Igizo la Corona limeishia wapi?

Kivumishi Kielezi

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2019
Posts
1,028
Reaction score
2,451
Hii isidingo ya corona mbona kama vile imefika tamati bila wadau kupewa taarifa rasmi?

Zile mbwembwe za machanjo na mabarakoa zimeishia wapi?

Ati ooh watu watakufa kama kumbikumbi sijui nini! Kiko wapi?

Bado kitambo kidogo tutajua tu ukweli wa hii movie ya kihindi.

Siku hizi sioni tena mabarakoa yakivaliwa?
 
Hahahah




 

Acha maskhara, tumepoteza watu wengi kwa corona. Ndugu, jamaa na marafiki.
 
Sasa mtu afe kwa kisukari, afe kwa ugonjwa wa moyo, halafu mseme ni Corona?! Kwanini msimseme kafariki kwa kisukari? Au huyo mgonjwa haingizwi kwenye takwimu za kisukari? Au anaingizwa kwenye takwimu zote 2?
Sababu wanapima coroma unapokuwa na dalili tuu, hivyo baadae magonjwa mengine yanapoanza kukutafuna, wanakuwa wanajua chanzo. Ni kama ukimwi, gonjwa mmoja litakukamata mpaka unakufa
 
Kwa Tz ilikuwa vita tu na JPM,maana hata wale waliokuwa wanasema misongamano kwanini inaruhusiwa,saizi wale wanaharakati siwaoni tena......... JPM alikuwa na mapungufu yake ila pia nchi hii inawanafiki wengi sana na hawana hata aibu
 
Subiri kwanza tumalize vita ya Urusi ndo turudi kuupdate corona yetu toleo jipya[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…