IFM the best place to be...Wale mliochaguliwa IFM someni hapa.

Zeddicus

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2012
Posts
627
Reaction score
535
Hongereni sana kwa kuchaguliwa chuo cha usimamizi wa fedha, chuo hiki kipo katikati kabisa ya jiji la Dar es salaam, kipo mkabala na Jumba la makumbusho ya taifa.

Taaluma.

Chuo kwa asilimia kubwa kinajitahidi kutoa elimu bora kuwaandaa wanafunzi kuhudumia jamii inayowazunguka katika science related fields (computer science & IT) na Finance related fields ( Banking, Accounting, Insurance e.t.c), facilities za kujifunzia zipo za kutosha kama lecture theatres, lecturers, tutors, library, computer labs na lecturers Handouts, ushindwe wewe tu. Hapa wanafunzi wengi hujisahau katika masomo yao kwasababu ya starehe nyingi because chuo kipo karibu na kumbi maarufu za starehe kama Savanah, club Billicanas, Samaki Samaki Posta na zinginezo, hivyo wanafunzi hujikuta karibu siku zote za week wanahudhuria kustareheka na kwa hili hujisahau katika taaluma na kupelekea kufeli mitihani yao.

Accomodations.

Chuo kina Hostel hapo hapo campus ila hazitoshelezi kuwachukua wanafunzi wote hivyo wadau mbalimbali wamejenga hostel nyingi tu eneo la Kigamboni, hivyo ikitokea umekosa Hostel Campus Kigamboni pia panakuhusu, yapo maeneo mengine ambako unaweza kupanga chumba kama magomeni na Kinondoni ila shida ya huko ni usafiri kama mnavyojua hali ya usafiri jijini, Ila kigamboni ndio mpango mzima kwani huko haina haja ya kupanda gari ni Tsh.400 tu sa kivuko kwenda na kurudi.

Meals.

Chakula kinapatikana katika canteen iliyopo chuoni kuanzia bei ya Tsh.800, pia kuna maeneo mengine nje ya chuo waweza kupata chakula kwa bei ya Tsh.1500 na kuendelea..kwa wale wenye nazo mnaweza kula katika migahawa standard ambapo chakula ni Tsh.5000 na kuendelea kama Steers, na mingineyo iliyopo Posta.

Wale wa Kigamboni huku mambo super tu kama umepanga geto unaweza kuwa unajipikia kuepuka gharama, pia vyakula vya kununua,sio gharama.

PRECAUTION.

IFM kuna wasichana wazuri sana mapaja nje nje hivyo ni wewe tu kuwa makini kwani mitandao ya ngono ni deep sana...lecturers wanajisevia, mapedeshee wa town ndio sehemu yao pale. Hivyo ni vema ukaenda kutafuta kilichokupeleka kwani utaratibu wa taaluma umebana sana IFM usipokuwa makini utadisco semister ya kwanza tu.

All in all karibuni sana chuoni IFM Shaban Robert Road, karibuni sana tuvuke maji kuelekea Kigamboni.

For more clarification do not hesitate to PM me.....
 
Haya nawatakia masomo mema kwenye TAASISI YA USIMAMIZI WA FEDHA
 
ahaaha hao mapaja nje nje ni hao hao first year...wanakuja na ushamba wa kuvaa...second yr na 3rd year tushavurugwa xo mapaja yetu imebidi tuyazibe...
 
je kuhusu kule kigamboni wanachuo wanavamiwa usiku na kuibiwa vitu vyao kama laptops na simu,pia suala la wanaume kuingiliwa kinyume na maumbile yao mbona hujaliongelea ili first year students wawe care na hostel za kigamboni,afu umesema inatoa wataalamu wazuri,je vyuo vingine haviwezi kutoa wataalamu waliobobea masuala ya fedha???? be care kwa kupost new topic kabla ya kufikiria,je UDSM wasemaje kama nyie mnasema chuo bora?????
 

Hiyo ni changamoto tu brother hata UDSM pia wavamizi wapo rejea tukio lilifanyika hivi Karibuni la mwanachuo kupigwa risasi na majambazi yaliyovamia hostel.

Sijaponda vyuo vingine hapa, tatizo kila mtu humu ndani akileta thread inayohusu chuo basi mnataka kuanzisha league..me nazungumzia IFM na wanafunzi waliochaguliwa pale so kama unataka kuanzisha league ya vyuo tafuta thread inayohusu hizo league na si hii.

Nafikiri tumeelewana mkuu PIECE:thumbup:
 

mbona hujawaambia mambo ya sup mkuu na kuandishana floor ya 5 na 6 bila sababu yoyote zaidi ya kuzodoana..
 
Xaxa mkuu,hebu tutaftie taarifa ya kuwa tunaanza lini kuripot hapo chuo
 
"lecturers wanajisevia.." hii kitu ni very serious! how extent is this issue??
 
Asantee mkuu.....huyo METAL ni kilaza nimeshamzoea ubishi wake wa kijinga... mpigamsuli karibu sana kwenye taasisi yetu
 
Last edited by a moderator:

shukrani sana kaka kwa hili!! Hostel application tunaanza lini?
 
afu ww mbrazil achana na mm eti unasema umenizoea,umezioaje ww kjana wa kizazi cha mulugo,mnaleta ishu zenu za kishamba unadhan uko facebook au twitter,mm najaribu kuwaelezea madogo wa first year kuwa kigamboni ni sehemu hatari sana kwa usalama wa wanachuo na mali zao,afu unaniita kilaza,poa ukikua utaacha utoto wako huo
 
Kigambon kwa sasa kumetulia sana sio kama mara ya kwanza...nakumbka hata mm first semister walinivamia rum wakachukua simu na laptop...ila baada ya watu chuo kuandamana mambo yakawa shwari..nowdayz kuna aman tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…