Huu mjadala wa chuo gani kizuri na kipi kibaya unachekesha sana. Binafsi nimesoma Tumaini na nilianza kazi pamoja na vijana wenzangu wengi tu kutoka hivyo bora vilivyotajwa hapo ju na mmoja wetu (UDSM, Mzumbe). Sina undgu na bosi yetote pale ila kwakujituma, hivi sasa mimi ni bosi wa wale vijana wenzangu tulioanza kazi pamoja. Je, niidharau degree yangu kwasababu inatoka Tumaini? Hivi, nikipata First Class ya Tumaini au IFM au SAUTI nitakuwa sawa na aliyepata Gentleman ya UDSM/Mzumbe/etc? Hivi sasa ninapokea wanafunzi wengi kutoka vyuo hivyo Havard za Tanzania na wengine kutoka vile ambavyo wenzetu mliobarikiwa mnaviita Vya Kata na kusema kweli wapo wanaonielewa haraka na wapo wasioelewa kabisa japo wanatoka vyuo vyote. Je, mchango wa chuo alichosoma mtu hapa ni upi katika utendaji kazi wake? Je, tumefikia kiwango cha kuwahukumu watu kwa vyuo walivyopitia? Hatuoni kuwa tunawakatisha tamaa wale wanaowekeza katika elimu? Binafsi ninaamini kuwa UDSM kumejaa walimu wengi sana na wenye good qualifications ila wengi wao wamekuwa wanasiasa. Kwa ujumla, walimu wengi, haswa ktk vyuo vyenye majina kama UDSM, siku hizi hawafundishi kutokana na kukata tamaa na ugumu wa maisha. Wanachangamkia zaidi projects za research. Tusidanganyane, hakuna chuo ambacho ni kizuri katika kila fani na hakuna chuo ambacho ni kibovu katika fani zote. Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni. IFM ni chuo kizuri kwa wanafunzi wanaokwenda kusoma na kibovu kwa wanafunzi wanaokenda kutalii. A bad writer always blames his/her pen!