SI KWELI IGP Camillus Wambura “Rais Samia ameshushwa kutoka mbinguni

SI KWELI IGP Camillus Wambura “Rais Samia ameshushwa kutoka mbinguni

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
NUKUU.jpeg
 
Tunachokijua
IGP Camillus Wambura Ndiye Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania (Inspector General of Police - IGP) tangu alipoteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan tarehe 19 Julai 2022. Yeye ni IGP wa 11 kuongoza jeshi hilo tangu nchi ipate uhuru, akichukua nafasi ya Simon Sirro.

Madai

Kumekuwepo Nukuu inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii, hususan Facebook, ikidaiwa kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Camillus Wambura, alisema kuwa “Rais Samia ameshushwa kutoka mbinguni.”

Nukuu hiyo inasambazwa ikidaiwa kuwa ilitolewa na IGP Wambura wakati wa hotuba au mazungumzo yake kuhusu Rais Samia Suluhu Hassan.

Uhalisia

Ufuatiliaji wa nukuu hiyo kwa kutumia maneno muhimu kwenye vyanzo mbalimbali vya habari haukupata ushahidi wa moja kwa moja unaothibitisha kuwa IGP Camillus Wambura amewahi kutoa kauli hiyo hadharani.

Aidha, hakuna ushahidi wa video, sauti ama hotuba kamili au taarifa rasmi iliyopatikana inayomuonyesha IGP Wambura akitamka maneno hayo au chanzo rasmi kutoa taarifa hiyo.

Pia, utafutaji haukubaini chombo cha habari kilichochapisha nukuu hiyo pamoja na maelezo ya tukio, tarehe au mahali ambapo kauli hiyo inadaiwa kutolewa

Licha ya hivyo ukurasa rasmi wa jeshi la polisi nchini Tanzania hakuana taarifa kwa ummma yenye nukuu ambayo inadaiwa kusambazwa kwenye mitndao ya kijamii.
Back
Top Bottom