"
MsemajiUkweli, post: 16008019, member: 91662"] Wewe unajenga hoja kwa kutumia msingi wa nadharia, Mimi ninajenga hoja kwa kutumia msingi wa uharisia.
Sidhani unatumia uhalisia, vinginevyo usingebabaika ukihamisha magoli kila asubuhi. Hujaeleza 'uhalisia' wa bunge kusema abcd, kamati zake efg, serikali hjk n.k.
utakumbuka ulisema 'hili suala lina utata sana, ndio uhalisia huo?
Ni nani unadhani anaficha ficha na kusita kulishughuliki, Kamati Ndogo ya Bunge inalishughurikia
Alaa, si ulisema ni la kamati ya ulinzi na usalama na mambo ya nje?
Hiyo ni baada ya kusema serikali inalishughulikia!
kama isingekuwa PAC,hisia zako zisingewepo,usingefahamu kuna mkataba unaohitaji clarification kutoka polisi.
PAC
.Kwakweli sikujua kama kuna mauza uza hayo, nadhani Watanzania wengi hawakaaujua ikiwemo PAC na PCCB. Wangalijua uchunguzi usingehitajika.
Kutojua ni sababu ya kutouliza? Niliwahi kusema katika uzi niliokupa, Tatizo la Watanzania ni watu wa kumeza, kuhoji ni 'uhalifu' na kukosa uzalendo kama CCM wanavyosema.
Kwamba, kukaa kimya ndio uzalendo uliotukuka, tena wakishangilia hata makosa!
Tuache Kamati Ndogo ya Bunge ifanye kazi zake labda kama hatuiamini
Ulisema tuache kamati ya ulinzi na usalama ifanye kazi zake
Sasa kama huelewi mwenye dhamana , kwa nini unasema kuna kuficha ficha.
Kwasababu kila mmoja anakimbia ! ndio msingi wa kusema hakuna anayechukua dhamana. Sidhani kama unaweza kunieleza
Kupitia tamko rasmi la Bunge mwenye dhamana ni Bunge kupitia PAC. Bunge ni taasisi mawasiliano.
kuchukua maandishi kutoka kwenye Magazeti au mitandao na kuyafanya ni maelezo ya Bunge inakuwa ni kununua udaku.
Ni kweli kabisa, lakini mawasiliano gani ikiwa hawakuweza kueleza tofauti ya mkataba na maelezo ya kina.
Kitu kinachoitwa maelezo ya kina kinasemwajwe kwa neno moja?
Mwasiliano yalikuwa wapi hadi kamati ya PAC ikaenda kudai mbele ya vyombo vya habari?
Nimekuambia, wiki nne siyo mbali, tusubiri ukweli utufikie kutoka kwenye chombo kilichopewa kazi kisheria ambacho ni Kamati Ndogo ya Bunge.
OK si kamati ya ulinzi , usalama na mambo ya nje? Si PCCB? Si serikali?
Sasa kama ulishahitimisha fikra zako kuhusiana na utendaji wa Serikali, kwa nini unahangaika na masuala ambayo ulishayafahamu?
Ili kukabiliana na washangiliaji wanaopotosha umma, wanaotaka umma uamini mambo safi, wanaosema uongo.
Ni kosa kukaa kimya umma ukibababishwa kwa mapambio ukweli ukifichwa
Mtu mwenye hekima na busara angesubiri baada ya 2020 kwa sababu anafahamu huu utawala hauna jipya.
Watu kama mimi tungebaki na matumaini yetu kwa sababu tunaamini we are at war with the army we have (Rais Magufuli), not the army you might want or wish to have at your irrational thoughts and ideas!
Nani kaukupoka matumaini mkuu? Endelea na matumaini wala usiahangaike na watu kama sisi. Jenga matumaini kwa nafsi na nafasi yako. Ni haki yako kikatiba na kibainadamu. Kuishi kwa matumaini hata kama ni mkate wa mawe! Hapa unatusingizia kufifisha matumaini yako! Si kweli. Kazi uzi mkuu
Well, 2005 walikuwa na matumaini kama wewe!
Mwaka jana wengine wakasema hali ya nchi ni njema kuelekea uchumi wa kati.
Mwaka huu wakasema hali ilifika pabaya sana
Wanaweza kusema hayo kwasababu wakipiga zumari wanaoitikia wengi hata kama hawajui wimbo wa zumari.
Wengine tunasema hapana, si suala la 'vita' tu, bali majemadari wa vita,nia , dhamira na mkakati. Vita haipiganwi kwa kubeba magobole na kwenda kichakani tu
Jeshi lililoshindwa miaka 20 na majemadari wale wale ni unlikely linaweza kuja na kitu kipya. Tatizo letu si vita, ni ni nia na dhamira ya vita, wapiganaji na mkakati
Jambo zuri ndani ya hekma zako huwezi kujibu hoja. Mimi nitasimama katika hoja nikiamini njia bora na matumizi sahihi ya ubongo ni kufikiri, kuhoji na kutaka kuelewa.
Kuendelea kukosoa serikali uliyosema toka siku ya kwanza haina jipya huku umejificha katika vazi la uzalendo ni kuendeleza unafiki tu au kupoteza muda wako adhimu.
Hapana suala la muda ni jambo binafsi na sioni linajibu vipi Lugumi.
Wengine tunasimama na Taifa kwanza kabla ya mtu au watu.
Kama kuhoji, kutoa maoni ni unafiki naafiki niwe hivyo na hakika najivunia hilo kuliko kujificha katika tumbo nikijua masilahi mapana ya Taifa yapo matatani
Ukweli wa Mkataba wanaofahamu ni polisi na Lugumu.
Hewalaa, ni mkataba wa umma, penye utata nini kinafichwa? Halafu una uhakika gani kama Polisi wanao?
Kwani kazi ilitolewa na nani? Nani mlipaji ? Mkataba ulisemaje kuhusu vifaa? tenda ilipatikanaje? Nani walishiriki?
Kwa hiyo unataka kutuambia unafahamu yote kuhusiana na mkataba wa polisi na Lugumi?
Sijui kabisa, ndio maana nashangaa kwanini mwezi mzima kuna kutupiana mpira, na baada ya wiki takribani tatu 'mwenye makataba' kwa mujibu wako anakuja na maswali badala ya majibu?
Unanunuaje kifaa eneo lisilo na internet?
Nani ali plan huu mradi? Nani aliidhinisha mradi huo? Wataalam gani walishiriki?
Kumbuka kama mlipa kodi na mwajiri wa serikali nina haki ya kuuliza
Huu
ni mtazamo wako ambao hauwezi kuwa ni sheria au mwanvuli kwa kila mwananchi.
Wapi mtazamo waangu nimeuita sharia au mwamvuli kwa wananchi?
Eti tutashindwa mahala pa kusimama. Huoni kama kusema tutashindwa pa kusimama ina maana kuwa kwa sasa tuna mahali pa kusimama au kwa maana nyingine unasema, The President is doing fantastic job.
Bandarini chereko, TRA chereko, Darajani kicheko, wafanyakazi hewa nderemo. Lugumi kimyaaa!
Lugumi imepelekwa ligi daraja la pili.
Ndio maana tunasema double std ni dalili njema za mbio kufikia ukingoni
Si kwa mujibu wa kauli zangu, bali wananchi wana akili za kupambanua
Kama mimi ni mshangiliaji, wewe ni nani?
Mimi jinga Fulani linalohoji mambo yasitokiwa. Nafiki Fulani lisilokubali kuimba wengine wakiserebuka.
Na puuzi Fulani lani tu linalotaka kudadisi dadisi kila kitu
Mkuu hoja zinajibiwa kwa hoja, nashangaa siku zote umekataa lugha tashtiti , mambo yakielemea unanyua silaha hiyo ambayo ni rahisi kuitumia. Haihitaji elimu au fikra
Huko siendi, lakini sitasita kutoa maoni hata kama yanachoma! au ungeshaurije mkuu!