeleweka.

Kwa nini Vodacom na Airtel washindwe?

Kitu kingine nilichokipenda kwa Mixx by Yas ni namna walivyogawa akaunti.

Ndani ya app moja una Personal Account yako na Merchant Account yako. Kubadilisha kutoka upande mmoja kwenda mwingine ni sekunde chache tu.

Hakuna kuchanganyikiwa.

Hakuna kuingia kwenye app nyingine.

Hakuna usumbufu wa kutafuta menu zisizoeleweka.

Huo ndiyo urahisi ambao wafanyabiashara wanauhitaji.

Kwa Vodacom wana Voda Business App, Airtel wana Airtel Merchant App.

Lakini ukiwa mtumiaji wa kawaida, mara nyingi utahisi kama app zimetengenezwa na watu wanaozijua wao wenyewe, si kwa kuzingatia uzoefu wa mteja anayezitumia kila siku.

Teknolojia bora sio ile yenye menu nyingi.

Teknolojia bora ni ile inayokufanya ufanye kazi nyingi kwa hatua chache.

Kama Yas wameonyesha inawezekana, kwa nini Vodacom na Airtel wasifanye hivyo pia?

Mwisho wa siku sisi wafanyabiashara hatutaki app yenye rangi nzuri au nembo nzuri.

Tunataka mfumo unaofanya biashara iwe rahisi.

Hayo ni maoni yangu kutokana na matumizi ya huduma zote tatu.

Je, wewe una uzoefu gani na Merchant Account za Yas, Vodacom au Airtel?
 
Uchambuzi mzuri sana , vipi kwenye upande wa makato wapi nafuu au hizo merchant account hazina makato ?
Upande wa makato hawajapishana sana, lakini yas pia amewapiga bao hapa coz unaweza ukatoa hela mara tatu kwa siku bila kukatwa, tofauti na hawa wengine, unatoa mara moja tuu kwa siku bila makato.
 
Voda walininyima Lipa kisa wananiambia nina acc ya uwakala ambayo mi mwenyewe hata siijui, nawaambia waifute bado kona zikawa nyingi!
Nilienda Yas acc iliwezeshwa hapo hapo!
 
Airtel unaweza kupata merchant account kwenye line yako hiyo hiyo ya airtel
 
Kuna wakati ushindani unatakiwa ukubali ukweli.

Sio kila kitu unachotengeneza lazima kiwe tofauti. Kuna muda unatakiwa ujifunze kutoka kwa aliyefanya vizuri zaidi.

Nimekuwa nikitumia Merchant Account za Yas, Vodacom na Airtel kwa biashara zangu, na kwa uzoefu wangu, upande wa Merchant Account, Yas wamewapita mbali sana hawa wawili.

Kitu cha kwanza walichofanya vizuri ni usajili.

Una line yako ya kawaida ya Yas? Basi hiyo hiyo unaweza kuitumia kufungua Merchant Account kupitia Mixx by Yas. Hakuna usumbufu wa kuambiwa utafute line nyingine, hakuna kuanza upya mchakato wa usajili.

Dakika chache unakuwa tayari unaanza kupokea malipo.

Lakini ukifika Vodacom...

Hapo ndipo utakapojua maana ya neno complicated.

Hatua ni nyingi, mfumo hauko rafiki, na mara nyingi unajikuta unazungushwa mpaka unaanza kujiuliza kama kweli wanataka watu watumie Merchant Account zao au la.

Badala ya kufanya mambo yawe rahisi, wameyafanya yaonekane kama unafungua akaunti benki.

Kwa Airtel nako hali sio tofauti sana.

Airtel Merchant App imekuwa ikinisumbua mara kadhaa. Kuna nyakati ina shida za kuingia, nyakati nyingine ku-link Merchant Account si jambo la moja kwa moja, na matumizi yake hayatoi ule urahisi ambao mfanyabiashara anautegemea.

Sasa swali la kujiuliza ni hili...

Yas wameweza kufanya mfumo uwe mwepesi, rahisi na unaoeleweka.

Kwa nini Vodacom na Airtel washindwe?

Kitu kingine nilichokipenda kwa Mixx by Yas ni namna walivyogawa akaunti.

Ndani ya app moja una Personal Account yako na Merchant Account yako. Kubadilisha kutoka upande mmoja kwenda mwingine ni sekunde chache tu.

Hakuna kuchanganyikiwa.

Hakuna kuingia kwenye app nyingine.

Hakuna usumbufu wa kutafuta menu zisizoeleweka.

Huo ndiyo urahisi ambao wafanyabiashara wanauhitaji.

Kwa Vodacom wana Voda Business App, Airtel wana Airtel Merchant App.

Lakini ukiwa mtumiaji wa kawaida, mara nyingi utahisi kama app zimetengenezwa na watu wanaozijua wao wenyewe, si kwa kuzingatia uzoefu wa mteja anayezitumia kila siku.

Teknolojia bora sio ile yenye menu nyingi.

Teknolojia bora ni ile inayokufanya ufanye kazi nyingi kwa hatua chache.

Kama Yas wameonyesha inawezekana, kwa nini Vodacom na Airtel wasifanye hivyo pia?

Mwisho wa siku sisi wafanyabiashara hatutaki app yenye rangi nzuri au nembo nzuri.

Tunataka mfumo unaofanya biashara iwe rahisi.

Hayo ni maoni yangu kutokana na matumizi ya huduma zote tatu.

Je, wewe una uzoefu gani na Merchant Account za Yas, Vodacom au Airtel?
MIMI NINAWAKUBALI HALOTEL UNATUMA PESA MTANDAO WOWOTE (STRAIGHT) BILA KUFANYA CHAGUO.
 
Back
Top Bottom