IGP: Ajali ya Shabiby Tunduma trafic aliyewahi kupiga faini bus lolote la Shabiby kuanzia Sep 2024 hadi sasa awasiliane nami

IGP: Ajali ya Shabiby Tunduma trafic aliyewahi kupiga faini bus lolote la Shabiby kuanzia Sep 2024 hadi sasa awasiliane nami

Ni mbinu yake kuyumbisha mjadala, lengo tutumie muda mwingi kumuuliza ana maanisha nini tuache kuhoji tabia za hao madereva na boss wao kuhonga traffic
Mkuu shida si madereva. Shida ni mfanyabiashara na mbunge pia. Ao askari watamwajibishaje?. Nyerere alikataa haya mambo kuwa Kama wewe ni mfanya biashara Kaa pembeni fanya biashara yako kihalali lipa Kodi. Sasa mtu anafanya biashara alafu ana mamlaka pia. Askali wakipiga faini wanaonywa na wakati mwingine wanaamishwa mpaka vituo vya kazi
 
IGP: Ajali ya Shabiby Tunduma

- Ajali ya Shabiby: Inahusisha mabasi ya kampuni ya Shabiby ambayo yanatumika katika safari za Tunduma.

- Faini za Trafiki: Taarifa inasema kuwa hakuna madereva wa mabasi ya Shabiby ambao wamepiga faini kuanzia Septemba 2024.

- Wasiliana NAMI: Ni wito kwa watu ambao wanaweza kuwa na habari au ambao wamepata faini kuwasiliana na mtu anayetoa taarifa hii.

- Kukosekana kwa Heshima za Kisheria: Inasisitizwa kuwa mabasi haya yanaendeshwa bila uoga wa kufanyiwa ukaguzi au kupigwa faini, jambo ambalo linaweza kuashiria ukiukwaji wa sheria za barabarani

Muktadha

Inavyoonekana, kuna wasiwasi kuhusu usalama wa abiria na utii wa sheria za barabarani katika safari za mabasi haya.

Ni muhimu kwa mamlaka zinazohusika kuchunguza suala hili ili kuhakikisha usalama wa abiria na kulinda haki za watumiaji wa huduma za usafiri.

Ikiwa una maelezo zaidi au unahitaji msaada wa ziada, tafadhali nijulishe!
View attachment 3156621
Haya mambo ndiyo yananifanya nataka kuwa kiongozi yaani kuna watu wanajikuta miungu watu. Aisee
 
Hawa madereva wa mabasi hawana tofauti na magaidi na hawana tofauti na mmiliki wa gorofa la kariakoo.

Kuna wakati natoka mwanza kuja Dar nipo na abood tukanusurika na ajali kibaigwa nikaenda mbele kugombana na dereva basi likasimama ajabu abiria wote ndani ya basi walinyamaza kimya Kama mazombie na abiria mmoja akawa anamtetea dereva.
Kichekesho kingine dada niliekuwa nae Siti ya jirani hakunichangamkia Tena 😁 aliniona mkorofi .
 
Ktk bus nilikua napata amani kusafiri nalo ni haya mabus ya Shabiby..ila sasa ndo hivi tena
 
Back
Top Bottom