Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,096
- 4,948
IGP upo katika kipindi ambacho serikali inakuhitaji kuliko wakati wowote. Watangulizi wako pamoja na wewe mmekuwa mkiomba bajeti ya kuboresha makazi ya askari bila mafanikio kwa miaka mingi. Lakini kila inapofika kipindi cha uchaguzi watu wale wale wasiokuwa na fedha ya kukusaidia kuboresha makazi ya watumishi wako utangaza na kupitisha mabilioni ya fedha kukutumia uwasaidie kwenye tendo la kisiasa.
Skiatai kwamba uchaguzi ni gharama ila naamini askari anachohitaji si fedha anahitaji jambo ambalo linampa hadhi na furaha. Mimi kwa mtizamo wangu, askari angependa kulea familia yake kama wanavyolea watumishi wengine wa bandari, TAkukuru, TRA na taasisi nyingine. Makazi ya watumishi wa taasisi nilizotaja yanaakisi fikra na mnunurisho ndani ya miyoyo yao na miyoyo ya familia zao. Makazi hayo yanawapa faragha na kuwafanya wawe na amani makazini.
Nakubali kwamba yapo maeneo askari wana makazi bora ikiwemo baadhi ya miji kama Dar, ila pia yapo makazi duni yaliyojengwa na mkoloni; naamini pia zipo familia za askari wanaishi chumba na sebule hata katika miji mikubwa.
Niwapongeze wapiganaji hawa kwa kuheshimu kiapo chao lakini nitumie fursa hii na jukwaa letu kuwafikirisha zaidi viongozi wa jeshi letu pamoja na viongozi wa kisiasa.
Mhe. Rais ameingia kusaka bilioni 125 kama mlivyoomba. Sijui fedha hizo mmesema zinakwenda kusaidia nini ila niwaombe pamoja na vipaombele vyote mlivyompa , kama kipaombele cha nyumba za askari siyo sehemu ya mkakati wenu kusimamia uchaguzi mtakuwa mmekosea sana.
Nikipiga mahesabu hizi fedha endapo mtawalipa posho sidhani kama kuna askari wa chini atalipwa jumla ya laki tano kwa chaguzi zote mbili yaani 2024 na 2025. Ila mkifanya maamuzi kwamba mnawanyima wengi posho mnawapatia wachache makazi I hope hii itasaidia hao wachache na watoto wao lakini pia itawasaidia wapiga kura kuepukana na treatment zisizo na staha kwa sababu mtu mwenye furaha ya nafsi utoa huduma yenye kiwango.
Viongozi wa jeshi la polisi, kupitia tafakuri hii; trudini kwa mama mkamwombe awape japo 50% ya fedha za uchaguzi mkarabati miundombinu ya makazi ya wale askari wadogo wanaokwenda kusimamia uchaguzi.
Bilioni 62 kwa mikoa tuseme kumi ni sawa na kutenga kiasi cha bilioni sita za ukarabati na ujenzi kwa kila mkoa.
Ni mimi mtetezi wa walinzi wetu; kambale wa Mwanza ahsanteni