IGP mstaafu Simon Sirro Kuagwa rasmi na Jeshi la Polisi

Watu walikamatwa? Ulijuwaje kuwa ni "wazungu" ?
 
Alichofanya kijijini kwao ni kujenga kanisa, hopeless
 
Unajenga kanisa kisha unamiki bar 50 kidogo? Unauwa, kushambulia na kuteka watu?
Na nyumba ndogo kadhaa, kakiwemo kale ka afande ka Morogoro, akakapa na cheo ngazi ya wilaya
 
Huyu IGP Namtakia ustaafu mwema amepitia misukosuko ambayo inabakia Kuwa fundisho Kwa wanadamu hata ule msemo wa tenda wema nenda zako unasimama.
Alipitia katika msimamo wa kutenda haki akiwa RPC MWANZA na alisimama katikati kuhakikisha matokeo ya uchaguzi yanatangazwa kama yalivyo lakini baada ya Mafanikio hayo akatengwa na alipitia magumu mengi hapo ndiyo naona fundisho nililolikusudia linapatikana namnukuu alipokuwa ana hojiwa na Kituo kimoja cha Television alisema katika KAZI za Polisi huwezi ukapendwa na watu wote kwasababu unapomkamata Mwizi familia ya Mwizi itakuchukia lakini walioibiwa hawatakuchukia.
Alipoteuliwa Kuwa IGP ni wazi isingekuwa rahisi kupendwa na watu wote lakini hakurudia Yale Makosa aliyoyafanya pale Mwanza ndiyo maana alionekana ni mtu tofauti hata alivyokuwa anafokewa na Mkuu wa Mkoa alihimili vishindo na kufanikiwa kuteuliwa.
Kumbe hata kama unaubabe au ujanja nk.unatakiwa kumtumikia kafiri,Sijajua hapa mwishoni nini kilimtokea Kwa jinsi alivyolipambania Taifa akazawadiwa ubalozi ! Pia SIELEWI kilichomtokea Mwanza kimegeuzwa kinyume chake au nini? Anyway wao wanajua zaidi la Muhimu katika maisha ni kutenda haki Kwa kadri ya uwezo wako wote.
 
IGP pekee aliyekuwa na weledi na akili nzuri kabisa lakini baadaye akadhihirisha kuwa akili pekee siyo kigezo cha kushindwa kutumikishwa na wanasiasa waliokosa akili na weledi.
 
Picha inaeleweka. Simon Sirro alisema Mo amepatikana. Halafu akaongeza kusema,"Kwa nini unataka kutugombanisha na majeshi mengine"?
Ina maana lipo jeshi lingine hapa lilimteka Mo,jambo ambalo halikumpendeza Kamanda Sirro.
 
Nimeona kwa millard hii kitu, kichwa cha habari kimenishtua nikajua amedead

Pumzika kwa amani na furaha bwana sirro
 
Kweli nchi hii sijui lini tutaamka na kujifunua hili blanketi la ujinga. Mheshimiwa IGP mstaafu ameondoka kwenye utumishi wa jeshi la polisi aliloliongoza zaidi ya miaka sita na kuzawadiwa vitu mbalimbali likiwemo gari la kifahari huku akiendelea kufaidi pension hadi kifo chake, lakini anaondoka bila kuwajibishwa kupata ukweli wa mabilioni yaliyopigwa mfuko wa kufa na kuzikana?

Tumelala au tu maiti kama marehemu Rais Kenyatta alivyomwambia mwl unaongoza maiti.

Kwa mtindo huu nani atakuwa madarakani aogope kufanya ufisadi? Tumelogwa!

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…