Ifike wakati viongozi wa mpira wawajibike kwa kauli na matamshi yao

This is...

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2014
Posts
5,050
Reaction score
5,204
Kama kichwa cha habari kinavyosomeka hapo juu, katika mpira wetu wa kitanzania kumekuwa na utamaduni usio mzuri wa viongozi wa vilabu vyetu kutoa matamshi ya tuhuma kwa viongozi wa klabu fulani lakini Cha kushangaza matamshi hayo pamoja na athari zake lkn hakuna hatua zozote zinazochukuliwa ili kuwataka wahusika kuthibitisha kauli zao.

Ikumbukwe kuwa Kuna tofauti ya kuwa kiongozi wa mpira au taasisi ya mpira na mashabiki wa kawaida mtaani Kiongozi wa timu hapaswi kuongea km vile tu yuko kijiweni tena mbele ya kamera. Kiongozi anatakiwa kuonyesha weledi wa kiuongozi, Ni tofauti na shabiki wa kawaida.

Tumesikia mara nyingi na siku za karibuni kiongozi wa klabu kusema Kuna mipango ya kumhonga refa, au kuhujumu mechi , hasa mechi za watani wa jadi Simba na Yanga. Tuhuma km hizi ni nzito na hazipaswi kupita hivi hivi tu. Si afya kwa soka letu. Hii inaleta hisia ndani na nje ya Tz kwamba mpira wetu ni wa ujanja ujanja kitu ambacho si kizuri.

Kwanini mamlaka zinazohusika km Tff na bodi ya ligi, Takukuru wasishughulike na Hawa viongozi. Ili kiongozi anapoongea awe anaongea km kiongozi, ana inakuwa Ni Taarifa ya klabu na si mtu kukurupuka kwa hisia zake tu na kuropoka kutoa tuhuma.

Wakati mwingine Hawa wasemaji wa klabu zetu hasa Simba na Yanga wamefanya ofisi zao km vijiwe vya soga, na baada ya soga mtu anatoka hapo anaitisha press na kuropoka tu atakavyo,akatoa tuhuma ,huo siyo mpira.

Mfano siku zanza karibun nmemsikia afisa habari mmoja wa klabu kongwe kabisa akidai Kuna mpango wa kuhonga refa wa mechi ya dabi ya mwezi Dec 2021,lkn Cha kushangaza hata refa mwenyewe wa mechi hata hajatajwa na Tff bado.Sasa hii ni kumweka refa atakayeteuliwa KTK tension kwa sababu anakuwa tayari ameshasetiwa kisaikolojia,na mwisho wa siku anaweza asifanye maamuzi yenye busara kwa kuzingatia sheria 17 za mpira.

Je Ni kweli kwamba yote wanayoongea wasemaji yanakuwa yameelekezwa na klabu husika? Kwamba Mkiti, katibu, CEO wanakuwa wanajua exactly dondoo zote za press husika?

Ikumbukwe kwamba Simba na Yanga ni kioo cha soka letu,wanapofanya mambo yasiyo ya kiuweledi yanaakisiwa km mwelekeo wa mpira wetu ulivyo.

Niishie hapa.

Nakaribisha maoni yenye kujenga. Nyongeza,mitazamo nk. Si mzaha na utoto, ushabiki.
 
Nahis kuna haja ya wasemaji wa timu kuwa na level flan ya elimu make naona wengi wanaropoka kwa sababu hawana taaluma ya mambo ya PR
 
K
 
Nahis kuna haja ya wasemaji wa timu kuwa na level flan ya elimu make naona wengi wanaropoka kwa sababu hawana taaluma ya mambo ya PR
Ukichunguza vizuri utagundua kwamba ktk mpira wetu kwa sasa huwezi kutofautisha kati ya Kiongozi na shabiki. Wanafanya.

Pili, Ni ktk mpira wetu wa miguu ambako mtu ambaye ana dhamana km kiingozi anaweza KUTUHUMU HADHARANI, na hakuna ufuatiliaji au hatua kuchukuliwa dhidi ya mhusika athibitishe kauli au matamshi yake.

RUSHWA Ni kosa!
 
Nahis kuna haja ya wasemaji wa timu kuwa na level flan ya elimu make naona wengi wanaropoka kwa sababu hawana taaluma ya mambo ya PR
Ukichunguza vizuri utagundua kwamba ktk mpira wetu kwa sasa huwezi kutofautisha kati ya Kiongozi na shabiki.

Pili, Ni ktk mpira wetu wa miguu ambako mtu ambaye ana dhamana km kiingozi anaweza KUTUHUMU HADHARANI, na hakuna ufuatiliaji au hatua kuchukuliwa dhidi ya mhusika athibitishe kauli au matamshi yake.

RUSHWA Ni kosa!
 
Nahis kuna haja ya wasemaji wa timu kuwa na level flan ya elimu make naona wengi wanaropoka kwa sababu hawana taaluma ya mambo ya PR
Uzushi na uongo haujali mtu mwenye elimu kubwa au ndogo.Hizo tabia huwa zipo kwenye "damu" kabisa.
 
Simba haina Afisa habari kwa sasa.
 
Tff na body ya league hamna kitu pale ndio Maana unaona wakina manara hata alipokuwa Simba na Sasa yanga Ni mtu anayejiona anaweza ongea lolote na asiguswe .
Kuna huyu wakuitwa Bumbuli sijui ilikuwaje Hadi yupo pale Maana naonaga Ni mtu mweupe Sana kufit kwenye Ile nafas ,muda wote Ni majungu ,kujihami na upuuz mwingine.
Mwijaku wa Simba aliyewaza kumpa nafas ya uhamasishaj nadhan achunguzwe akil yake ,yaan mnaacha watu wa mpira mnatuletea machawa ambao hawana break linapokuja swala la kuropoka Tena huyu Nina iman hajui idad ya wachezaj wawapo uwanjan Ni mweupe Sana kwenye Mambo ya mpira.
Mwakalebela hili ndio takataka kabisa kwenye ujinga linatangulizwa mbele ,kwenye Mambo ya Maana halionekani.

Wachambuz ,Hawa Sasa ndio wanaenda kuharibu mpira jumla ,Kwanza wamejaa mahaba ya timu zao ,kila mchambuzi Ana timu yake na kibaya Zaid hawajifichi kuonyesha mahaba, kuna kitenge na yanga yake pia Kuna jemedari na Simba yake ,yan Hawa Ni mfano tu.

Marefa ndio ushuzi kabisa ,imefika mahali watu wanajua yule Ni shabik wa timu fulan na kibaya Zaid bado anaendelea kupewa majukumu hayo hayo .Kuna penalty Ile ya yanga na namungo ilileta maswal mengi Sana ,Kuna kuibeba timu lakin sio kwa style Ile huku Ni kunajisi mpira wetu ,alafu et tutegemee kufika mbali kwa ushubwada Kama huu?
Sisi level yetu kimpira bado Sana ,na ukitaka kuona Hilo Ni pale tunapokutana na timu zinazotoka kwenye mataifa yanayojua Maana halis ya mpira Ni nn
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…