Igoma - Kishiri - Buhongwa

Igoma - Kishiri - Buhongwa

Silly

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
569
Reaction score
180
Hapa kuna barabara ambalo kimsingi linahudumia watu wengi, na kwa wengi sana limekuwa ni msaada mkubwa kwa kuwawezesha watu kufika Buhongwa bila ya ulazima wa kupita mjini kati.

Siku za hivi karibuni linatumika sana hata na magari makubwa na ukweli ni kwamba litakuwa ni msaada mkubwa sana kuepusha msongamano usio wa lazima kuwezesha kuingilia Buhongwa hadi ukanda wa mashariki mwa mji - (Igoma au Nyamongolo).

Zimekuwepo tetesi za siku nyingi zinazohusu hili barabara na majuzi wakati wanafanya upimaji barabara limeonekana kuhitaji mita 50 na tayari vigingi vimewekwa kuonyesha mipaka.

Hapa pia watu wengi wamesogea kupisha ujenzi huu. Swali ni lini kazi itaanza huku na je route ya hili barabara ni ipi maana Sahwa ya Chini na Juu zote zinaonekana kuwa na mahitaji makubwa.

Je ni lini Serikali itatujali sisi watumiaji wa hili barabara na wengine wengi ambao ni wahitaji.
 
Sasa umeshasema wamepita na wameweka na vigingi, si usubiri? Subra huvuta kheri.
 
Kwani jf nzima ni wakazi wa igoma??

Em iweke kisomi mkuu, huenda kuna watu wanajua kinachojiri maeneo hayo ila wanapuuza kwasababu hujatoa taarifa za kutosha.
Na si ajabu igoma zipo nyingi Tz hii.

FAFANUA.
 
Vuta subra mkuu tayari tenda imeshatangazwa (hapa najua Nyanza Road tu ndio watakao shinda tenda) tangu mwezi uliopita ujenzi ni barabara ya lami toka Igoma (nahisi itaanzia Bango) hadi Buhongwa kupitia Kishiri pia kutoka Kishiri hadi Fumagila (lami nyepesi)
 
Kua mpole mkuu kazi itafanyika punde
 
Back
Top Bottom