Uchaguzi 2020 IGP Simon Sirro asema hali katika Vituo vya Kupigia kura ni shwari

Uchaguzi 2020 IGP Simon Sirro asema hali katika Vituo vya Kupigia kura ni shwari

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro amesema ametembelea Vituo kadhaa vya kupigia kura na hali ni shwari, jambo linaloashiria Watanzania wanaelewa umuhimi wa siku ya leo.

Ameomba utulivu ambao umeanza uendelee mpaka pale kura zitakapomaliza kupigwa na hatimaye matokeo kutolewa.

Ameeleza, "Najua wakati wa matokeo yanatolewa ndio baadhi ya watu hupata mihemko, na mihemko huwa haina tija. Atakayechaguliwa kuwa Kiongozi wako huyo huyo atakusaidia kuhakikisha nchi yetu inakuwa na maendeleo"

 
Wasiliana na kule Kilimanjaro,RPC Jana saa sita usiku alitumia hekima na busara kumnusuru DED wa halmashauri ya Moshi, baada ya kukataa kuwapa mawakala wa chadema barua zao. Hongera RPC Kilimanjaro tenda Haki Mungu atakulinda.
 
Zile kura zaTume zilizofichwa Chini ya Meza Sirro hajaziona.
 
Nikupongeze IGP na Jeshi la Polisi kwa kazi nzuri.
 
Kweli nimeamni uchaguzi ni sayansi na mtaji wa CCM ni Akina mama maana nimeenda kupiga kura almost wakati napiga kura maana vituo vina namba kila nilipo kuwa nikipiga macho naona akina mama ndo wengi na akina baba wa umri wa kuanzia 50 and above ndo wanamiminika vijana wa mihemko kwenye campaign za CCM na Chadema ni hakuna au ni wa kuhesabu tofauti na akina mama CCM inatashinda uchaghuzi kwa difference kubwa sana. Peoplezzzzz
 
Hivi hii kauli kwamba kiongozi 'atakuletea maendeleo' tuliipata wapi, mbona ni kauli ya kijinga sana!
 
Kwenye Kupiga Kura hali itakuwa shwari na Salama kabisa, ila kwenye kuhesabu na kwenye kutangazwa matokeo ndio hali ya hewa itakapo Badilika na kuwa sio Shwari itakuwa Shari bin dhahama.
 
Back
Top Bottom