Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 17,047
- 63,206
Duh!Ndugu IGP, siku hizi kila ikifika jioni saa kumi na moja mpaka saa moja jioni kuna foleni ya kutisha njia hii. Watu wanakaa hata masaa mawili.kutoka Morocco kufika Mwenge.
Watu wanakushutumu wewe kuwa Msafara wako wa kutoka kazini, ni sababu mojawapo ya njia kufungwa, ili wewe upite. Hii ni ajabu kwamba mamilioni wanakaa masaa kibao kukusubiri mtu mmoja upite. Hiyo siyo sawa, siyo fair. Kwanza siyo spirit ya uaskari inayotaka iweke raia mbele kabla ya wao binafsi.
Tafadhali tuondolee adha hii maana hii imekuwa kero kubwa,
watu wanachelewa kufika majumbani mwao, foleni ni kubwa sana.
Nakushauri ikibidi utumie helcopter kurudi nyumbani kwako au uchelewe kurudi nyumbani ili wananchi wengi wapungue barabarani.
Uchumi unashuka kwa sababu ya foleni kubwa.
Nawasilisha
Hahaha nimecheka mpaka bhasi, na hii ni kweli kosa tu kuna kakikundi fulani kinaforce kiendelee kuabudiwa wakati zama zao na sera zao zimeshapitwa na wakati na wameshachokwa mpaka na watoto.Uholanzi nchi inayobeba uchumi wake yenyewe waziri mkuu anakwenda kazini kwa baiskeli, huku kwetu nchi inayotegemea misaada hata mgambo anafunga barabara. Kama sio ulofa ni nini?
Hahaha nimecheka mpaka bhasi, na hii ni kweli kosa tu kuna kakikundi fulani kinaforce kiendelee kuabudiwa wakati zama zao na sera zao zimeshapitwa na wakati na wameshachokwa mpaka na watoto.
Mimi ningeumbwa mzungu ningebagua mwafrika na ningekaa naye mita 1000000000. Kiumbe cha hovyo kupata kutokea.Muafrika muda kwake sio rasilimali. Ndio maana watu hawawezi lipwa kwa masaa Africa. Kuna muda mwingi sana unapotea kufanya mambo ya kijinga Afrika. 😊
Kwakweli ni upumbavu mkubwa sana. Na hili linasababishwa na wengi kugeuza siasa kama ndio njia kuu ya kuingiza kipato yaani ajira rasmi na bila wao familia zao haziwezi kusonga mbele ndiomana wanashiriko kwenye ufisadi mkubwa na wanaogopa wakitoka wengi watafirisiwa na kwenda jera. Ipo siku tuWaafrika tuna ile power trip, mtu akiwa kwenye nafasi flani basi anataka aabudiwe kama Messiah, pumbavu kabisa