IGP mstaafu Simon Sirro Kuagwa rasmi na Jeshi la Polisi

IGP mstaafu Simon Sirro Kuagwa rasmi na Jeshi la Polisi

Jeshi la Polisi limetangaza kwamba IGP mstaafu ataagwa rasmi kesho na Jeshi hilo kwenye hafla itakayofanyika kwenye viwanja vya chuo cha Polisi Kurasini mkoani Dar es Salaam

Msemaji wa Polisi amewaambia Waandishi wa Habari kwamba sherehe za kumuaga Sirro ambaye sasa ni balozi wa Tanzania nchini zimbabwe zitaanza saa 1 asubuhi kwa gwaride maalum .

Simon Sirro atakumbukwa milele kwa upelelezi wake kabambe kwenye sakata la kutekwa kwa mfanyabiashara Mohamed Dewji , pale alipotumia intelijensia kabambe na kukamata gari lililotumiwa na wale Wazungu wawili waliomteka MO

View attachment 2615927

Tunamtakia kila la heri .

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
Watu walikamatwa? Ulijuwaje kuwa ni "wazungu" ?
 
Alichofanya kijijini kwao ni kujenga kanisa, hopeless
 
Huyu IGP Namtakia ustaafu mwema amepitia misukosuko ambayo inabakia Kuwa fundisho Kwa wanadamu hata ule msemo wa tenda wema nenda zako unasimama.
Alipitia katika msimamo wa kutenda haki akiwa RPC MWANZA na alisimama katikati kuhakikisha matokeo ya uchaguzi yanatangazwa kama yalivyo lakini baada ya Mafanikio hayo akatengwa na alipitia magumu mengi hapo ndiyo naona fundisho nililolikusudia linapatikana namnukuu alipokuwa ana hojiwa na Kituo kimoja cha Television alisema katika KAZI za Polisi huwezi ukapendwa na watu wote kwasababu unapomkamata Mwizi familia ya Mwizi itakuchukia lakini walioibiwa hawatakuchukia.
Alipoteuliwa Kuwa IGP ni wazi isingekuwa rahisi kupendwa na watu wote lakini hakurudia Yale Makosa aliyoyafanya pale Mwanza ndiyo maana alionekana ni mtu tofauti hata alivyokuwa anafokewa na Mkuu wa Mkoa alihimili vishindo na kufanikiwa kuteuliwa.
Kumbe hata kama unaubabe au ujanja nk.unatakiwa kumtumikia kafiri,Sijajua hapa mwishoni nini kilimtokea Kwa jinsi alivyolipambania Taifa akazawadiwa ubalozi ! Pia SIELEWI kilichomtokea Mwanza kimegeuzwa kinyume chake au nini? Anyway wao wanajua zaidi la Muhimu katika maisha ni kutenda haki Kwa kadri ya uwezo wako wote.
 
IGP pekee aliyekuwa na weledi na akili nzuri kabisa lakini baadaye akadhihirisha kuwa akili pekee siyo kigezo cha kushindwa kutumikishwa na wanasiasa waliokosa akili na weledi.
 
Jeshi la Polisi limetangaza kwamba IGP mstaafu ataagwa rasmi kesho na Jeshi hilo kwenye hafla itakayofanyika kwenye viwanja vya chuo cha Polisi Kurasini mkoani Dar es Salaam

Msemaji wa Polisi amewaambia Waandishi wa Habari kwamba sherehe za kumuaga Sirro ambaye sasa ni balozi wa Tanzania nchini zimbabwe zitaanza saa 1 asubuhi kwa gwaride maalum .

Simon Sirro atakumbukwa milele kwa upelelezi wake kabambe kwenye sakata la kutekwa kwa mfanyabiashara Mohamed Dewji , pale alipotumia intelijensia kabambe na kukamata gari lililotumiwa na wale Wazungu wawili waliomteka MO

View attachment 2615927

Tunamtakia kila la heri .

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
Picha inaeleweka. Simon Sirro alisema Mo amepatikana. Halafu akaongeza kusema,"Kwa nini unataka kutugombanisha na majeshi mengine"?
Ina maana lipo jeshi lingine hapa lilimteka Mo,jambo ambalo halikumpendeza Kamanda Sirro.
 
Nimeona kwa millard hii kitu, kichwa cha habari kimenishtua nikajua amedead

Pumzika kwa amani na furaha bwana sirro
 
Kweli nchi hii sijui lini tutaamka na kujifunua hili blanketi la ujinga. Mheshimiwa IGP mstaafu ameondoka kwenye utumishi wa jeshi la polisi aliloliongoza zaidi ya miaka sita na kuzawadiwa vitu mbalimbali likiwemo gari la kifahari huku akiendelea kufaidi pension hadi kifo chake, lakini anaondoka bila kuwajibishwa kupata ukweli wa mabilioni yaliyopigwa mfuko wa kufa na kuzikana?

Tumelala au tu maiti kama marehemu Rais Kenyatta alivyomwambia mwl unaongoza maiti.

Kwa mtindo huu nani atakuwa madarakani aogope kufanya ufisadi? Tumelogwa!

20230511_111418.jpg
 
Back
Top Bottom