IGP Mangu: Lugumi ilitekeleza mkataba wake na Jeshi la Polisi

IGP Mangu: Lugumi ilitekeleza mkataba wake na Jeshi la Polisi

Hata Kama wangepeleka Asikari wote kusomea hizo mashine isingefika hizo gharama kubali ukatae kuwa pesa nyingi imepigwa kupitia huo mladi wa kifisadi.

= mradi

Tupe mchanganuo wa huo mradi tafadhali.

Nnaona hauelewi kuwa pia kuna kitu kinaitwa software katika mambo kama hayo ili kuwezesha kazi iliyokusudiwa ifanyike. Jee, unaijuwa thamani yake hiyo software inayotumika hapo?

Pia ungetumia akili japo kiduchu, kuna vitu vinaitwa, planning, designing, mobilization, demobilization, installation, testing, commissioning, training, after sales service, warranties, guarantees. Unajuwa thamani yake yote hayo? Au ulifikiri mradi kama huo ni kwenda kununuwa ugoro na kubugia?

Ooh Isitoshe, pia kuna kitu kinachoitwa profit margin. Au ulifikiri hiyo ilikuwa ni sadaka?

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
 
....kila kimoja kiligharimu 343 million....!/
TUJARIBU KUGOOGLE BEI ZAKE
CHINA , UK ,U.S , FRANCE.
KILA KAMOJA HAKAZIDI LAKI 600000/- na hapo nimemaximase Juu mno,bei halisi ni ~20$-120$@.
centraliser pamoja na minara ya kukontral vijimashine vyote katika ku-access Info's au kulinganisha taarifa na KUZIHIFADHI haizidi $ 150,000/-.
 
Kwa ghalama ya huo mradi na unyeti wake wa nini wategemee Internet ili kuwa connected.
Nadhani intranet ingewafaa zaidi
 
Si kuna kamati ndogo ya PAC imeundwa kupita kila kituo kuona kama mashine hizo zipo zilifungwa na kufanya kazi, au?

Anajihami kwa lipi ndugu IGP? Awasubirie wanakamati huko huko kwenye vituo vyake na kuwaonesha hizo mashine.

Hata kama Lugumi hakuwa amezifunga, wamwambie afanye fasta kuzifunga kabla kamati haijawafikia. Hata hivyo akumbuke tu kuwa, siku zote siku za mwizi ni 39 ya 40 ananaswa!!
Sasa hivi hatuna Bunge. Bunge lavsasa ni sehemu ya vitengo au wizara zilizopo chini ya Ikulu.
 
....kila kimoja kiligharimu 343 million....!/
TUJARIBU KUGOOGLE BEI ZAKE
CHINA , UK ,U.S , FRANCE.
KILA KAMOJA HAKAZIDI LAKI 600000/- na hapo nimemaximase Juu mno,bei halisi ni ~20$-120$@.
centraliser pamoja na minara ya kukontral vijimashine vyote katika ku-access Info's au kulinganisha taarifa haizidj $ 150,000/-.
Hivyo vifaa Thamani yake ni ndogo sana haifiki hata bilion 1 ina maana billion zingine zote zimepigwa na sasa zinatumika kuficha JIPU lisitumbuliwe
 
Jambo la lugumi lipo kisiasa tu na inawezekana yanayosemwa yote yasiwepo mfano ilizuka taarifa katoroka siku mbili zinakanushwa na mhusika
 
Mmmmh funza wewe ni Mkurya? Kwenye "r" unawekaje "l" na panapohitaji "l" unawekaje "r"? Ukweli mradi wa LugumiPolisi ni wizi mtupu na hela yote hiyo imeingia mfukoni mwa familia mbili ambazo ni DUGU MOYA! Nizitaje? JIONGEZE NA WEWE!! Sasa huyu naye anaropoka hadharani? Ina maana kamati ya bunge ni waongo? MAGUFULI NJOO HUKU KUNA JIPU LIMEIVA! Anafikri bado ni wakati wa "business as usual?"
poa mkuu kifimbo cheza sisi huku Uganda kiswahili kimeanza kututupa mkono lakini 9 na 10 lengo ni kuwajuza kuwa pesa ya Lugumi 80% imepigwa yaani imeliwa na wajanja wachache.
 
Mtu
Mkuu wa Jeshi la Polisi – Inspekta Jenerali (IGP), Ernest Mangu amekanusha madai ya wabunge na hata taarifa zinazosambaa mitandaoni na kwenye vyombo vya habari kuhusu kampuni ya Lugumi kushindwa kufunga mashine kwenye vituo vya Polisi 108 kama mkataba wake ulivyomtaka.

Akizungumza mwishoni mwa wiki, IGP Mangu alisema anashangazwa na habari hizo na kueleza kuwa kampuni ya Lugumi ilitekeleza mradi wa kufunga mashine hizo kama ilivyokubaliana na serikali.

“Siyo kweli, watu wana ugomvi wao, lakini nakueleza wazi kwamba, tembelea vituo vyote tulivyokubaliana, utakuta mashine zipo. Inawezekana zingine hazifanyi kazi kwa sababu ya kukosekana kwa intaneti,” aliongeza mkuu huyo wa polisi.

Alipoulizwa mwenye jukumu la kufunga mtandao wa intaneti ni nani, IGP alijibu, “...ni TTCL (Kamuni ya Simu) ingawa sehemu nyingi ofisi zetu zimekatiwa huduma hiyo kwa kuwa jeshi halijalipa.”

Mtu akiichoka kazi si lazima aandike barua!!
 
Sasa wanawekaje vifaa vinavyohitaji internet kwenye vituo ambavyo havina internet?hapa ni jipu, aliyebuni mradi huo kabla ya kuhakikisha internet inapatikana ndio jipu lenyewe.

Mbona mitandao ya simu hipo mpaka vijijini, kwa nini hawatumii kuconnect na Internet hata kama speed ya Internet ni ndogo kuna njia lukuki za kui boost.
 
Mimi sijui kwa nini Afande Magu anajipa pressure ya bure?

Kwa nini hataki kusuburi taarifa za kamati ndogo ya Bunge iliyo pewa jukumu ya kuchunguza kwa kina kuhusu mwenendo/utekelezaji wa mradi wenyewe, haiwezekani CAG na Kamati ya Bunge waseme kuna tatizo somewhere yeye aseme kila kitu balabala - mtu mmoja anawezaje kupingana na kauli za watu wengi wengine wana uelewa mkubwa kwenye masuala ya IT sio mbumbumbu kivile, yeye kama kiongozi mkuu wa jeshi la Polisi alipashwa kutumia a diplomatic language kwamba kwa muda huu awezi kusema lolote mpaka Tume ikamilishe uchunguzi wake wakina, basi, oh yes 'NO COMMENT' would've been an ideal answer.
 
....kila kimoja kiligharimu 343 million....!/
TUJARIBU KUGOOGLE BEI ZAKE
CHINA , UK ,U.S , FRANCE.
KILA KAMOJA HAKAZIDI LAKI 600000/- na hapo nimemaximase Juu mno,bei halisi ni ~20$-120$@.
centraliser pamoja na minara ya kukontral vijimashine vyote katika ku-access Info's au kulinganisha taarifa na KUZIHIFADHI haizidi $ 150,000/-.
Aisee! Kitakuwa cha Ujerumani au Canada.
 
Hata Kama wangepeleka Asikari wote kusomea hizo mashine isingefika hizo gharama kubali ukatae kuwa pesa nyingi imepigwa kupitia huo mladi wa kifisadi.
Wewe unapoteza muda kubishana na huyo bibi alielelewa kwa ela za kifisadi? Huyu haamini kama kuna wizi nchi hii
 
Kwa jinsi mlivyokuwa mnapasiana ile ripoti tulijua mlikuwa mnatengeneza mikakati ya kuwasafisha WASTAAFU. Kila la heri kwa alieshika kijiti sasa sie yetu macho tu.
 
Ukisoma vizuri hii mada utaona kuwa hadi hii leo sehemu nyingine zilizofungwa hizo mashine hakuna hata access ya Internet, sasa elezea watajifunzaje online hata kama ni bure.

Nnashauri saa nyingine utumie kichwa chako kufikiri japo kiduchu na si kukiwacha kama mzigo tu juu ya mabega yako.
Kukiwacha=kukiacha
 
Back
Top Bottom