IGP Simon Sirro; madaraka hupita, toba hutengeneza mwisho mwema

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2018
Posts
539
Reaction score
3,507
Nadhani ipo nafasi ukitika katika utumishi unachobaki nacho ni kama binadamu mwenye imani kwamba Mungu yupo nikumshukuru Mungu nakuendelea kumtukuza kwa uhai na madaraka uliyopewa.

Ukipewa madaraka, ukapewa maarifa ya mema na mabaya, ukapewa maarifa ya kujua pumzi si mali itokayo kwa mwanadamu bali kwa Mungu, basi utaheshimu kila nafsi ulilokabidhiwa kuilinda.

Nimemsikiliza mzee Sirro kauli yake dhidi ya Lissu, nimeumia kwamba uhai wa mwanadamu umepewa nafasi ndogo kuliko mshahara na ulinzi wa smg. Natamani viongozi waache kuona mshahara, waone Taifa na kuwaona binadamu.

Hiki alichokitamka huyu mzee kwa umri wake na kwa kutoshurutishwa na mtu naamini hakitoishi masikioni mwake. Ametenda kosa ambalo linawanufaisha wanasiasa lakini linachipa na kuimomonyoa nafsi yake hasa pale anapokuwa kwenye binafsi na ambayo anakwenda kuyaanza hivi karibuni.

Nimeumia kwa aina hii ya viongozi.
 
Siro anaangalia upande utakaomlindia mlo wake akistaafu. Ila Siro ameshiriki uchafu mwingi chini ya utawala wa yule mtu muovu, anachofanya sasa ni kuendelea kulinda alichosimamia muda wote.
 
Nchi yetu imeshakuwa kama fumbo la Imani
Aiseh kweli Mungu ni wa kutumainiwa milele
 
Hukumu ya Mungu inamsubiri kwa udhalimu alioufumbia/alioshiriki kwa nafasi yake.

Mungu hadhihakiwi.
 
Mzee SIRRO Damu ya LISSU itakulilia mpaka KABURINI kwako umeshindwa Kujitoa kwenye Mtengo clio Tegewa na MUUAJI kwa kuamini Madaraka na Mshahara Ukasahau anatoa ROHO ni yule Aliyewaumba
 
"Lissu anatumia kilema alichonacho kupata fadhila za wazungu".

HII KAULI, KAULI HII! Haitakuacha salama Sirro. Iwe Leo duniani au kesho ahera, hutakuwa salama kwa kukejeli kilema cha mwenzio kilichosababishwa na watu unaowajua.

Yaani Lissu afurahie kuwa kilema kuliko kuwa mzima? Kwahiyo unaungana na kina Musiba walioitisha press conference na kusema Lissu hakupigwa risasi za moto bali risasi baridi (blanks)? Na wewe unatuletea jambo jipya kwamba Lissu yuko kwenye hali hiyo kwa kupenda kwake?

Yaani amefanyiwa operesheni zaidi ya 20 mwilini mwake ili tu apate ufadhili?

KWAMBA; Amukuwa tayari kuishi akitobolewa mwili, kuvunjwa mifupa na kuwekewa vyuma ili apate kufadhiliwa na Wazungu?

SIRRO! Tema mate chini braza, wewe ni Mkristo Mkatoliki si mpagani. Kumbuka ukuu wa Mungu na maelekezo yake kwa watu wake kuhusu huruma na upendo.

UNAJIMALIZA KIIMANI NA KIBINADAMU.
 
Makelele yote Yale ya Lisu hakuyasikia? Mbona hatujamsikia anaongea chochote akiwa kiongozi wa walinda amani ya taifa anavyosema. Ndani ya nyumba mtu mmoja akijeruhiwa lazima watu wajiulize kuna Nini?

Kama ni makelele watanzania walisikia na ni mashahidi hata mbele ya mungu. Hata waliokuwa mahutihuti mahosptalini na watoto wachanga walisikia sauti ya Lisu.

Watanzania tujifunze kuwa wakweli. Huu muhimili sio wa mchezo kwa kweli. Hata Mimi majibu ya Sirro kuhusu Lissu yameniumiza.

Sirro akumbuke yeye ni kiongozi wa ulinzi na usalama wa taifa na nimpatanishi wa pande zote na kurekebisha kitabia. Akubali kukaa na Lissu wayajenge.
 
Dah! Mbona ana roho mbaya hivi? Anyway sishangai sana kwasababu Askari wengi hawana akili,hawawazi mbali,na wakistaafu huwa wanaishia kuwa na maisha mabaya Sana,na kisha kufa ktk hali mbaya.
 
Nadhani ipo nafasi ukitika katika utumishi unachobaki nacho ni kama binadamu mwenye imani kwamba Mungu yupo nikumshukuru Mungu nakuendelea kumtukuza kwa uhai na madaraka uliyopewa.

Ukipewa madaraka, ukapewa maarifa ya mema na mabaya, ukapewa maarifa ya kujua pumzi si mali itokayo kwa mwanadamu bali kwa Mungu, basi utaheshimu kila nafsi ulilokabidhiwa kuilinda.

Nimemsikiliza mzee Sirro kauli yake dhidi ya Lissu, nimeumia kwamba uhai wa mwanadamu umepewa nafasi ndogo kuliko mshahara na ulinzi wa smg. Natamani viongozi waache kuona mshahara, waone Taifa na kuwaona binadamu.

Hiki alichokitamka huyu mzee kwa umri wake na kwa kutoshurutishwa na mtu naamini hakitoishi masikioni mwake. Ametenda kosa ambalo linawanufaisha wanasiasa lakini linachipa na kuimomonyoa nafsi yake hasa pale anapokuwa kwenye binafsi na ambayo anakwenda kuyaanza hivi karibuni.

Nimeumia kwa aina hii ya viongozi
Huyu mzee alishiriki kwa 100% kwenye tukio la Lisu
 
Makelele yote Yale ya Lisu hakuyasikia? Mbona hatujamsikia anaongea chochote akiwa kiongozi wa walinda amani ya taifa anavyosema. Ndani ya nyumba mtu mmoja akijeruhiwa lazima watu wajiulize kuna Nini?

Kama ni makelele watanzania walisikia na ni mashahidi hata mbele ya mungu. Hata waliokuwa mahutihuti mahosptalini na watoto wachanga walisikia sauti ya Lisu.

Watanzania tujifunze kuwa wakweli. Huu muhimili sio wa mchezo kwa kweli. Hata Mimi majibu ya Sirro kuhusu Lissu yameniumiza.

Sirro akumbuke yeye ni kiongozi wa ulinzi na usalama wa taifa na nimpatanishi wa pande zote na kurekebisha kitabia. Akubali kukaa na Lissu wayajenge.
Haya ni matokeo ya kuwa na katiba mbovu
 
Back
Top Bottom