#COVID19 Ifike muda Mwenge wa Uhuru uhifadhiwe Makumbusho ili kupambana na COVID-19

#COVID19 Ifike muda Mwenge wa Uhuru uhifadhiwe Makumbusho ili kupambana na COVID-19

Kashishi yetu

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2014
Posts
3,509
Reaction score
3,741
Leo ulikuwa maeneo ya Chalinze.

Tumesimama tangu asubuhi hadi muda huu gari haziendi kisa Mwenge!

Wanafunzi wamekatishwa masomo yao wapo wamejipanga mistari hapo kushuhudia Mwenge!

Tunaanzaje kupona na hii Corona?

Wagonjwa wangapi wameathirika kutokana na kucheleweshwa na misafara ya Mwenge?

Uchumi kiasi gani umeathirika kutokana na watu kucheleweshwa na msafara wa Mwenge?

MAONI YANGU

SASA TUSEME IMETOSHA . TUUHIFADHI MAKUMBUSHO.DUNIA YA LEO NI YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA.

AU LA KAMA BADO NI MUHIMU BASI, Namna ya utekelezaji wa hili zoezi lipitiwe upya ili lisiathiri shughuli za wananchi wengine wasio na hatia yoyote.

LAKINI LA PILI ,NAOMBA MNIPE DARASA DOGO HAPA NAAMINI MPO WAHUSIKA WA MWENGE.

Kuhusu ule ulinzi wa Mwenge,!! Kinacholindwa ni huo Mwenge au ni kipi kinacholindwa hapo hadi kusababisha magari yapaki pembeni?

Kama nitakuwa nimekosea mahali basi mnikosoe kisha mnirekebishe .

TUEPUKE MIKUSANYIKO ISIYO YA LAZIMA.CORONA INATISHA.AHSANTENI
 
Uchawi wa ccm upo kwenye mwenge rejea maakubaliano yao na shetani mapangoni,ccm inatakiwa ipigwe kiroho kwanza
 
Bora hata katiba wanaweza kukusikiliza walau wakaja na rasimu Kisha wakapotezea lakini suala la mwenge sijui hata Kama utaeleweka

Uchawi wote ndo uko pale yaani achana na habari ya mwenge .
 
Si afiki mwenge ukae makumbusho,waupeleke jalalani kabisa,usahaulike!
 
Weee jamaaa. Ndg zangu wanakesha mwengeni Leo ni siku ya 7 wakiusubiri
 
Back
Top Bottom