This is...
JF-Expert Member
- Dec 28, 2014
- 5,050
- 5,204
Kama kichwa cha habari kinavyosomeka hapo juu, katika mpira wetu wa kitanzania kumekuwa na utamaduni usio mzuri wa viongozi wa vilabu vyetu kutoa matamshi ya tuhuma kwa viongozi wa klabu fulani lakini Cha kushangaza matamshi hayo pamoja na athari zake lkn hakuna hatua zozote zinazochukuliwa ili kuwataka wahusika kuthibitisha kauli zao.
Ikumbukwe kuwa Kuna tofauti ya kuwa kiongozi wa mpira au taasisi ya mpira na mashabiki wa kawaida mtaani Kiongozi wa timu hapaswi kuongea km vile tu yuko kijiweni tena mbele ya kamera. Kiongozi anatakiwa kuonyesha weledi wa kiuongozi, Ni tofauti na shabiki wa kawaida.
Tumesikia mara nyingi na siku za karibuni kiongozi wa klabu kusema Kuna mipango ya kumhonga refa, au kuhujumu mechi , hasa mechi za watani wa jadi Simba na Yanga. Tuhuma km hizi ni nzito na hazipaswi kupita hivi hivi tu. Si afya kwa soka letu. Hii inaleta hisia ndani na nje ya Tz kwamba mpira wetu ni wa ujanja ujanja kitu ambacho si kizuri.
Kwanini mamlaka zinazohusika km Tff na bodi ya ligi, Takukuru wasishughulike na Hawa viongozi. Ili kiongozi anapoongea awe anaongea km kiongozi, ana inakuwa Ni Taarifa ya klabu na si mtu kukurupuka kwa hisia zake tu na kuropoka kutoa tuhuma.
Wakati mwingine Hawa wasemaji wa klabu zetu hasa Simba na Yanga wamefanya ofisi zao km vijiwe vya soga, na baada ya soga mtu anatoka hapo anaitisha press na kuropoka tu atakavyo,akatoa tuhuma ,huo siyo mpira.
Mfano siku zanza karibun nmemsikia afisa habari mmoja wa klabu kongwe kabisa akidai Kuna mpango wa kuhonga refa wa mechi ya dabi ya mwezi Dec 2021,lkn Cha kushangaza hata refa mwenyewe wa mechi hata hajatajwa na Tff bado.Sasa hii ni kumweka refa atakayeteuliwa KTK tension kwa sababu anakuwa tayari ameshasetiwa kisaikolojia,na mwisho wa siku anaweza asifanye maamuzi yenye busara kwa kuzingatia sheria 17 za mpira.
Je Ni kweli kwamba yote wanayoongea wasemaji yanakuwa yameelekezwa na klabu husika? Kwamba Mkiti, katibu, CEO wanakuwa wanajua exactly dondoo zote za press husika?
Ikumbukwe kwamba Simba na Yanga ni kioo cha soka letu,wanapofanya mambo yasiyo ya kiuweledi yanaakisiwa km mwelekeo wa mpira wetu ulivyo.
Niishie hapa.
Nakaribisha maoni yenye kujenga. Nyongeza,mitazamo nk. Si mzaha na utoto, ushabiki.